Hivi kifaru cha kijeshi kinaendeshwaje wakati kimefunikwa kote?

Yuda Legacy

JF-Expert Member
Jun 21, 2023
534
1,746
Kama kichwa cha habari kisemavyo na ni naomba radhi maana sijui jina lake fasaha ni lipi mimi toka utotoni nakiita kifaru,, tuendelee najua humu JF kuna wataalum wenye ujuzi mtujuze hivi kifaru cha jeshi kinaendeshwaje wakati hakina kioo cha mbele.

Na Je, anaendesha anamuonaje adui sasa mfano adui kakidandia kwa nyuma sasa anamuonaje

Mimi naona hamna silaha dhaifu kama kifaru cha jeshi maana kuuwawa ni dakika sifuri. Ukinipa gobole na kifaru kwangu Mimi nitachagua gobore Ila kifaru ni Silaha dhaifu aliebuni alishindwa ubunifu.

Screenshot_20240123-085851.jpg
 
Kama kichwa cha habari kisemavyo na ni naomba radhi maana sijui jina lake fasaha ni lipi mimi toka utotoni nakiita kifaru,, tuendelee najua humu jf kuna wataalum wenye ujuzi mtujuze hivi kifaru cha jeshi kinaendeshwaje wakati hakina kioo cha mbele.

Na Je anaendesha anamuonaje adui sasa mfano adui kakidandia kwa nyuma sasa anamuonaje

Mimi naona hamna Silaha dhaifu kama kifaru cha jeshi maana kuuwawa ni dk sifuri. Ukinipa gobole na kifaru kwangu Mimi nitachagua gobore Ila kifaru ni Silaha dhaifu aliebuni alishindwa ubunifu.
View attachment 2880170
Kina GPS na camera kibao, pamoja na hayo pia kuna sehemu kwa chini yenye kio kigumu dereva anapo angalia nje kwa mbele.
 
Sasa wewe uangalie Kamera alafu adui kabana chocho na Rpg zile za kudungua utapona kweli. Kwangu bado kifaru ndio Silaha dhaifu hata nikiwa na kisu adui ana kifaru mimi nammaliza
Vifaru vya kisasa ni mifumo ya kijeshi iliyoendelezwa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu. Wanajumuisha sifa kama:

1. Teknolojia ya Kielektroniki: Vifaru vya kisasa huwa na mifumo ya kielektroniki kama vile mifumo ya kompyuta, rada, na vifaa vya kuzuia mashambulizi ya kielektroniki.

2. Silaha za Mbali: Mara nyingi hujengwa na silaha za mbali kama vile makombora ya kudungua ndege au mashine za adui.

3. Nguvu za Kujikinga: Vifaru hivi vina mifumo ya kujikinga kama vile mifumo ya kuzuia makombora na vifaa vya kufyonza na kuvunja mizinga.

4. Udhibiti wa Mbali: Baadhi ya vifaru vya kisasa vinaweza kudhibitiwa kutoka kwa mbali, kuruhusu operesheni salama kwa walinzi.

5. Teknolojia ya Mawasiliano: Mifumo ya mawasiliano ya hali ya juu hukuruhusu vifaru kuwasiliana kwa ufanisi na vitengo vingine vya jeshi.

6. Nguvu na Uimara: Vifaru hivi vinaundwa kuwa na nguvu na uimara, na mara nyingine huwa na vifaa vya kujikinga dhidi ya milipuko.

Haya yote hufanya vifaru vya kisasa kuwa nguvu za kijeshi zenye ufanisi na za kisasa.
 
Sasa wewe uangalie Kamera alafu adui kabana chocho na Rpg zile za kudungua utapona kweli. Kwangu bado kifaru ndio Silaha dhaifu hata nikiwa na kisu adui ana kifaru mimi nammaliza
Kama vifaru vingekuwa silaha dhaifu vingekuwa vimeshaachwa siku nyingi. Vifaru vinatumika toka enzi na enzi na vimedhihirisha wazi kwamba ni zana za kuaminika za kivita. Ingia youtube kuna videos kibao za kuonyesha jinsi kifaru kinavyofanya kazi.
 
