Hivi hili la Msasani liko sawa?

Hivi hili la Msasani liko sawa?

mujusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2010
Posts
237
Reaction score
58
Inasemekana kuna mvutano kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni imeuza Kiwanja cha wazi Kata ya Msasani. Wakazi wanalalamika na Mbunge wao pia anaelezea ubadhilifu kwenye mikataba ya Kuuza maeneo ya Wazi. ( Source ITV News saa 2 usiku tarehe 10/5/2010). Hii sio mara ya kwanza kwa shutuma kama hizi. Wakazi wa eneo wanapendekeza wahusika wafukuzwe kazi.
Hali hii ndiyo inayosababisha wengine walioko kazini kuendelea na vitendo kama hivi. Mtu anachukua hongo ya Millioni 50 kwa kutoa kibali kwa eneo la wazi halafu ikigundulika anahamishiwa kituo kingine au kufukuzwa kazi ili kwenda kutumia pesa zake vizuri wakati eneo limeshapotea kwa sababu anyemilikishwa kamilikishwa na nyaraka za Serikali, na Serikali huwa haishindi kesi mahakamani kwa hapa kwetu.
Hii inakaa sawa kweli wana JF na itaendelea mpaka lini?
 
mpaka watanzania watakapoamua kubadilika akuna mabadiliko
 
Back
Top Bottom