Hivi karibuni tumesikia watumishi wakibar

Chemtrail

JF-Expert Member
Aug 15, 2016
827
442
Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika Kanisa kuhusu unywaji wa pombe.Imefika mahali wanaojiita "watumishi wa Mungu"wamebariki pombe wazi wazi na wengine bila aibu wakikutwa wamelewa.Lakini Biblia inasemaje hasa kuhusu unywaji wa pombe na mvinyo katika Kanisa?Tuangalie mifano katika Biblia ya watu ambao walitumia mvinyo na matokeo ya matumizi hayo mwilini.
AGANO LA KALE:
Katika Agano la kale Haruni na wanawe walikatazwa na Mungu mwenyewe kunywa mvinyo waingiapo hekaluni.Amri hii ilikuwa ya milele katika vizazi vyao vyote!(Walawi 10:9)
Waisrael pia walikatazwa kunywa mvinyo katika nadhiri zao wakati wa kuwekwa wakfu(Hes.6:1-3;Waamuzi 13:4--7).Warekabi waliishi kama mfano wa kuigwa wa kutotumia kilevi cha aina yeyote kabisa(Yeremia 35:1-8;14).Kitabu cha Mithali kiimejaa maonyo mengi kuhusu tabia ya kunywa mvinyo na vinywaji
vingine vikali (Mit.20:1;21:17;23:29-35;31:4).Mvinyo unadhihaki na huleta magomvi (Mit.20:1).Divai pia huleta matatizo mengine mengi yasiyo ya msingi(Mit.23:29-30).Mvinyo huuma kama nyoka;huchoma kama fira.Nabii Isaya yeye alisema,"Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu,watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo."Daniel na wenzake waliweka mfano wa kutokunywa divai ya mfalme (Dan.1:8).Daniel hakunywa divai kabisa(10:3).

AGANO JIPYA.
Katika Agano Jipya,neno la kawaida la mvinyo iwe kilevi au juice ni oivoc au oinos.Bwana Yesu alifananisha mafundisho yake na mvinyo mpya ambao ungesababisha viriba vya zamani
kuvunjika(Mat.9:17).Mtume Paulo alionya waumini kuhusu tabia ya ulevi(Waefeso 5:18) na akasema Watumishi wasitumie mvinyo sana(1Tim.3:8)Akampa ushauri Tito kwamba wazee wa kike wasiwe wenye kutumia mvinyo mwingi(Tito 2:3)
Paulo pia alimshauri Timotheo kwamba atumie mvinyo kidogo kama dawa kwa ajili ya tumbo linalomsumbua(1Tim.5:23).Ieleweke hapa kwamba Paulo alimshauri Timotheo kutumia mvinyo kama dawa sio kama kileo.Dawa zetu nyingi siku hizi zina "alkohol."

Biblia inasema kwamba miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu(1Kor 6:16) Kwa hiyo ni lazima umtukuze Mungu kwa mwili wako.Hii inahusisha unaachokula,kunywa na kufanya."Basi,mlapo,au mnywapo,au mtendapo neno lolote,fanyeni yote kwa utujufu wa Mungu."(1Kor.10:31).Jitafakari,jee unapokunywa kileo ni katika utukufu wa Mungu?Na je,unadhani Bwana Yesu naye angekunywa pombe?Mtume Suleiman alisema,"Mvinyo hudhihaki,kileo huleta ugomvi;na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima."(Mithali 20:1).

Mwisho,pombe ina madhara mengi ya kiafya kwa hiyo si busara kuitumia.Matatizo ni mengi kama ugonjwa wa ini,moyo,aina fulani za kansa,pressure nk..
Bwana Yesu alisema,"Nimekuja ili wawe na uzima,tena wawe nao tele." (Yohana 10:10).Matumizi ya pombe yanaharibu maisha yetu na maisha ya wengine.Hata kwa matumizi kidogo,pombe inaleta matatizo ya kimwili,kiakili na kiroho.Si ajabu kwamba Biblia inaonya kuhusu matumizi ya pombe.Mungu katika Isaya 1:18 anasema,"Haya njoni tusemezane asema Bwana.Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana,zitakuwa nyeupe kama theluji;zijapokuwa nyekundu kama bendera,zitakuwa kama sufu."Je,unaweza kusemezana na Mungu ukiwa umekunywa pombe
kweli?Tafakari.Katika kitabu cha Luka sura ya kwanza mstari wa 15 tunaona maandiko ya msingi sana kuhusu
kileo,"Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana;hatakunywa divai wala kileo;naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye."Huyu ni Yohana mbatizaji. Ndugu yangu,unataka kuwa mkuu mbele za Bwana,acha kutumia kileo.Acha kudanganywa na watumishi waliojiinngiza kwa siri ili kuliharibu kanisa la Mungu.Ombea kanisa la Mungu ili Mungu alilinde na uharibifu huu.
 
Back
Top Bottom