Kashi
JF-Expert Member
- Jan 6, 2013
- 897
- 743
Ndugu wana Jf ninashangazwa sana na hii serikali yetu kukurupuka katika matumizi ya teknolojia ambazo haina uwezo nazo.Leo ni wiki ya tatu tangu walimu na watumishi wengine wa Halmashauri waanze likizo zao lakini nauli bado hazijatolewa kisa mfumo wa EPICA umekata network.Kazi nyingi kwenye Mahalmashauri zimesimama kisa EPICA,kama imetushinda si turudie mfumo wa zamani tujipange upya? Najua hili litakuwa ni shinikizo tu la IFM kutumia madudu tusiyoyaweza.Naomba kuwasilisha.