Hivi ilikuwaje CHADEMA kutowashirikisha washirika wa UKAWA katika UKUTA?

ZNM

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
1,217
1,273
Tangu kuanzishwa kwa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) na kuungwa na vyama vya siasa vinne, wamekuwa wakishirikiana vema na kwa ukaribu katika mipango yao ambayo kiukweli umoja huo umevuna mafanikio makubwa sana hasa kwa CHADEMA na bila shaka hakuna asiyejua!

Issue ya kungoza majiji yote isipokuwa jiji la Mwanza pekee si kazi ndogo jamani, sasa ninachojiuliza, kwa nini CHADEMA hawajawahusisha washirika wenzao katika suala la UKUTA? Ni kweli CHADEMA wamesahau Mchango wa James Mbatia, Maarim Seif, Haji Duni na wengine wengi waliopambana na kuwawezesha kupata wabunge wengi safari hii?

Kweli kuna sababu za msingi kumtenga hata huyu Mbatia ambaye hivi karibuni tu aliongoza wabunge wa UKAWA kuweka plaster midomoni na kuondoka bungeni? kuna ajenda gani nyuma ya pazia? Mpaka sasa Mbatia amekuwa kama hayupo nchini kwa kutengwa katika hili wakati hakuna asiyejua uwezo wa Mbatia katika kujenga hoja!

Binafsi naona Washirika wa UKAWA katika suala la UKUTA hawajatendewa haki labda kama kuna hoja za msingi! Na niwaombe tu hata wafuasi wengine wengi wanaoshabikia UKUTA, msidhani lolote litakalotokea juu yenu lenye kuwadhuru mtapata ushirikiano kutoka kwa mnaowaunga mkono, mfano mdogo tu ni huo wa Kusahaulika kwa washirika wa UKAWA wakati walifanya kazi kubwa kufanikisha mipango mingi ya CHADEMA.
 
May be hao wengine hawataki kushikishwa UKUTA. May be ni family matter (Mtei & Co).

Unategemea msomi kama Mbatia kweli ashikishwe ukuta hivi hivi? September mosi sikai mbali na TV...
 
Labda niulize, Mbatia yupo? labda ktk hili hakushirikishwa kwa kuwa alikuwa nje ya nchi kikazi!
 
Nilimsikia Mbowe kuwa wanafanya mpango ili ktk mpango huu wa ukuta, act wazalendo kwa uzalendo wao nao waunge mkono! ni kweli chadema mnaomba kuungwa mkono na zitto? kwa kuwasahau waliowawezesha kupata mafanikio, mnaanza kumtafuta tena zitto?
 
Back
Top Bottom