Hivi hizi fedha za "toa elfu ushinde mamilioni" ni za kweli?

Mkuu ni bora ubeti timu ikichana utajua kuwa mkeka umechanika, kuliko hao ambao ni uzushi, baba yangu mdogo aliwahi cheza sana hizo mambo akiwa anatamani ashinde gari, mpaka kesho hajawahi shinda na alishatemana na hizo issue.
 
Mfano mnacheza watu elfu moja halafu probability ya kushinda ni mtu mmoja.
What do you expect?

Hata kila siku awe anashinda mmoja kati yenu, kama utakuwa wa mwisho kupata zawadi ni baada ya 1000/365 = 2.7 years, yaani baada ya miezi 32 ndipo utapata zawadi, sasa si ukichaa huo.
 
Hiyo haina tofauti na uibiwe smartphone halafu uende polisi ukatoe 50,000/- wai-track wakwambie njoo kesho kutwa utaenda utawapa tena pesa, hivyo hivyo na hautaipata mpaka utakaposhtuka na kuacha kwenda kuifuatilia. Umepoteza muda na pesa.
 
Kuna hawa wa SMS eti upo kwenye tano bora kushinda 5,000,000 buku yako tu itakufanya uwe mshindi.

Hivi hawa na wale wa tuma kwenye namba hii wana tofauti gani?
 
Huyo jamaa anaskiliza sana redio na tv
Simple tuuh hivi hizo hela wanazotoa kwanini wasifanye matangazo bureeee
(LIWE LAMAANA LAKINI)
 
Ukiona unaitwa sana kwenye fursa, jua kabisa wewe ndio fursa yenyewe.

Akili kichwani
 
Mshindi atapewa mln 5,000,000/

Hapo bahati nasibu inachezeshwa

Mnaliwa 1000 zenu ,wao wakipata mln 50,000,000/ ndy wanakuja itoa mln 5,000,000/ kwenye hyo hyo hela yenu mliyokuwa mnachezea

Wajinga waliwao

Wajinga hawaishi

Wajinga hawasiki

Ova
 
Back
Top Bottom