Amba Samedi
Senior Member
- Apr 5, 2024
- 193
- 326
Habari wanaJF,
Ni siku nyingi sana sijazungumza humu. Nimekuwa tu zangu macho kufuatilia matokeo ya uchaguzi na ghasia na fujo zilizotokana na uchaguzi huu. Jamani, Mungu awape utulivu waliopoteza wapendwa wao katika matukio haya ya kusikitisha, na amani itawale nchini Tanzania.
Tanzania ilishuhudia kile kinachoitwa total internet shutdown (kuzima kwa intaneti) — hali ambapo huduma za mtandao zilipungua au kusimama kabisa nchini kote kwa siku kadhaa (kama 5 hivi).
Watu wengi walijaribu kudadavua tukio hili, wengine wakifikiri ni hitilafu ya kawaida ya kampuni za mtandao (binafsi nilipigia voda, wakawa wanajing'atang'ata. Baadaye na support center ikazima, lo!)
Lakini ukweli ni kwamba, hili lilikuwa kuzimwa kwa makusudi (deliberate shutdown).
Hebu tuangalie kilichotokea, kwa nini hufanyika, na namna tunavyoweza kujitayarisha kwa siku zijazo (endapo hili litajirudia).
Ukitaka article kwa kiingereza, makala haya hapa:
Fikiria intaneti kama barabara kuu za mawasiliano. Kuzimwa ni kama polisi kufunga barabara zote hizo — hakuna gari (data) linaloingia wala kutoka.
Kwa baadhi ya watu, hii ina maana ya kukosa habari, kutoweza kufanya biashara, au kushindwa kuwasiliana na familia.
Amri hizo zinaweza kusema:
VPN (Virtual Private Network) ni kama handaki la siri kwenye mtandao.
Inaficha data yako na kuipitisha kupitia nchi nyingine, hivyo mmiliki wa mtandao haoni unachofanya ndani ya himaya yake.
VPN inaweza kufungua programu zilizozuiwa (kama Facebook au X) endapo intaneti ipo. Hata hivyo, VPN haiwezi kufanya kazi kama intaneti imekatwa kabisa. Unahitaji mtandao wa kawaida ili VPN iweze kuanzisha handaki hilo.
Ndo maana, wakati wa kuzimwa kabisa (Oktoba 29 – Nov 3), VPN hazikusaidia. Hata hivyo, baada ya intaneti kurudi, VPN zikawa msaada wa kukwepea vizuizi vya mitandao ya kijamii.
Ila siku ikikata tena, hakikisha umejipanga. Usiseme sikukuambia.
Ni siku nyingi sana sijazungumza humu. Nimekuwa tu zangu macho kufuatilia matokeo ya uchaguzi na ghasia na fujo zilizotokana na uchaguzi huu. Jamani, Mungu awape utulivu waliopoteza wapendwa wao katika matukio haya ya kusikitisha, na amani itawale nchini Tanzania.
Tanzania ilishuhudia kile kinachoitwa total internet shutdown (kuzima kwa intaneti) — hali ambapo huduma za mtandao zilipungua au kusimama kabisa nchini kote kwa siku kadhaa (kama 5 hivi).
Watu wengi walijaribu kudadavua tukio hili, wengine wakifikiri ni hitilafu ya kawaida ya kampuni za mtandao (binafsi nilipigia voda, wakawa wanajing'atang'ata. Baadaye na support center ikazima, lo!)
Lakini ukweli ni kwamba, hili lilikuwa kuzimwa kwa makusudi (deliberate shutdown).
Hebu tuangalie kilichotokea, kwa nini hufanyika, na namna tunavyoweza kujitayarisha kwa siku zijazo (endapo hili litajirudia).
Ukitaka article kwa kiingereza, makala haya hapa:
1. Kilichotokea Oktoba 29 – Novemba 3 2025
- 🗓️ Oktoba 29, 2025 – Siku ya Uchaguzi: intaneti ilizimwa ghafla nchini kote.
- 🌍 NetBlocks na taasisi zingine zilithibitisha kuwa kasi ya intaneti Tanzania ilishuka kwa karibu asilimia 90.
- 📵 Kwa takribani siku tano, watumiaji wengi hawakuweza kufungua tovuti au apps za simu.
- 📅 Novemba 3, 2025 – Baada ya kuapishwa kwa Rais, intaneti ilianza kurudi kwa kunyatia.
- 🚫 Lakini programu maarufu kama Facebook, X (Twitter), WhatsApp, JamiiForums, YouTube, na Instagram Live zilikuwa bado zimezuiwa.
- 🔑 Ili kuzifikia, watu wengi walilazimika kutumia VPN.
2. Kuzima kwa Intaneti ni Nini?
Kuzima kwa intaneti hutokea pale ambapo kampuni za simu na intaneti husitisha au kupunguza huduma za mtandao kwa watu wengi (kwa hiari au kwa kuagizwa na mamlaka husika).Fikiria intaneti kama barabara kuu za mawasiliano. Kuzimwa ni kama polisi kufunga barabara zote hizo — hakuna gari (data) linaloingia wala kutoka.
Kwa baadhi ya watu, hii ina maana ya kukosa habari, kutoweza kufanya biashara, au kushindwa kuwasiliana na familia.
3. Aina Kuu za Kuzima Mtandao
a) Kuzima Jumla (Total Blackout)
- Kila kitu kinafungwa.
- Simu, kompyuta, programu, hata tovuti za benki hazipatikani kabisa.
b) Kuminya Kasi (Throttling)
- Mtandao unakuwa mzito sana kwa makusudi.
- Video hazichezi, WhatsApp haipitishi meseji kwa wakati, na kila kitu “kinalodi” bila mafanikio.
c) Kuzuia Programu Maalum (App Blocking)
- Serikali huamuru kampuni kuzuia programu chache, kama Facebook, X, JF au YouTube.
