Hivi hizi habari zina ukweli wowote???

juju000

Senior Member
Apr 2, 2015
151
94
[6/4, 12:15] Eliah: Habari kwa wahitimu wote wa kidato cha sita na wahitimu wote wa stashahada mwaka 2016. Ni dhahiri kumefanyika mabadiliko makubwa Katika bodi ya usajili vyuo vikuu hii imehusisha mabadiliko ya viongozi wa bodi pamoja na baadhi ya miongozo ya usimamizi.kwa wahitimu wa kidato cha sita,wanafunzi watakao pata daraja la kwanza na la pili yaan division one na division two ndio watakosajiriwa kwa elimu ya shahada yaan degree na kwa wale watakaomaliza diploma ni wale watakaopata hazini ya ufaulu Kuanzia 3.3 na kuendelea yaani GPA ya 3.3.kwa wahitimu wa kidato cha sita watakaopata daraja la tatu yaani division 3 watasoma stashahada adhiri yaani special diploma hii itachukua na wahitimu wa stashahada ambao hawakukidhi viwango. Ieleweke wazi hakutakua na usajili wa wahitimu watakao pata daraja la nne na wale watakaopata GPA chini ya 3.3 kwa wahitimu wa stashahada pia hakutakua na mkopo wa wanafunzi wa stashahada adhiri kama ilivyokua awali,Bali patakuwa na punguzo la ada la asilimia 35 kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka 2016/2017.imesainiwa na kupit
[6/4, 12:17] Eliah: MAELEZO JUU YA KUOMBA MKOPO.

Bodi ya mikopo tayari imefungua dirisha Kwa waombaji wote wa mikopo, tangu tarehe, 19/ 05/2016 hadi tarehe 30/ 6/ 2016.

Maombi ya mkopo yanafanywa na mwanafunzi ambaye hadhaminiwi na anufaiki na mkopo huo kutoka bodi wala shirika lolote.

Mwanafunzi huyo awe amemaliza kidato cha Sita Kati ya mwaka 2013 na 2016. na asiwe ameajiriwa.

Pia mwanafunzi huyo anapaswa awe mtanzania,kama sheria no. 9 ya 2004. ya bodi.

Lazima mwanafunzi aombe ONLINE, kupitia OLAS yaani (online loan application system). Baada ya kuwa umenunua vocha ya shilingi 30000/=.M-PESA unaingiza namba zile za vocha. ulizonunua M-PESA.

Unaanza jaza details kadhaa online, kama matokeo, mahali unapoishi, kazi ya baba, mama, Jina la mdhamini, anapoishi, na details zako zingine zitakazo hitajika. Pia Kwa wale CONTINOUS katika fomu hiyo online mtapaswa Jaza matokeo yote ya kidato cha nne na kidato cha Sita.

Ukimaliza una print fomu zile, ukimaliza print unajaza sehemu kadhaa maalum Kwa kalamu, unaziambatanisha na na nakala zifuatazo.

*nakala ya cheti cha kuzaliwa
* nakala ya cheti cha kidato cha nne.
*nakala cheti cha kifo kama mzazi /wazaz wamekufa.
*nakala ya barua ya daktari kama mzazi ni mgonjwa au mlemavu.
*>nakala ya barua ya kustaafishwa kama mzazi, mlezi, Hana kazi au amestaafu
>nakala ya kitambulisho cha mdhamini. Hasa I uraia au cha mpiga kura.
>passport size yako na ya mdhamini wako.

Baada ya hapo unapeleka Kwa mwanasheria anayetambulika, aidha wakili au hakim. Kuna sehemu yake ya kujaza pia kupiga mhuri na saini yake katika kila nakala ulioiambatanisha ili kuthibitisha.

Baada ya hapo nenda Posta katume Kwa njia ya EMS.

MAELEZO YA ZIADA.

Mkopo unaotolewa unajumuisha yafuatayo.
>meals and accommodation
>tuition fees
>books and stationary
>special faculty
>field and training
>research expenses

Kwa CONTINOUS STUDENTS, yeyote anaye nufaika na malipo yeyote hapo,hata kama ni 0% huyo hapaswi kuomba Tena mkopo.

Bali mtu wa namna hiyo anapaswa asubiri akate rufaa ili kuomba aongezewe kiasi cha fedha, anaweza akawa analipiwa meals and accommodation tuu, anapaswa aombe aandike sababu Za msingi, na Za mashiko wakati wa kukata rufaa (appeal). Ili aongezewe kiasi cha fedha au malipo.

