Hivi jamani humu hamna wapenzi wa tamthiliya

Kbd

JF-Expert Member
Oct 9, 2009
1,260
447
Hivi kweli JF yote imejaa wapenzi wa mpira tuuuu.......hamna hata mtu anapenda tamthiliya? Mi napenda na huwa naangaliaga chache, ningependa kufahamu kama kuna mtu anayependa na angependa tuwe tunashirikiana kuelezana na kusimuliana...............Asanteni.
 
Hukupita shule ya msingi wewe? Huko ndiko kuna kusimuliana tamthilia lol!
By the way mimi pia ni mpenzi wa tamthilia but siwezi kusimulia and i don't like kusimuliwa, if ilipita sikuangalia, its over!
 
Hukupita shule ya msingi wewe? Huko ndiko kuna kusimuliana tamthilia lol!
By the way mimi pia ni mpenzi wa tamthilia but siwezi kusimulia and i don't like kusimuliwa, if ilipita sikuangalia, its over!

Ndugu yangu mi shule niliyoma ni zile za msondo ngoma primary school, mambo ya tamthiliya hatukuyajua kabisa. Yaani mi napenda na natamani kusikia maoni ya wanaopenda ili tuendeleze libeneke. Asante.
 
Ok, bac tupo pamoja, ila kuhadithia siwezi lol!

Asante sana my dia, wala usijali maana hapa jamvini mbona hapaharibiki neno. Usichokiweza wewe wengine kwao ni kitu kidogo sana. Sit back and enjoy!!
 
tuanze na ipi...zipo nyingi

My dia tuanze na isidingo, vile iko hot kipindi hiki mi imenivutia sana. Natamani kujua ma Agnes akijua kuwa Thandi anamimba ya Zebedee badala ya Parsons sijui itakuwaje.

Ila pia njia nyingine; waweza fungua tredi tofauti za tamthiliya hivyo kila mtu anapata nafasi ya kuchangia zote au ile anayoipenda.

Karibuni sana!!
 
oooh ok...nilikuwa naifuatilia lakini kutokana na majukumu nashindwa...vipi Parsons amerudiana na Nandhipa? huwa nawaona ona ila sijui kinachoendelea...ilikuwaje mpaka Thandi akapata mimba ya baba mkwe?...duh
 
My dia wee ndio uko nyuma kweli.

Nandipa na Parsons walishaachana na akamuoa Thandi. Sasa wakawa wanataka mtoto ndio ikabidi waende hospital kupima na matokeo ni kuwa Thandi yuko poa ila Parsons ndio hawezi kuzaa.

Sasa sijui ilikuwaje maana sijaangalia muda mrefu juzi naangalia nikakuta ngumi Parsons na baba yake kwenye mgahawa wa ma Agnes. Na ma Agnes hajui sababu kwa nini wanapigana.

Kufupisha ni kwamba leo amegundua kuwa Zebedee na Thandi wanaexpect mtoto na amechukia sana na amemfukuza zebedee nyumbani kwao na amekwenda kupanga hotelini.

Ma Agnes anasoma biblia yake na anasali kwa machozi, Parsons anakunywa sleein pills ili angalau alale, Thandi analia tu wala hana amani na anaogopa hata kutoka nje maana kijiji kizima kinajua ufisadi alioufanya na Zebedee mwenyewe yuko hotelini na ajui afanyeje.

Yaani ni vurugu mechi kwenye familia ya Zebedee.
 
Ishu ya Parsons ni ngumu kumesa katika reality..
Incase anazaliwa atamwitaje mdogo wangu au mtoto wangu??
Ila choice ya Parsons nzuri..bora itolewe tuu..hata ningekuwa mimi angeitoa au ndo mwisho wa ndoa..!
 
kdd na Iza wengi wetu tunaangalia Isidingo kupitia SABC3 hiyo ya ITV ipo nyuma miezi zaidi ya sita
 
kdd na Iza wengi wetu tunaangalia Isidingo kupitia SABC3 hiyo ya ITV ipo nyuma miezi zaidi ya sita

Duuuu..........ama kweli tumepitwa na wakati yaani nyuma miezi sita.....that is tooooooo december.

Sasa ndugu yangu blackpepper kama na wewe ni mpenzi wa hii tamthiliya hebu tupe basi japo kwa muhtasari yatakayojiri hukoo baadae kati ya zeb na ma agnes na parsons na mkewe ili nasi japo roho zitulie kidogo.
 
Jana Lesedi kampa live Vusi kwamba amefall sasa tujiandae kuangalia new lovers..Vusi nae inaelekea ka-fall
 
Jana Lesedi kampa live Vusi kwamba amefall sasa tujiandae kuangalia new lovers..Vusi nae inaelekea ka-fall

Sasa dia Lesedi si anamume wake yule ambae alitaka kuchoma hoteli yao?? Au walikuwa wapenzi tu bila kufunga ndoa?
 
Ishu ya Parsons ni ngumu kumesa katika reality..
Incase anazaliwa atamwitaje mdogo wangu au mtoto wangu??
Ila choice ya Parsons nzuri..bora itolewe tuu..hata ningekuwa mimi angeitoa au ndo mwisho wa ndoa..!

ikitolewa ndo warudiane??

afu mi ndo wale wadandiaji, sikuelewa hiyo mimba alipandikizwa mbegu za mkwe au walifanya uzinzi kabisa??
 
ikitolewa ndo warudiane??

afu mi ndo wale wadandiaji, sikuelewa hiyo mimba alipandikizwa mbegu za mkwe au walifanya uzinzi kabisa??

Hawakufanya uzinzi my dia.......walipandikiza na nadhani bila kuwashirikisha wanafamilia wengine ndio maana sasa hivi hapatoshi horizon deep.
 
Hawakufanya uzinzi my dia.......walipandikiza na nadhani bila kuwashirikisha wanafamilia wengine ndio maana sasa hivi hapatoshi horizon deep.

aaaah Zebedi na yeye bana...........!!!!
 
Back
Top Bottom