Hivi hili ni kosa jamani?

Hivi hili ni kosa jamani?

Ndugu zangu akiwemo mama mzazi wamenichukia kwa kumkabidhi mke wangu tuliyeishi naye miaka 16 kusimamia biashara niliyoanzisha na mke wangu. Wana Jf nisaidieni kwa maoni, hili ni kosa au nilitakiwa kufanya nini ili ndugu zangu waridhike?
huwezi kuwaridhisha wanadamu wote,sasa mtu umemkabidhi moyo wako kwa miaka hyo yote itakuwa biashara?
 
Ebooooooh.....
Walitaka umpe nani asimamie?
Waambie mkeo ni wajibu wake kusimamia, mali zako ni za mkeo na za mkeo ni zako...wao hawana umiliki wa biashara wala mali zako....

Tena kwa ndugu wa namna hiyo nikushauri mapema, kama ulikuwa hujaandika wosia andika mapema, ukifumba macho ghafla watampokonya mkeo hadi vijiko apate shidaa na watoto...

Hawajui kuwa wajibu wako ni kwa familia yako, ambayo ni mke na watoto kama mnao? Wao unawasaidia tu lakini huwajibiki kwao....
Ndugu zangu akiwemo mama mzazi wamenichukia kwa kumkabidhi mke wangu tuliyeishi naye miaka 16 kusimamia biashara niliyoanzisha na mke wangu. Wana Jf nisaidieni kwa maoni, hili ni kosa au nilitakiwa kufanya nini ili ndugu zangu waridhike?
 
Lara 1 u seem to understand my situation very well. Visa, maneno, sabotage utadhani hiyo business ni ya mtu baki. Kweli inanipa shida kuamini ingawa wanafahamu tangu awali kuwa biashara hiyo ni ya kampuni ya familia yangu na shareholders ni mimi na wife

wacha wanune, in time watazoea. Hawa ndugu wa namna hii ukiwaendekeza watakusumbua. Tena waweke wazi kuwa kila ulichonacho ni cha mkeo
 
Siyo kosa hata kidogo. Wala usibadilishe maamuzi yako ya kumpa mkeo asimamie biashara yenu labda kama utaona biashara haifanyi vizuri kama mlivyotarajia. Kuna familia nyingine za mke/mume hawajui mipaka yao pale wanandoa wanapofanya maamuzi yao mbali mbali katika maisha yao wanataka kuingilia na kuwa na sauti katika kila jambo la wanandoa kitu ambacho si sawasawa.

Ndugu zangu akiwemo mama mzazi wamenichukia kwa kumkabidhi mke wangu tuliyeishi naye miaka 16 kusimamia biashara niliyoanzisha na mke wangu. Wana Jf nisaidieni kwa maoni, hili ni kosa au nilitakiwa kufanya nini ili ndugu zangu waridhike?
 
Pole mkuu Sweeper, you know one thing, ukishakua na familia kuwashirikisha ndugu zako katika maamuzi ni optional, family yako inakua separate entity,
Kuwaambia ndugu zako ni heshima tu.
Tell me one thing if what I am thinking it is right, wewe umeendelea kuliko ndugu zako siyo? If that is, nafikiri ndio wanaweza pata muda wa haya yote. . .What to do then, Kuna member katoa ushauri uwasaidie, have a separate plan ambayo haita ku cost in terms of time, money and devotion ya kuwainua ndugu zako let it be kuwasomesha wao or watoto wao, mitaji ya biashara, business ideas, networking assistance and all that. wasione kama umewatupa ukawapa chance ya kuongea.
All the best.
 
Nanyi mtakuwa mwili mmoja na si wawili tena.

Mke ni wako, biashara ni yenu wewe na mke wako + watoto wenu (familia = Baba + Mama + watoto)

Maamuzi yoyote ni yako wewe na mke wako, mkishakubaliana na kuridhika kumshirikisha kiumbe mwingine ni kutia ukakasi katika upendo na maendeleo yenu.

