Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,920
- 15,607
Wadau ni wazi kuwa katika maisha yetu ya kisasa, kina dada wengi huwa wanawachukia wakwe zao wa kike na wifi zao, hasa pale Mama wa Mume anapoona kachoka na hivyo angehitaji kuishi kwa mwanawe wa kiume ili kupata matunzo na uangalizi wa karibu lakini pia kufurahia matunda ya jasho lake katika kumlea mtoto wake wa kiume.
Itokeapo hilo, basi migogoro, mikwaruzano na bifu babu kubwa hutokea kati ya Mke na Mama mkwe. Kwa bifu zile zilivyo, hivi inapotokea wifi au Mama mkwe kufariki nyie kina dada huwa kweli mnahuzunika kwa misiba hiyo, au huwa mnaigiza tu kuhuzunika wakati moyoni moyoni mwasema bora hivyo?