Hivi Jay Z hana Jina lake halisi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Jay Z hana Jina lake halisi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Feb 17, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,889
  Likes Received: 37,109
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kisima hiki kilizinduliwa na Shawn Corey Carter alizindua kisima hiki,
  lakini cha kushangaza badala ya kuandikwa jina lake halisi, limeandikwa jina ambalo hata kwenye passport yake halipo.
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Acha nishangae pamoja nawe......kaazi kweli kweli.
   
 3. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,457
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Kuna madhala kuandika jina hilo???? Mi naona poa tu, ili mradi wakazi wa mwananyamala wanapata maji...maisha yanaendelea!! Au likiandikwa jina lake halisi bomba litatoa maziwa??
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mradi huo ungezinduliwa na Puff Daddy (wa enzi hizo) inamaana kila baada ya miaka kadhaa wangefuta jina la mgunduzi ku-reflect jina lake la kiusanii?? Jamani matumizi ya mabano kwenye sentensi yamekuwa magumu namna hii siku hizi?

  Btw mkuu, hiyo issue ya bomba kutoa maziwa au maji mimi nadhani ni tofauti kabisa na swala linaloongelewa hapa, unless unataka kuwaziba tu midomo watu wasihoji.
   
 5. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  ndo wabongo tulivyo uncle yani wanataka akumbukwe kwa jina hilo ambalo ni jepesi maana wangeandika jina lake halisi wabongo wangeharibu kabsa"shon korey kata"Shawn Corey Carter
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,889
  Likes Received: 37,109
  Trophy Points: 280
  Kweli Therengeti Mamushka unawajua wabongo walivyo.
  sasa wa kutoka kwenye kabila ketu ndio wamezidi.
  Salome wanaita Salume,
  Francis wanaita Falanchisi,
  Humphrey wanaita humpule,
  Modesta wanaita Mondesta,
  yaani raha kwelikweli
   
 7. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Hii ndo bongo uncle kila kitu short cut tu!watu hatutaki shida kabsa,kisa cha kujing'ata ulimi bure!buji buji watakuita bui bui!ah ah ah wakifikia hapo ntawachapa mm!Pearl wataita pele!
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  hahahah wewe ni kakaangu thi tumetoka kijiji kimoja bujibuji :)
   
 9. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,457
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Point yangu inabaki palepale, jina is not a big deal kwa wakazi wa pale! Kama maji yanatoka, inatosha!! Ukiona ni issue sana mwambie Mwamvita Makamba akafute Jay Z na aweke Shawn Carter!!

  Naomba niulize swali wakuu...hizi kuweka majina ya waliofungua miradi inasaidia nini? Pengine hapa ndo ninapo miss mantiki ya hoja yako!!
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Inawezekana kabisaa...

  Kwani pahali popote pale palipoandikwa "mradi huu ulizinduliwa na..." au "jengo hili lilizinduliwa na..." hakuna mantiki yoyote ile tena, maana wale walioamua kufanya hivyo watakuwa wameelekeza nguvu zao zaidi kwenye protokali za uzinduzi badala ya kujua iwapo 'maji yanatoka au hayatoki' au jengo 'lina madirisha na milango au halina'.
   
 11. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,457
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Umenigusa sana....binafsi nina mtizamo huo huo. Miradi mingi inatazamwa kisiasa zaidi kuliko ufanisi wa mradi wenyewe baada ya kuzinduliwa.

  Ndo maana binafsi naona hakuna mantiki, nina mifano mingi ya miradi iliyozindulia na mh. rais na waziri mkuu mwaka 2008 & 2009 ambayo ni non performing na hakuna anayejali! Ukipita ukisoma jiwe la msingi unabaki kusikitika tu!!
   
 12. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,851
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  J-Z anatoka USA kuja kuzindua mradi wa kisima cha maji mwananyamali ni mradi wa sh.ngapi? na kweli karne tunahitaji visima vya aina hii AU ni huduma hii kuwa karibu na watumiaji? VIONGOZI WAJIPANGE
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,889
  Likes Received: 37,109
  Trophy Points: 280
  Tunaisubiri kwa hamu ilani ya uchaguzi ya mwaka huu, tutasikia mengi.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...