Ukiwasikiliza hao believe me ndoa yako iko mashakani. You and your wife for each and everything forever.
 
Lara 1? For Gods sake unamuonea. Ma wife hana hajui hata kama siku hizi kuna saluni za kucha. Kwa kifupi am in control of all finances


waambie ukweli wewe na mkeo ni kitu kimoja
na ndoa ni kati yenu nyie wawili, tena waeleweshe kuwa mali ni za kwenu na si za kwako peke yako au za kwao!!
Kila mtu asimamie nyumba yake waache majungu
 
kabisa kabisa ....
Inawezekana ndugu wanahofu kuwa biashara ikikabidhiwa kwa mkeo, wao watakosa pa kuegemea na kujipatia chochote!
huwa najiuliza kama hapa duniani tupo kwa ajili ya kusaidia watu wengine, then hao watu wengine wapo kwa sababu gani?
 
kesi za aina hii huwa siachi kumkumbuka nyumba kubwa ,sijui yuko wapi yaillahi!
 
Last edited by a moderator:
Nanyi mtakuwa mwili mmoja na si wawili tena.

Mke ni wako, biashara ni yenu wewe na mke wako + watoto wenu (familia = Baba + Mama + watoto)

Maamuzi yoyote ni yako wewe na mke wako, mkishakubaliana na kuridhika kumshirikisha kiumbe mwingine ni kutia ukakasi katika upendo na maendeleo yenu.

Ukiwasikiliza hao believe me ndoa yako iko mashakani. You and your wife for each and everything forever.

I can see all signs for the red text in your comment
 
Pole mkuu Sweeper, you know one thing, ukishakua na familia kuwashirikisha ndugu zako katika maamuzi ni optional, family yako inakua separate entity,
Kuwaambia ndugu zako ni heshima tu.
Tell me one thing if what I am thinking it is right, wewe umeendelea kuliko ndugu zako siyo? If that is, nafikiri ndio wanaweza pata muda wa haya yote. . .What to do then, Kuna member katoa ushauri uwasaidie, have a separate plan ambayo haita ku cost in terms of time, money and devotion ya kuwainua ndugu zako let it be kuwasomesha wao or watoto wao, mitaji ya biashara, business ideas, networking assistance and all that. wasione kama umewatupa ukawapa chance ya kuongea.
All the best.
You are very right Don mangi. Nashukuru ka advice nzuri
 
Ebooooooh.....
Walitaka umpe nani asimamie?
Waambie mkeo ni wajibu wake kusimamia, mali zako ni za mkeo na za mkeo ni zako...wao hawana umiliki wa biashara wala mali zako....

Tena kwa ndugu wa namna hiyo nikushauri mapema, kama ulikuwa hujaandika wosia andika mapema, ukifumba macho ghafla watampokonya mkeo hadi vijiko apate shidaa na watoto...

Hawajui kuwa wajibu wako ni kwa familia yako, ambayo ni mke na watoto kama mnao? Wao unawasaidia tu lakini huwajibiki kwao....

Thats my worry. I dont find in them affection to my children ingawa hawapendi nimsecond wife kwenye business zangu. Fate ya kids in my absence is uncertain
 
As long as ni shared biznec kati yako na mkeo, waambie nduguzo waelewe kua hata mkeo anahusika............. above ol cmamia unachoamua na kukiamini coz siku zote "baba ni kichwa cha familia ila mama ni shingo"
 
Ndugu zangu akiwemo mama mzazi wamenichukia kwa kumkabidhi mke wangu tuliyeishi naye miaka 16 kusimamia biashara niliyoanzisha na mke wangu. Wana Jf nisaidieni kwa maoni, hili ni kosa au nilitakiwa kufanya nini ili ndugu zangu waridhike?

hao ndugu wana matatizo tena makubwa hata hawafai kabisa. we waache wanune wakipata shida watakuja.
 
Back
Top Bottom