Hivi hili tatizo la wanawake kuomba wanaume pesa kwenye mahusiano ni Tanzania pekee au ni dunia nzima?

Hivi hili tatizo la wanawake kuomba wanaume pesa kwenye mahusiano ni Tanzania pekee au ni dunia nzima?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,516
Reaction score
46,602
Katika kuangalia filamu mbalimbali za nchi za magharibi, nimegundua kwamba tatizo la kuombana ombana pesa kwenye mahusiano lipo hapa Tz tu, sidhani hata kama Kenya, Uganda au Rwanda wana haya mambo.

Jamani, mwanaume akiingia gharama za outing ambapo analipia usafiri (gari yake), chakula, vinywaji, hotel nk., itoshe! Sio kila siku mara kodi, mara nani sijui anaumwa, mara sijui nini, mara kusuka.., mara vocha.., kwani nyie pesa zenu mnapeleka wapi? Are you disabled?!

Kuna mtu anawakataza kwenda shule? Kuna mtu anawakataza msiombe ajira? Kuna mtu anawazuia msifungue biashara? Kila anachofanya mwanaume hata mwanamke anaweza kufanya, iwe ni kusoma , kuomba ajira au kufungua biashara, hata wanawake wanaweza, sasa iweje kwenye mahusiano muwe ni omba omba?! Whats wrong with u!!
 
ACHA KU DATE NA WANAWAKE WA KISWAHILI/ MASKINI 😊
 
Mbona ni standard dunia nzima, wewe huoni wachezaji wakifanikiwa wanawake wanaomba talaka wagawane mali.
Wao na hela ni vidole vinavyofuatana
 
Jambo ambalo huwa linanikera ni mtu anakutafuta mwenyew kwamba kakumis,unajitahid inabid umtoe out na unampunguzia uzito afu asubuh usipompa hela ananuna

Kuna mmoja aliwah ntafuta nikamwambia siko vzur kipesa kwasasa akanimaind eti kwamba nakosaje hela ya lodge tu,hajui tutakula chakula na hela ya usafir lazima ihusike bado yake yeye
 
Achana na tamthiliya hizo zinakudanganya wanawake matamanio Yao ni kua na mwanaume mwenye pesa Bora sisi watu weusi ila Kwa wenzetu ni balaa wakiona wakatalikiana mambo ya 50/50
Hz muvi wazungu wametudanganya sana,siku hz kidogo wanaigiza hata usaliti kwenye muvi zao lakin zamani ilikuwa ni full upendo watu hawasalitiani kumbe walikuwa wanatuchora tu na wao huwa wanamichepuko
 
Wewe: Mambo vipi, mzima wa afya?

Yeye: Mi mzima tu. (kiufupi hajataka hata kukuuliza hali yako)

Wewe: Ahaa powa, nikasema nikusalimie. Kama vipi baadae basi.

Yeye: ok powa (yaani hataki usumbufu).

Wewe: Mbona unajibu kinyonge au unaumwa. (Unajiingiza kwenye mtego mwenyewe)

Yeye: Siumwi wala nini, sema mawazo tu hapa sijala, umeme ni zamu yangu, kodi yenyewe inaisha keshokutwa na mwenye nyumba amenikumbusha yaani sijui hata nifanyeje (ashakuingiza kwenye mfumo mazima)

Wewe: Duh pole sana, kwa hiyo utafanyaje?

Yeye: My naomba uniazime hata ya kodi tu, nitakurudishia kuna hela yangu ya mchezo nacheza nikiipata tu nakurudishia 🥰

Wewe: Ngoja nijipigepige nadhani haitokesakana hata nusu, unajua sipendi kukuona ukiwa katika hiyo hali. (kuitwa my na kupewa busu la emoji tayari kichwa kishakuwa kikubwa nakutaka kubeba majukumu yasiyo yako)

Yeye: Asante baby 🥰🥰, nakupenda sana. Utanitumia kwenye simu saa ngapi?

Wewe: usijali nitakuja jioni, halafu nimemwagiza Juma akuletee Chipsi kuku.

Yeye: thank you 🥰🥰🥰. Halafu nilitaka kusahau Jumapili ni birthday yangu, nitakuwa na marafiki zangu, si utanisaidia baby kuniandalia party? Yaani nataka party la maana kila mmoja ashangae.. Juzi nilienda ya yule rafiki yangu Mary ilikuwa balaa, watu walikula, kunywa hadi wengine walishindwa kurudi kwao.

Wewe: Sawa tutacheki ngoja niendelee na kazi, bye.
=======================

Nilichogundua sisi wanaume mara nyingi huwa tunatafuta sana kuombwa hizo hela kwa kujilazimisha kwenye mahusiano tusiyotakiwa.
 
Bro, mwanamke anamiliki harrier kanunua kwa pesa yake, na anafanya biashara, ila anaomba pesa ya kodi, ni masikini huyo au ni kujiendekeza?!
Wanawake huwaga wanaumiaga kutumia pesa zao kujigharamia ☺️😊 aiseeee ni Bora achunee Ila kutumia chakwake kwa ajiri ya familia na wewe hawawezi.
 
Pesa ya mwanaume si tu inapendwa na mwanamke wa kibongo ni dunia nzima. Poleni, mkiombwa pesa kama hamtaki kutoa msiwe mnatoa.
 
Back
Top Bottom