Hivi hili ni kosa au sio kosa?

Hivi hili ni kosa au sio kosa?

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,077
Reaction score
17,267
Kwa mfano mtu amepata taarifa kuhusu jambo la uhalifu lililopangwa kutokea, Let say Kuna mipango inayosukwa kwaajili ya mlipuko wa bomu mahali fulani, na mtu huyo baada ya kupata siri hizo akaamua kuzipost JF,

je, ni kosa kulingana na sheria za JF na za Nchi?
Je, endapo hilo tukio likitokea kweli kuna haja ya kumtafuta mtoa post kwaajili ya kukamilisha upelelezi?

N.B; Baada ya matukio ya polisi wasio wazalendo kuanza kuvujisha data za mtoaji taarifa, hivyo kuhatarisha maisha ya raia wema, naona wengi wanaona bora kutoa taarifa bila kujulikana na vyombo vya usalama.
 
🙂 🙂 tena unaweza hata uhukumiwe kwa kesi ya ugaidi, maana kama ulikuwa unaujua mchongo mapema kwanini usitoe taarifa kwenye vyombo vya usalama?,
utatafutwa, utawekwa chini ya ulinzi ili kulisaidia jeshi la police ikiwezekana na wewe ukaambatanishwa nao pia
 
Sasa kwamfano taarifa umezitolea kwenye vyombo vya usalama pia kuna sababu ya kukamatwa?? Kwasababu nadhani hakuna umuhimu au sababu yoyote ya kuhusishwa na hiyo taarifa
 
Mwenzangu bora ujikalie zako kimya! unaeza kujikuta wanaanza nawewe hata kwenye hii post ya mfano.
Sasa ni sehemu ipi iliyokuwa salama kwa raia kwenda kutoa taarifa(kwa usalama).
Na hata tukio likitokea basi asitafutwe?
Manake hapo itakuwa ni uzembe wa hao polisi kushindwa kuzuia tukio
 
Kama Taarifa utatoa kwenye Vyombo vya Usalama, kwa Uzembe wao wakashundwa kufatilia na jambo kutokea then huna kosa lolote.

Lakini kama hukusema, basi utatafutwa na Polisi uwasaidie katika upelelezi.
 
Sasa ni sehemu ipi iliyokuwa salama kwa raia kwenda kutoa taarifa(kwa usalama).
Na hata tukio likitokea basi asitafutwe?
Manake hapo itakuwa ni uzembe wa hao polisi kushindwa kuzuia tukio
Ndugu siku hizi mambo yamebadilika siku moja uibiwe uone inavyokuwa kwanza ukienda polisi bila kitu kidogo utazungushwa hadi ukome! kingine mie naona neno la ulinzi shirikishi siku hizi siyo dili maana ukiibua maovu nawe unaunganishwa kwenye kesi,cha msingi tuwaache wafanye kazi yao tu.
 
Kama Taarifa utatoa kwenye Vyombo vya Usalama, kwa Uzembe wao wakashundwa kufatilia na jambo kutokea then huna kosa lolote.

Lakini kama hukusema, basi utatafutwa na Polisi uwasaidie katika upelelezi.
Na je, kwamfano taarifa ukizitolea JF. Na polisi wakaziona.
Je, kuna ulazima wowote wa mtoa taarifa kuanza kutafutwa???
Kwani hakuna kifungu cha sheria kinachoruhusu mtu kutoa taarifa pasipo kujulikana? Kwani lazima mtoa taarifa ajulikane?
 
Ulitakiwa utoe taarifa kwenye vyombo,husika sio jf au aina yoyote ya media kufanya ivo uta jeopardize uchunguzi,..kufanya ivo utsababisha majanga mengine makubwa zaidi
 
Ulitakiwa utoe taarifa kwenye vyombo,husika sio jf au aina yoyote ya media kufanya ivo uta jeopardize uchunguzi,..kufanya ivo utsababisha majanga mengine makubwa zaidi
Kwani hakuna namna itakayomuwezesha mtoa taarifa asijulikane hata na polisi?? Kwani lazima ajulikane?
 
Ndugu siku hizi mambo yamebadilika siku moja uibiwe uone inavyokuwa kwanza ukienda polisi bila kitu kidogo utazungushwa hadi ukome! kingine mie naona neno la ulinzi shirikishi siku hizi siyo dili maana ukiibua maovu nawe unaunganishwa kwenye kesi,cha msingi tuwaache wafanye kazi yao tu.
Aisee nadhani polisi wangekuwa wapole tu, manake taarifa nyingi zinaanzia kwetu raia wakawaida, sasa wangeshirikiana na JamiiForums kisha kukawekwa jukwaa la ualifu ili watu watumie hata new ID kupost matukio, naamini tungepiga hatua kwa kiasi fulani
 
BORA UKAE KIMYA MAANA SHUGHULI YA KUSAIDIA UPELELEZI SI KAZI NDOGO.
UNAWEZA KUJIKUTA NA WEWE NI MTUHUMIWA PIA.
 
Kwani hakuna namna itakayomuwezesha mtoa taarifa asijulikane hata na polisi?? Kwani lazima ajulikane?

Tatizo sio kujulikana tatizo ni iyo taarifa ikiwafikia magaidi watachukua uwamuzi UPI badae,..
 
Kibongo bongo ni kosa sababu wana usalama wenyewe na serikali haiamini kama social network ni njia sahihi ya kufikisha taarifa serious.
 
Back
Top Bottom