hivi inawezekana ama ni kwangu tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hivi inawezekana ama ni kwangu tu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by manshiroo, Jul 2, 2012.

 1. manshiroo

  manshiroo Senior Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wapenzi wana mmu najitokeza mara ya kwanza hapa jukwaani nikiwa kama memba baada ta kuingia kama mgeni ka siku nyingi sana.

  leo hii kilichonifanya nitamani kuingia humu ni hiki hapa, niko safarini naenda msibani Arusha wifi yangu kafiwa na mumewe. cha ajabu wk nzima iliyopita ndani kwangu hakukaliki, kila saa ugomvi tu amani hakuna wala raha hakuna nimejikuta kama naona ndoa ni chungu. sasa jana wakati niko ndani ya basi la mtei niligbahatika kukaa siti moja na baba mmoja siyo mzee ila siyo kijana ni kama wa miaka 45. Tulipokuwa maeneo ya king'atit basi liliharibika na kwakua huyu baba ni mwenyeji wa arusha akasema usiwe na tabu kwasababu wewe ni mgeni miye nitakusindikiza hadi huko. kweli aliita gari na nikapata lift, kwakweli care za huyu baba, zilinipagawisha sana, nikakuta kule kunifungulia mlango na kufunga, kule kunibebea kipochi changu, kunikaribisha tu kasupu b4 sijafika eneo la tukio kulinifanya nimuone mtu mwema sana nikajikuta naanza kumfananisha na hubby ambaye hivyo hafanyi kabisa.

  kibaya zaid hapa msibani kaja kuniulia hali na kasalimiana na wifi vizuri, na kisha baada ya mazishi nikamsindikiza kwenye gari, jamani amenionyesha upendo ambao sijawah kuupata kwenye ndoa sasa amekwisha ondoka ila najiuliza hali hii imewah kukuta? yaani inafika mahali mtu unasema natamani ningeolewaga na huyu au ni kwangu tu? imagine kaniambia kesho atakuja kunichukua anipeleke stendi jamani nifanyeje mbona kama nataka kuanguka dhambini? Siyo kwamba simpendi mr ila tu maudhi ya ndani ndio yananifanya nianze kumcompea
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Epuka hilo na na usilogwe na tamaa ya fisi ya kufikiria mkono wa binadam utaanguka muda wowote
  Wema wa siku moja kufunguliwa gari au kusalimiwa na kupewa pole zisikufanye uanguke dhambini na uisaliti ndoa yako
  katengeneze kwako na ikiwezekana mkaribishe Mungu katika mahuasiano yako na angalia umeanguka wapi kabla ya kuanza kufikiria kutoka nje ya ndoa
  Heshimu ndoa yako na wala usilaghaiwe kwa wema wa siku moja may be uniambie huyo mzee umemfaham siku nyingi na sio kuwa umekutana nae kwenye gari
   
 3. manshiroo

  manshiroo Senior Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sijawah hata kumuona zaid ya tulivykutana kwenye gari basi. Hapa mimi najiuliza kwanini hali kama hii itokee? mbona mume wangu hanijali jamani ama nilikosea kupenda? nimesali sana kaka na nimelia sana tena mpaka nimesema silii tena lakini mume wangu hanionyeshi hata wema ambao wengine wananionyesha.

  siyo mwanaume wa kwanza kunitaka huyu huwa naruka viunz sana tu lakni kwanini mume wangu hanion kama n wa thamani kam wengne wanavyoniona?

  kaka yangu hebu jiulize wewe kama mkaka hata siku moja mkeo haja kusifia kwa jambo lolote lakin kila siku wanawake unaokutana nao wanakusifu tena kwa vitu ambavyo vipo wazi utajiskiaje?
   
 4. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Uko msibani mwanangu!!. Kumbe "ngoma" nyingine za kujitakia.

