Mahusiano Kati ya Kijana, Mama wa Kijana, dada wa Kijana na mke wa Kijana

baptist

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
426
255
Nimetafakari Sana Mahusiano ya watu tajwa hapo juu, Yan kabla ya kijana kuoa na baada ya kijana kuoa.

Katika uchunguzi wangu mdogo familia nyingi kabla ya kijana kuoa zinakuwaga na utulivu amani na upendo baina ya kijana, Mama wa kijana na (ma)dada wa Kijana.

Lakini baada ya kijana kuoa na kuanza maisha yake mapya ya ndoa, mahusiano haya hupukutika taratibu na mwisho kuishia kabisa au kubakia na upendo wa kinafki.

Unakuta mwanamke ameolewa na kijana Hana tatizo lolote na wakwe au mawifi zake tabia njema, ustaarabu, heshima utiii vyote anavyo, lakini muda unavyozidi kwenda kunakuwaga na chuki zisizo julikana hutokea wapi kutoka kwa mama wa kijana kwenda kwa mwali, au Dada wa Kijana kwenda kwa wifi yake huyo.

Hapa sijazungumzia upande wa mke mkorofi. Nimezungumzia upande wa mke mwenye utii, heshima,adabu na kila sifa impasayo kuwa nayo " wife material"

Vitaanza visa, mikasa, chuki uchonganishi wa ajabu ajabu hapo usiombe kijana awe ameoa halafu anakaa na mama yake Mzazi au dada nyumba moja.. Huyo mke Cha moto atakiona...

Najaribu kuwaza ni kwanini mama mkwe hajawahi kukubaliana na Hali ya kwamba kijana ameoa na ampende mwali wake upendo ule ule anaompa kijana wake.. maana kimsingi hawa wote ni watoto wake.

Hii chuki huenda mbali mpaka kwa watoto wa Kijana na watoto wa dada wa Kijana.. upendo wa Bibi Mara nyingi kwa hawa wajukuu zake Mara nyingi hauwezagi kuwa sawa lazima tunkwa kiasi fulan watoto wa dada wa Kijana watapendelewa zaidi..😔😔

Mwisho wa siku Kama kijana atashindwa kuwa na msimamo mkali na kuweka mipaka Kati ya pande hizi mbili (mama mkwe)mawifi na familia yake mpya) ndoa hii huvunjika kabisa.🤔🤔

Ni kwanini familia ya kijana inashindwa kabisa kumpokea binti anayeingia kwenye familia yao moja kwa moja bila hizi figisu.🤓🤓

Japokuwa kuna baadhi ya familia mambo ni shwari upendo baina ya pande zote mbili upo wa kutosha.

Karibuni tubadilishane mawazo wanajamvi, wengi tunapitia hizi changamoto na zinaumiza Sana.
 
Mimi binafsi nimejitahid kusuluhisha utata kati ya mke na mama yangu na ndugu zangu wote lakini mara kadhaa naishia kufeli na kuachana na mkewangu mpendwa na baada ya kufikiri kwa kina naamua kumrudia tena mkewangu nimeachana na kurudiana na mkewangu mara 4 kwa Sasa nimeamua niishi tu na mkewangu sitaki kabisa kusikiliza chokochoko za mama na nduguzangu wengine japo wao wanaamini nimewekewa limbwata na nimerogwa na mkewangu.

Lakini me sijali maana nampenda mkewangu namama nampenda pia na tayari mama yangu kesha nilaani kuwa kama naendelea kuwa na mkewangu basi yeye sie mama yangu na kwenye msiba wake nisikanyage. Kimsingi mama yangu anadai mkewangu ni maskini kwao kwahiyo mzigo wa majukumu utanielemea pia ananicheka eti sijui kuchagua wanawake wazuri basi nimeamua poa tu sasa ni miaka 5 bado mama yangu amekaza tuna mtoto wakike ana miaka 3 hamjui kabisa bibi yake kutokana na kutokuwepo kwa maelewano.
 
Haya yanatokea sana kwa wale wanao oa wakiwa bado hawana miji yao. Imagine unaoa unaishi na mkeo kwa wazazi wako lazima mambo kama hayo yatokee tena mapema tu.
Wapo ambao wanaishi kwenye miji yao na mambo ni hayo hutokea, kwa ufupi ni ujinga,ukosefu wa elimu ya utambuzi kwamba kutambua sasa kaka au mwanangu ana maisha yake nimuache aishi kivyake, na yote wanachoanzisha chuki na visa hasa kijana wao akiwa na vijisenti wanaona mke amekuja kukata mirija yao hivo mke ndio atakua anapewa nafas ya kipekee kwanza ndipo wao waje.

Kinachowaumiza ni chuki zisizo msingi kwa kuona tu ile nafas waliokua nayo sasa haipo na kaka lazima ajali familia yake ndipo wao waje.
 