- Mtandao mwingine unaendelea kufanya kazi kama kawaida.
- Hii ndiyo hali iliyotokea Tanzania kabla na baada ya Novemba 3, 2025 (hasa kwa mtandao wa JF).
d) Kuzuia Sehemu Fulani Pekee (Feature Blocking)
- Baadhi ya huduma za ndani ya programu hufungwa.
- Kwa mfano hata sasa, si rahisi kutuma picha, document, au video ndani ya WhatsApp bila VPN au Tor Browser.
4. Jinsi Serikali Inavyotekeleza Kuzima Mtandao
a) Amri Rasmi
TCRA (mamlaka ya mawasiliano) hutuma maagizo rasmi kwa kampuni zote za simu na intaneti — kama Vodacom, Tigo, Airtel, Halotel, n.k.Amri hizo zinaweza kusema:
- “Zima intaneti ya nchi nzima.”
- “Zima tovuti hizi maalum.”
b) Njia Zinazotumika Kuzuia
- DNS Blocking – kama kufuta namba ya simu ya tovuti fulani kwenye “kitabu cha simu cha intaneti”.
- IP Blocking – kufunga anwani ya namba (IP) ya tovuti ili data isifike huko.
- Port Blocking – kufunga “mlango” fulani wa huduma, mfano ule unaotumika kwa video mubashara.
- WhatsApp inabaki na tiki moja.
- Facebook haipakii post mpya.
- YouTube inazunguka tu bila kucheza video.
5. Mifano Kutoka Afrika
- Cameroon (2017–2018): Serikali ilikata intaneti kwa miezi kadhaa wakati wa maandamano.
- Uganda (2016 & 2021): Intaneti ilizimwa kabisa wakati wa uchaguzi, na mitandao ya kijamii ilizuiwa kwa siku nyingi.
- Tanzania (2020): Mitandao ya kijamii ilifungwa. Hukuweza kuipata bila VPN. Na wakati fulani hungeweza kupakua VPN playstore (labda utumiwe kupitia Xender)
6. Athari kwa Maisha ya Kawaida
Kuzima kwa intaneti si suala la siasa pekee — linaathiri kila sekta ya maisha:- Biashara : Huduma kama M-Pesa na TigoPesa zilikwama; maduka ya mtandaoni yalipoteza wateja. Soko la Kariakoo lilikiri kupoteza mabilioni ya pesa kwa dili zilizoyeyuka.
- Usafiri: Madereva walikwama. Bolt na Uber hazikuweza kusafiri (si ramani hamna).
- Huduma za Dharura: Kutuma fedha kwa ndugu kulikuwa na changamoto.
- Elimu na Kazi: Masomo na kazi za mtandaoni zilisimama kabisa. Watu walibaki nyumbani. Jana na leo ndo shule imerejea.
7. VPN ni Nini, na Inasaidiaje?
VPN (Virtual Private Network) ni kama handaki la siri kwenye mtandao.
Inaficha data yako na kuipitisha kupitia nchi nyingine, hivyo mmiliki wa mtandao haoni unachofanya ndani ya himaya yake.
VPN inaweza kufungua programu zilizozuiwa (kama Facebook au X) endapo intaneti ipo. Hata hivyo, VPN haiwezi kufanya kazi kama intaneti imekatwa kabisa. Unahitaji mtandao wa kawaida ili VPN iweze kuanzisha handaki hilo.
Ndo maana, wakati wa kuzimwa kabisa (Oktoba 29 – Nov 3), VPN hazikusaidia. Hata hivyo, baada ya intaneti kurudi, VPN zikawa msaada wa kukwepea vizuizi vya mitandao ya kijamii.
8. Jinsi ya Kujiandaa kwa Siku Zijazo
Kwa kweli, sio wakati wa kubweteka tena. Hasa kwa sisi tunaotegemea mitandao kwa kazi zetu (online workers), huu wakati ni wa kujipanga kikamili. Kuna mambo mengi ya kufanya, pamoja na:a) Maandalizi Binafsi
- Jifunze kutumia SMS na USSD (kama *150*00#) kwa huduma za kifedha. Wengi walikuwa wamezoea app, jambo ambalo liliwaponza.
- Weka nakala za nyaraka zako muhimu offline (nje ya mtandao).
- Kuwa na pesa za akiba, in cash (Nje na hela ya kwenye simu kama MPESA na Yas, wengi wa benki na VICOBA walikwama. Hela unayo, lakini huwezi kuitoa).
b) Njia Mbadala ya Mtandao
- Fikiria kutumia intaneti ya setilaiti (kama Konnect Africa au Starlink. Nafanya mchakato wa kuwa nazo zote mbili. Ntaleta mrejesho humu). Haitegemei nyaya au kampuni za simu, hivyo inaweza kusaidia hata wakati wa kuzimwa.
- Wataalamu wajifunze kutengeneza "Offline First Apps". Natamani hata huduma za serikali zingeadopt teknolojia hii. Ili hata mkonga ukikata, huduma ziendelee kupatikana offline, ili mtandao ukirudi, ifanye uploading. Na akili mnemba (AI) inawezesha uwepo wa information offline, na inaweza kutumika bila ya mtandao.
Hitimisho
Siku hizi, intaneti ni hitaji la msingi kama maji, chakula, na makazi. Tunaitumia kwa biashara, afya, elimu, na kuwasiliana na familia. Kuzimwa kwake kunamaanisha:- Biashara hazendeshwi,
- Wanafunzi hawasomi,
- Familia hazipati habari.
Ila siku ikikata tena, hakikisha umejipanga. Usiseme sikukuambia.