Ukiwa mwalimu kuna wakat huwa unajiuliza inakuaje umeme ukiwashwa unawaka kila sehem ndan ya muda mfupi bila kutegeana
Vivyohivyo hata kwenye hizo tank za kijesh(kifaru) wewe kama raia wa kawaida kuielewa ni ngumu ila wanaotumia wanaelewa faida yake
Matumizi yake pia
#Ila hata mimi natamani kujua namna kinafanya kazi.
 
Lakini Bado Sijashawishiwa Mimi kwangu Kifaru ni Silaha dhaifu... HEBU WAZIA KIFARU KUPIGA KWAKE MPAKA KIGEUZE ULE MZINGA WAKE ILI KUM FACE ADUI KUTOKANA NA ANGLE ALIYO KAA NDIO KIPIGE NA KUGEUZA KWAKE LILE LISHINGO LAKE KIPO SLOW KAMA MTU ANAE UMWA SHINGO....MAANA KIFARU HAKINA RISASI NI LILE LIMZINGA LAKE TU NDIO KINATEGEMEA.

SASA HUYO ADUI KASHIKA ULE MZINGA WA KUDUNGUA ATAKUWA ANAKUSUBIRI TU ULIEPO KWENYE KIFARU???
 
Vifaru vya kisasa ni mifumo ya kijeshi iliyoendelezwa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu. Wanajumuisha sifa kama:

1. Teknolojia ya Kielektroniki: Vifaru vya kisasa huwa na mifumo ya kielektroniki kama vile mifumo ya kompyuta, rada, na vifaa vya kuzuia mashambulizi ya kielektroniki.

2. Silaha za Mbali: Mara nyingi hujengwa na silaha za mbali kama vile makombora ya kudungua ndege au mashine za adui.

3. Nguvu za Kujikinga: Vifaru hivi vina mifumo ya kujikinga kama vile mifumo ya kuzuia makombora na vifaa vya kufyonza na kuvunja mizinga.

4. Udhibiti wa Mbali: Baadhi ya vifaru vya kisasa vinaweza kudhibitiwa kutoka kwa mbali, kuruhusu operesheni salama kwa walinzi.

5. Teknolojia ya Mawasiliano: Mifumo ya mawasiliano ya hali ya juu hukuruhusu vifaru kuwasiliana kwa ufanisi na vitengo vingine vya jeshi.

6. Nguvu na Uimara: Vifaru hivi vinaundwa kuwa na nguvu na uimara, na mara nyingine huwa na vifaa vya kujikinga dhidi ya milipuko.

Haya yote hufanya vifaru vya kisasa kuwa nguvu za kijeshi zenye ufanisi na za kisasa.
Je kifaru kinaweza kulipuliwa na silaha ya kawaida mfn smg au AK47?engine yake inatumia mafuta au gas au nishati gani?
 
Je kifaru kinaweza kulipuliwa na silaha ya kawaida mfn smg au AK47?engine yake inatumia mafuta au gas au nishati gani?
Vifaru vinatumia mafuta ya diesel ️.

Silaha ndogo kwa kawaida hazina uwezo wa kuharibu au kulipua vifaru.

Vifaru vina vifaa vya kujikinga kama vile mabati ya chuma na vifaa vya kuzuia milipuko.

Zinaweza kuwa na athari ndogo kwenye vifaru na mara nyingi hutumika zaidi dhidi ya wanajeshi wa ardhini.

Kuharibu au kudhuru vifaru, silaha kubwa kama vile makombora ya kudungua mizinga au mabomu yenye nguvu hutumika.
 
Kama vifaru(tanks) vingekuwa ni dhaifu visingetumika kwenye vita vikali!!
Hivi unajua gharama ya kifaru mfano hivi vya kwetu vya kizamani vya world war huko achilia mbali hivi vya kisasa??
Unajua ni kirahisirahisi kukilipua kifaru?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom