Hivi hizi bei za vinywaji na vyakula kwenye migahawa ya ndani ya Uwanja wa ndege ni sawa?

Mr Bean.

Senior Member
Jan 25, 2015
185
128
Wanajamii wenye ufahamu na hili.Sina uhakika ni ushamba wangu labda au la.

Leo nikadai kujitutumua nile chakula huku juu tunakopumzika tukisubiria ndege.Katika huu uwanja unaoitwa wa kimataifa wa J Nyerere.

Kuna migahawa na maduka mengi sana Lakini karibu yote yanaendeshwa na wahidi. Hoja yangu sio hao wadosi kumiliki hayo maduka, hoja ni bei za bidhaa katika maduka hayo ndo balaa.

Utadhani hizo products wanazitoa mbinguni. Nimeingia mgahawa mmoja kwa jina la Flamingo Cafeteria nikataka nile wali naambiwa plate ya wali Tsh 27,000.

Nikamuiliza yule mdosi tena nikidhani labda kasahau. Jibu halikuwa tofauti na mwanzo tofauti niliiona katika kuniangalia Mara hii aliniangalia kama vile wale paka wanaomendea chakula kwenye mabaa hupenda sana kukaa chini ya meza za wateja na hasa wakigundua kitu gani mteja anakula.

Basi moyoni nikasema si kitu ngoja nijaribu basi hata Chips pengine hizo zitakua nafuu kidogo. He chips ndo balaa vipande vya viazi ambavyo ukivihesabu havifiki 35 na kijipande cha kuku wa kwenye friza.

Naambiwa nilipie Tsh 21000. Kwa aibu wasinione msumbufu nikaomba nipewe soda Pepsi nikijua pengine hiyo itakuwa rahisi naambiwa Pepsi Tsh3500.

Nikajilambalamba midomo kwa aibu nikatoka nje. Wadau je hizi bei ni halali? au ni kodi kubwa wanayotozwa kwa kuendesha biashara katika uwanja wa kimataifa?

Kama sivyo why?. Sometimes huwa nashindwa kabisa kuelewa maana ya Feeduty.
 
Wanajamii wenye ufahamu na hili.Sina uhakika ni ushamba wangu labda au la. Leo nikadai kujitutumua nile chakula huku juu tunakopumzika tukisubiria ndege.Katika huu uwanja unaoitwa wa kimataifa wa J Nyerere. Kuna migahawa na maduka mengi sana Lakini karibu yote yanaendeshwa na wahidi. Hoja yangu sio hao wadosi kumiliki hayo maduka, hoja ni bei za bidhaa katika maduka hayo ndo balaa.Utadhani hizo products wanazitoa mbinguni. Nimeingia mgahawa mmoja kwa jina la Flamingo Cafeteria nikataka nile wali naambiwa plate ya wali Tsh 27,000.Nikamuiliza yule mdosi tena nikidhani labda kasahau. Jibu halikuwa tofauti na mwanzo tofauti niliiona katika kuniangalia Mara hii aliniangalia kama vile wale paka wanaomendea chakula kwenye mabaa hupenda sana kukaa chini ya meza za wateja na hasa wakigundua kitu gani mteja anakula. Basi moyoni nikasema si kitu ngoja nijaribu basi hata Chips pengine hizo zitakua nafuu kidogo. He chips ndo balaa vipande vya viazi ambavyo ukivihesabu havifiki 35 na kijipande cha kuku wa kwenye friza.. Naambiwa nilipie Tsh 21000. Kwa aibu wasinione msumbufu nikaomba nipewe soda Pepsi nikijua pengine hiyo itakuwa rahisi naambiwa Pepsi Tsh3500. Nikajilambalamba midomo kwa aibu nikatoka nje. Wadau je hizi bei ni halali? au ni kodi kubwa wanayotozwa kwa kuendesha biashara katika uwanja wa kimataifa? Kama sivyo why?. Sometimes huwa nashindwa kabisa kuelewa maana ya Feeduty.
Kuna siku nikawauliza Kama chakula chao kina 3G bluetooth na memorycard wakabaki tu kunishangaa
 
Haya mambo mbona ya kawaida tu..

hata Oman kwenye aiport yao msosi angalau uwe na Rial 5 same na dubai bei ni zile zile


ila huku kwetu wangaliage na kipato cha watu wengi.. dubai, oman tunasema sawa ni transit kwa hiyo kuna watu mbalimbali duniani wanapita pale sasa hapa ambao hatuna ndege inakuwaje?
 
Gharama ya pango, mikataba ya wafanyakazi, ubora wa chakula, aina ya wateja, kipato cha wateja. Inawezekana wewe hukuwa mteja wa pale, siku nyingine tanguliza ugali na matembele nyumbani kwako. By the way kama ni international, ungevizia msosi wa kwenye ndege. Ungevumilia ukipanda tu, unaanza kutafuna.
 
Teh teh umenichekesha hapo uliposema ukajilamba mdomo ukatoka nje ...nlijua ungejikaza kisabuni vipi huyo muhudumu hakua mwanamke ??
 
unashangaa! hujui hapo airport unakuwa upo nusu ulaya nusu tanzania, nakumbuka niliuziwa pampaz ya mtoto moja 12000.
 
Wateja wao ni wale internationals ambao hizo bei kwao ni kawaida sana, we ulijichanganya tu mkuu
 
Nilikua hamna maindi ha kuchoma angalau upoze njaa!!hahahaha hapo sio ubungo kaka siku nyingine kula kabisa nyumbani!!
 
mkuu ungelipia tu,chakula ni buffet,unalipa mpunga wako unakuwa unaenda kujipakulia tani yako.hata urudia mara mia.ts up to you.pia wanalipa pango kubwa sana.ndo maana ikaitwa airport.almost dunia nzima huwezi ukakuta kitu kiwe bei nafuu airport kuliko mtaani.siyo kwa wahindi tu hata maduka ya pale nje,ingia uulizie pen unayonunua 200 huko mtaani,pale ni jero
 
Back
Top Bottom