Haya yanatokea sana kwa wale wanao oa wakiwa bado hawana miji yao. Imagine unaoa unaishi na mkeo kwa wazazi wako lazima mambo kama hayo yatokee tena mapema tu.
Inatokea pia kwa wale wenye miji yao ila wanaishi na dada zao na mama zao.

Mf: alikiba,diamond n.k
 
Inatokea pia kwa wale wenye miji yao ila wanaishi na dada zao na mama zao.

Mf: alikiba,diamond n.k

Yes ipo hivyo, mtu unaishi kwa kaka ameoa na yupo na familia yake kwenye mji wake alafu wanakuja ndugu zake wanataka muishi the way wanavyotaka/wanavyopenda wao lazima hali itabadilika tu.
 
wapo ambao wanaishi kwenye miji yao na mambo ni hayo hutokea, kwa ufupi ni ujinga,ukosefu wa elimu ya utambuzi kwamba kutambua sasa kaka au mwanangu ana maisha yake nimuache aishi kivyake, na yote wanachoanzisha chuki na visa hasa kijana wao akiwa na vijisenti wanaona mke amekuja kukata mirija yao hivo mke ndio atakua anapewa nafas ya kipekee kwanza ndipo wao waje

kinachowaumiza ni chuki zisizo msingi kwa kuona tu ile nafas waliokua nayo sasa haipo na kaka lazima ajali familia yake ndipo wao waje

Umeeleza vyema sana Madame, kuna watu wana chuki sana ndugu wengine hudiriki hata kufanya namna fulani ili tu kuwatenganisha ili wao wanufaike zaidi. Alafu kwa experience yangu hii hali ipo sana kwa ndugu wa kike wa bwana sijui sababu n nini?
 
Mimi binafsi nimejitahid kusuluhisha utata kati ya mke na mama yangu na ndugu zangu wote lakini mara kadhaa naishia kufeli na kuachana na mkewangu mpendwa na baada ya kufikiri kwa kina naamua kumrudia tena mkewangu nimeachana na kurudiana na mkewangu mara 4 kwa Sasa nimeamua niishi tu na mkewangu sitaki kabisa kusikiliza chokochoko za mama na nduguzangu wengine japo wao wanaamini nimewekewa limbwata na nimerogwa na mkewangu lakini me sijali maana nampenda mkewangu namama nampenda pia na tayari mama yangu kesha nilaani kuwa kama naendelea kuwa na mkewangu basi yeye sie mama yangu na kwenye msiba wake nisikanyage. Kimsingi mama yangu anadai mkewangu ni maskini kwao kwahiyo mzigo wa majukumu utanielemea pia ananicheka eti sijui kuchagua wanawake wazuri basi nimeamua poa tu sasa ni miaka 5 bado mama yangu amekaza tuna mtoto wakike ana miaka 3 hamjui kabisa bibi yake kutokana na kutokuwepo kwa maelewano
Kha wee jamaa hufai kabisa. Yaani umechagua mbususu over ur mother!

Huyo mwanamke angekutaka kweli kama mama yako asinge kuandaa kimaisha?
Ungreatful kabisa wewe
 
Wapo ambao wanaishi kwenye miji yao na mambo ni hayo hutokea, kwa ufupi ni ujinga,ukosefu wa elimu ya utambuzi kwamba kutambua sasa kaka au mwanangu ana maisha yake nimuache aishi kivyake, na yote wanachoanzisha chuki na visa hasa kijana wao akiwa na vijisenti wanaona mke amekuja kukata mirija yao hivo mke ndio atakua anapewa nafas ya kipekee kwanza ndipo wao waje.

Kinachowaumiza ni chuki zisizo msingi kwa kuona tu ile nafas waliokua nayo sasa haipo na kaka lazima ajali familia yake ndipo wao waje.
Na hii ndio haswaaa, no chuki za kijinga kuona kama mke ndio kaja kufaidi....
Agggrrrr to hell....
 
Umeeleza Vyema sana Madame, kuna watu wana chuki sana ndugu wengine hudiriki hata kufanya namna fulani ili tu kuwatenganisha ili wao wanufaike zaidi. Alafu kwa experience yangu hii hali ipo sana kwa ndugu wa kike wa bwana sijui sababu n nn?
Na hasa ndugu wa kike ambao olewa na hawana maisha ndo wanakuwaga na shida sana
 
Kuna jamaa yangu mmoja alivyoona figisu zimezidi akamwambia mama yake tafadhali maana naomba uniache na Mimi nifurahie maisha ya ndoa Kama wewe ulivyofaidi na baba yangu..
Kha wee jamaa hufai kabisa. Yaani umechagua mbususu over ur mother!

Huyo mwanamke angekutaka kweli kama mama yako asinge kuandaa kimaisha?
Ungreatful kabisa wewe
 
Back
Top Bottom