Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Tumemsikia wenyewe wakati anahutubia wafanyibiashara aliowaalika Ikulu hivi karibuni akiwaambia kuwa anatamani, kipindi anatoka madarakani awaache wafanyibiashara mabilionea wakiongezeka nchini, ikiwezekana awaache mabilionea wasiopungua 100, wakati anaondoka madarakani mwaka 2025!
Nimekuwa nikijiuliza sana, si ndiyo huyu huyu mtu, ambaye siku za nyuma, aliwahi kutamka kuwa anatamani wafanyibiashara matajiri, waliokuwa wakiishi kama malaika, waishi kama mashetani, katika awamu yake?
Hivi so ndiyo huyu huyu aliyesema, yuko tayari kuona anapokea meli moja bandarini, inayoweza kulipa kodi, kuliko kuona meli 100, zisizolipa kodi??
Katika kikao hicho cha wafanyibiashara, walieleza kero zao nyingi kuhusiana na namna wanavyonyanyaswa na hao tumaoambiwa ni wakadiriaji kodi, watu wa TRA, ambao walidaiwa kuwa hawana ubinadamu hata kidogo wakati wa ukadiriaji wao kodi
Waliendelea kueleza wafanyibiashara hao kuwa hao TRA wamekuwa wanyama zaidi ya "Israel" kwa namna wanavyokadiria kodi kubwa, kiasi kilichofanya wafanyibiashara wengi wafunge biashara zao
Najua kuwa unyama huo wa watu wa TRA ulikuwa na "full blessings" za Mkuu, lakini nimeshangaa majuzi akiwaruka maili 100, hao TRA, kuwa eti ni wao wenyewe wanaojipangia kodi kubwa zisizoweza kulipika!
Akaendelea kueleza kuwa hakuna Taifa lolote lililopata maendeleo duniani, bila kutegemea sekta binafsi
Pengine tuseme kuwa Mkulu ameona pato la Taifa linazidi "kukauka" kwenye hazina ya Taifa, kutokana na hizi kauli za kinyama za hao watu wa TRA kuwa lipa kodi au funga biashara..........
Hao wafanyibiashara waliona hawana "option" nyingine zaidi ya kufunga biashara zao kwa kuwa hizo kodi walizokadiriwa nazo hazilipiki!
Hebu tembelea eneo maarufu kwa biashara nchi hii eneo la Kariakoo uone namna wafanyibiashara kwa maelfu, namna wanavyofunga biashara zao, kutokana na makadirio ya kodi ya "kinyama" za hao watoza ushuru
Ni hayo tu maoni yangu