Hivi hili suala la mikopo diploma bado lipo?

Lio tz

Member
Joined
Apr 16, 2018
Posts
71
Reaction score
26
Muswada ulishapita bungeni je kuna anayefahamu chochote je ishasainiwa? au itaanza lini?
Wenye Diploma waula,sasa kuanza kupata mikopo

11 months ago Wenye Diploma waula,sasa kuanza kupata mikopo

Serikali imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuwezesha wanafunzi wanaochukua Stashahada katika vipaumbele vya kitaifa, kupewa mikopo ili kuwawezesha kuchukua elimu husika.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako,amesema mabadiliko hayo, yanalenga kuwezesha kasi katika uchumi wa viwanda.

Aidha, Ndalichako amesema mabadiliko katika Sheria Namba 4 ya Mwaka 2016 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), yamelenga kutoa nafasi ya Kada ya Stashahada inayohitajika ambao wamekuwa hawapati mikopo.

“Kwa lengo la kupata usawa na kwa kuwa Diploma nayo iko kwenye Elimu ya Juu, watoto ni wale wale,kuna wengine nao wanashindwa kumudu gharama na ili Serikali ipate uwiano mzuri tumeona ni vizuri kuwe na marekebisho ya sheria,”amesema Profesa Ndalichako.

Hata hivyo, Ndalichako amesema kuna umuhimu mkubwa wa Kada ya Stashahada, hasa wanaokwenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa kwenye msukumo wa Serikali ya Awamu ya Tano wa Ujenzi wa Taifa la Vijana, kama ilivyo kwa wenye Shahada.

Hata hivyo, HESLB imesema kuwa maamuzi ya kusitisha utoaji wa mikopo, ulilenga kutekeleza maagizo ya Serikali, ambapo, Ndalichako amesema kwamba uamuzi wa kusimamisha mikopo hiyo, ulitokana na nia ya Serikali kufanya mabadiliko katika sheria hiyo ili kuipa wigo mpana zaidi kuliko kujikita katika eneo la Sayansi pekee.
 
Kwa utawala huu hizi ni porojo, time will tell
 
Wametangaza rasmi mikopo itakuwepo kwa wanaosomea DIPLOMA. Angalizo ni wale tu "watakao kidhi" vigezo ndio watapata. Vigezo ni pamoja na fedha kuwepo kwa hiyo kuwa na uhitaji tu peke yake haitoshi ingawa inasaidia.
 
Nasikia mwaka huu wanatoa mikopo kwa wanafunzi 80,000 ,so jiandae kupikea booom,, jaza fom yako vizur,,,, boom linakuja soon,,,,,,, kusoma rahaaaaaaaa
 
Je ,inshu ya utoaji mikopo Kwa wanafunzi wanaosoma diploma(stashahada) kwa mwaka wa Masomo 2018/2019 kutoka bodi ya mikopo (HESLB) Ni rasmi?
 
Hizi porojo kwa mambo ya msingi kama haya sijui serikali yetu itaacha linii.....kama ni kweli Magufuri saini haraka kama ulivyofanya kwenye mikataba ya madini jamaniiii
 
Muswada ulishapita bungeni je kuna anayefahamu chochote je ishasainiwa? au itaanza lini?
Wenye Diploma waula,sasa kuanza kupata mikopo

Kwa utawala huu hizi ni porojo, time will tell

Wametangaza rasmi mikopo itakuwepo kwa wanaosomea DIPLOMA. Angalizo ni wale tu "watakao kidhi" vigezo ndio watapata. Vigezo ni pamoja na fedha kuwepo kwa hiyo kuwa na uhitaji tu peke yake haitoshi ingawa inasaidia.

Hata baada ya kutangaza watatoa, wametangaza tena hawatatoa. Nafikiri mafungu ndio yamewaishia au nia ya mgawa mafungu imeyeyuka. Hivyo poleni mlio kuwa mnasubiri haki hii.
 
Hizi porojo kwa mambo ya msingi kama haya sijui serikali yetu itaacha linii.....kama ni kweli Magufuri saini haraka kama ulivyofanya kwenye mikataba ya madini jamaniiii
Washabaki kuwa watu wa siasa lakin wakisimama mbele ya watu wanasema wao sio wanasiasa
 
Back
Top Bottom