Hivi hijab ni vazi rasmi bbc swahili?

Hivi hijab ni vazi rasmi bbc swahili?

Status
Not open for further replies.

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,940
Reaction score
7,849
Tv ya BBC swahili ni shirika la kimataifa la utangazaji. Siku si nyingi wameanza kua na mtangazaji mmoja mwanamke kwa taarifa ya habari ambaye huvaa hijab. Nilidhani wana utaratibu namna ya watangazaji wa habari kuvaa. Naona uvaaji wa vazi la kidini kama hijab kwa mtangazaji wa taarifa ya habari unakera hadi mimi nimeacha kutazama hiyo tv wakati wa taarifa ya habari. Sioni kama kuna haja ya mtangazaji kuwaambia watazamaji wake kama 'mimi ni muislaam au mimi ni wa dini fulani' kwa mavazi yake. Ikiwa shirika kubwa kama BBC linaruhusu mwelekeo kama huo kwenye idhaa yake ya kiswahili inaweza kutuletea shida kwenye idhaa zetu za kitaifa. Kwa muelekeo huo BBC wanaweza kuanza kutuwekea watangaza taarifa ya habari waliovalia kininja au kanzu za ibada. Naomba tuchangie bila bila ya jazba.
 
Mbona lile ni vazi tuu kama mavazi mengine, hata Zanzibar watu wanavaa wakati siyo wa iman hiyo unayosema mkuu
 
Acha ubaguzi we we wale masister kule kanisani hawavai hijab?Hilo ni vazi tu na ni uamuzi binafsi wa mtu kuamua kuvaa hilo vazi chukulia mfano mrema ni dini gani na mbona anavaa barghashia?mbona wanigeria wanaume wengi wanavaa kanzu INA maana wote wanaenda mckitini?
 
Hilo ni vazi la kawaida tu mbona sawa tu na mtu kufunga kilemba,vazi baya ni wale wanaofunika hadi nyuso kama Boko Haram.Mimi ni Mkristo na binafsi nampenda Zukhra Yunus na mavazi yake na kiswahili chake murua...& she's such a beauty aliyeoa hapo kalenga goal.
 
Sasa wewe lile vazi linakufanya usiielewe taarifa ya habari au.?
 
Tv ya BBC swahili ni shirika la kimataifa la utangazaji. Siku si nyingi wameanza kua na mtangazaji mmoja mwanamke kwa taarifa ya habari ambaye huvaa hijab. Nilidhani wana utaratibu namna ya watangazaji wa habari kuvaa. Naona uvaaji wa vazi la kidini kama hijab kwa mtangazaji wa taarifa ya habari unakera hadi mimi nimeacha kutazama hiyo tv wakati wa taarifa ya habari. Sioni kama kuna haja ya mtangazaji kuwaambia watazamaji wake kama 'mimi ni muislaam au mimi ni wa dini fulani' kwa mavazi yake. Ikiwa shirika kubwa kama BBC linaruhusu mwelekeo kama huo kwenye idhaa yake ya kiswahili inaweza kutuletea shida kwenye idhaa zetu za kitaifa. Kwa muelekeo huo BBC wanaweza kuanza kutuwekea watangaza taarifa ya habari waliovalia kininja au kanzu za ibada. Naomba tuchangie bila bila ya jazba.

kmbwembwe naomba tulitendee haki jukwaa kwa kuwa na arguments za kiutu uzima. Hiki ulichoandika ni utoto . Wewe una chuki na waislam au mavazi ya kiislam? Sasa hiyo hijab imekuudhi nini? Dada yako anavaaje aendapo matembezini? Mama yako je? Na Masister kanisani kwako je? Sasa kwa taarifa yako Hijab ndio vazi sahihi kwa mwanamke yeyote anayejiheshimu. Acha udini wako hapa!
 
Last edited by a moderator:
Mbona papa wako anavaa gaunii na usikerekee na vazi hiloo

Chukii yako ni mbayaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom