Hivi kazi ya mwanajeshi ni ipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kazi ya mwanajeshi ni ipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Obhusegwe, Jan 21, 2009.

 1. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Wajameni wandugu!

  Heshima mbele!!

  Mimi ni mpitaji wa hii barabara inayopita Lugalo kuelekea maeneo ya mbezi mpaka b.moyo. Karibu kila siku napita hapo nikielekea kwny kibarua changu.

  Cha kushangaza almost kila siku nikipita nakuta wanajeshi wakifyekafyeka na kuokotaokoa takataka karibu na barabara kwenye eneo lote la jeshi. Hii nimeiangalia kwa muda mrefu sana na nimeanza kujiuliza hivi kazi ya mwanajeshi(lets say daily routine) ni nini? Bado sijapenda kuamini kama ndo hiyo.. kama ileeeeee tuliyokuwa tunafanya kila siku asubuhi kwenye shule zetu za saint mapapai anzi zileeeeeeee!!!

  Je serikali haioni kama inabwetesha nguvu kazi? kwa nini jeshi lisifungue miradi ya kuwashirikisha hawa jamaa ili at least washiriki ktk uzalishaji?

  NAOMBA KUWASILISHA!!
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Afadhali hao wananekana wanafyeka wakati huu wa AMANI. Tembelea maofisi mengine ya Serikali/mashirika ya UMMA uone jinsi watu wanavyoshinda wakisoma INTERNET, wakiongea siasa na EPA kutwa nzima, ruhusa za kila aina kwenda kuzika, hospitali,... UFISADI uko aina nyingi nji hii!
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280


  Heshima mbele mkuu obhusegwe.

  Kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi BBC mwaka juzi Tanzania ni nchi yenye jeshi kubwa kuliko nchi zote kusini mwa jangwa la sahara.Sababu za kuwa na jeshi kubwa pengine ni siasa za Tanzania wakati ule wa utawala wa Baba wa Taifa Mwl Nyerere za kusaidia nchi zilizokuwa bado kupata uhuru.Sababu za kuendelea kuwa na jeshi kubwa kwa sasa hazipo tena.

  Mzigo wa kuendelea kuwa na jeshi kubwa wakati hakuna sababu wala viashiria vya kuwepo vita ni wawananchi{walipa kodi}.Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa wanatakiwa kuja na mkakati wa kutumia nguvu kazi kubwa waliyonayo kwa manufaa ya nchi katka kipindi hiki cha amani.

  Wanajeshi wanaweza kutumika katika kipindi hiki cha amani kuzalisha mali.Nchi yetu imebarikiwa kuwa na ardhi kubwa isiyotumika mpaka nchi majirani wanaitamni.Jeshi letu likipewa vifaa vya kisasa kama Tractors na nk Tanzania itaweza kupiga hatua kubwa katika sector ya kilimo na hatimaye kuongeza pato la taifa badala ya kufyeka na kuokota makaratasi.

  Kuwepo mpango wa muda mrefu kulipunguza jeshi.Tanzania inatakiwa iwe na jeshi dogo na vifaa vya kisasa.

  Tatizo kubwa kwa sasa Tanzania ni kukosekana kwa vision na mission kwa viongozi wetu.
   
Loading...