   
 5. E

  Edo JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nabii kwao????? ukikumbuka hili utaepuka, maana japo simjui hata mumeo mwanzoni alikuwa anakujali kama huyu nudgu yetu!
   
 6. Laigwanan76

  Laigwanan76 JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wanaume dizaini kwa wake zao wa halali ni mabazazi kinoma........
   
 7. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Duuh mshinde shetani, kila ndoa ina balaa lake. Mwanaume anaweza uza ukoo wako ili amlale mwanamche achilia kumwoa. Kwahiyo huyo baba ni fix tu za wazee wa mjini.
   
 8. kapistrano

  kapistrano JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,204
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kuna wanaume wanaswaga kiasi kwamba wanatongoza mpaka wanalia sasa huyu jamaa kakupa swaga za kiutu uzima pengine hata kwake ni mkali matata fanya mchezo utie kitumbua chako mchanga mpende mumeo.
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Sijui,ila lazima siku ukila chakula ambacho hujakila au una siku hujakila huwa kizuri sana,ila ukizoea huwa kawaida na pengine cha zamani hukumbukwa!
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  hivi mie nimezaliwa nawindwa njiwa pori, kweli ntashindwa kujua teknik ndogo ndogo kama hizo???

  Wanamme at 40's bado wana nguvu na wanaexperience na wanawake so wanajua how to treat ladies.

  Yaani wee vimtama hata robo havifiki vinataka kukuangusha zambini? Je akiweka na ka ulimbo si unaachika?
   
 11. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Ukweli mtupu, wakati niko boarding school nilikua natamani sana kula wali nyama kila siku, sasahivi natamani kupata mihogo, viazi, magimbi na ugali.

  Anabahati kuuliza hapa atajirekebisha, vinginevyo atajuta kumfahamu huyo baba!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,875
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Duh! Manshiroo ni aje bana!?

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mmmmmh yaani huyo akishapata anachotaka Anaweza akabadilila hadi ikabaki kinywa wazi.
   
 14. l

  lunyonga New Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we mwanamke kuwa mjasiri usimchune mmeo!
   
 15. mito

  mito JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,653
  Likes Received: 2,039
  Trophy Points: 280
  Umenishangaza sana manshiroo (hapo kwa redi), yaani wewe unachopenda ni kusifiwa, kubebewa pochi, kufunguliwa mlango wa gari .... loh! very artificial life!! wengi wenye mtizamo kama wako wameishia kuumizwa! Yaani hata unashindwa kutambua kuwa hizo zote ni gia za kukupata? kalaghabaho!
   
 16. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Dah tutake radhi sisi wanaume wenye heshima zetu!
   
 17. T

  Tafakuru Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Binti, haya sio mapenz mazuri sana ni vile tu ya kwako hayaja kaa vizuri. Ata yy akikupata anakuacha vile vile, tulia matatizo kwenye ndoa kawaida tu

  Yani wee binti sijui kama kweli unampenda mumeo au ni penda penda. Rekebisha mambo yako mumeo anamengi tu mazuri ambayo uyo babu hana, jitaidi kuudumia ndoa yako
   
 18. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  so kesho ndo unaenda kutoa kitumbua kabla ya kurudi ulikotokea?

  dada mpende mumeo usimsaliti, ongea nae mwambie unavyopenda aku-trit
   
 19. T

  Tafakuru Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Yani wanawake naomba niwaambie. Wanaume ni watu waskivu sana, asilimia kama 90 ya wanaume wanabadilishwa na wanawake wao. Sasa kama kila ataekua anakupa msaada msibani anakulala, atakaekusaidia mwamvuli kwenye mvua anakulala, mangi akikupa discount anakulala kweli tutafika???!!!!!!!!!!!!!! Sio kila anaekupenda umpe mwili wako, fkiria mumeo angekufanyia ivo kama ww unavoshawishika kufanya
   
 20. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  badili ladha bana... kisha rudi kwa mumeo na sahau yaliyotokea
   
Loading...