Hivyo yeyote ambaye anadhaminiwa na bodi hata kama ni kidogo, asifanyi maombi asubiri Muda wa kukata rufaa. Ambapo tutafahamishana pia.

Shukrani saana, ninawaomba wote ambao hamjawahi fanya maombi au mlifanya mkakosa, msikati tamaa.

OMBA TENA MKOPO!!
OMBA TENA MKOPO!!
OMBA TENA MKOPO!!

By mahmudu, Abdul omary Nondo.
(naibu waziri wa mikopo udsm).
 
Sasa we kilaza Kuna haja gani ya Kuja hapa kuuliza kama ni kweli wakati website ya bodi ya mikopo unaifahamu?? www.heslb.go.tz au ndo uwapotezee Muda watu kusoma hayo madudu uliyojitungia
 
Hii Habari Ni Ya Uongo Na Wala Sio Confirmed kwani Si Habari inayotoka Bodi ya Mikopo wala TCU (Not Official Announcement) Bali Ni Propagandas/Rumors Zinazozunguka Mitandaoni.

Kwanza HESLB hawajafungua Milango Yao Kuomba Mkopo, Kwahiyo Unaposema "Bodi ya mikopo tayari imefungua dirisha Kwa waombaji wote wa mikopo, tangu tarehe, 19/ 05/2016 hadi tarehe 30/ 6/ 2016".
Hapo Utakua Na Wewe ni Victim wa Hizo Propaganda.

Waliokuwa Wamefungua Dirisha Si Bodi Ya Mikopo, Bali Ni NACTE kwa Ujali Kupokea Maombi Ya Kujiunga na Vyuo! Tena Ni Kwa Baadhi Ya Vyuo Viche tu Vya Ufundi.

Kwahiyo Jitahidi Kutafuta Habari Za Kweli Na Achana na Propaganda Za Vijiweni.
 
Hata mi hii habari nimeiona kwenye mitandao nikastuka sana, King gwada naomba kuuliza kipindi nacte wametoa vuo vyao, he kama MTU unataka kuapply online baada ya TCU kuruhusu kuapply itawezekana kwa wenye diploma kuapply degree wakata nacte wameshafunga kuapply?
 
Pia jamani naombeni kuuliza, ni kweli bodi ya mikopo wameanza kuruhu kuapply online?, màana nasikia wameruhusu lkn nikiingia kwenye website yao siioni, msaada anayefaham
 
Hata mi hii habari nimeiona kwenye mitandao nikastuka sana, King gwada naomba kuuliza kipindi nacte wametoa vuo vyao, he kama MTU unataka kuapply online baada ya TCU kuruhusu kuapply itawezekana kwa wenye diploma kuapply degree wakata nacte wameshafunga kuapply?

Baada Ya Matokeo ya F6 na TCU kuanza Kupokea Maombi Basi NACTE nao Watafungua Tena na Watapokea Tena Maombi!
Kwani Nacte Sababu Ya Kueka Vyuo Vya Ufundi tu Bila Ya Kueka Vile Vinavyotoa Bachela Za Afya ni Kwasababu TCU hawajafungua na Wala Hawajatoa Guide Book Yao.
Subiri Utaapply.
 
Pia jamani naombeni kuuliza, ni kweli bodi ya mikopo wameanza kuruhu kuapply online?, màana nasikia wameruhusu lkn nikiingia kwenye website yao siioni, msaada anayefaham
Hakuna Bodi Ya Mkopo iliyoanza Kuruhusu Maombi, Bali Voda Wanakula Buku 30 za Watu tu Kiulaini.
 
Hizi tetesi kwamba mwaka huu chuo ni wale watakaopata div 1 na 2 katika matokeo ya kidato cha sita. Zina ukweli wowote?
 
hizo div ni kwa wale wa koz za afya ila kwa mujib wa guidebook ya body ya mikopo ni kwamba koz za arts, biashara na na ualimu wa masomo ya arts hakuna mkopo
 
Uyu Nae Anamdanganya Mwenzie Akuna Ki2 Kilichobadilika Juu Ya Mkopo Vile Vile Uonavyo Kwa Wale Waliokutangulia Walipata Kwa Dv3 Nawe Utapata Walikuwa Art Wakapata Nawe Utapata Ayo Mengne Na Udaku
 
Wwe Jamaa Kama Wa Art Fanya Maombi Achana Na Kelele Za Mitandao Utajuta Badae Wenzio Wanapewa Ww Ujafanya Maombi Utalalia Mwaka Kijana
 
Back
Top Bottom