Hivi Hii Ya Marando Imekaaje?

Shinto

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
1,781
96
Wandugu napenda kueleweshwa Mh. Mabere Marando ni mtu aliye mstari wa mbele katika kupiga vita ufisadi na mafisadi akiwa na joho la CDM. Lakini wakati huo huo anakuwa wakili wa Manji (mtuhumiwa wa ufisadi) ili kupinga kumuhusisha yeye Manji na ufisadi. Je hapa hamna conflict of interests? au sio unafiki kabisa?
 
Ndio unafiki wenyewe huo kwani unatakaje, hukujua kwamba Marando ana uchu mkubwa sana wa pesa. hapo yeye atakuja na kauli mbiu yake oooh mimi ni mwanasheria, ooooh mimi namtete amanji ili nijue siri za mafisadi wakati yeye mwenyewe ni fisadi.
 
Siasa za nchi hii ngumu sana ukiona mtu anapiga kelele nje ya boma la Ikulu utafikiri akiwezeshwa kutawala boma hilo atatukomboa watanzania kumbe wapi? angalia tu vitendo kama hivi ni vya kukatisha tamaa. manji ni kada wa CCM kamtega kijanja kwa pesa nzuri akategeka kama samaki aliyenaswa na ndoana. Huyu bwana siasa zimemshinda awaachie wanaozijua
 
Ndugu hiii ni ndio Tz na wanasiasa wake,kumbuka mabele marando ni mwanasheria so yupo pale kikazi kwani asipo fanya hivyo familia yake yaweza kufanjaaaaaa
nadhani tumwache afanye kazi aliyosomea tusimwingilie

msemakweli hapendwiiii daimaaaaaa:popcorn:
 
Kamwe siwaamini wanasiasa wetu, hata awe nani....labda kama watathibitisha wako tofauti tena kwa vitendo na uadilifu wao
 
Sasa inamaana hata kanisani/msikitini anakosali/swali RA wasimkubali coz fisadi? Kutetewa ni haki ya kila mtu hata aliyeua bado anapewa/ anatakiwa kupata wakili upo hapo?
 
Nani alikuambia kuna mwanaseasa anayemaanisha anachosema?
 
kwani mengi sio fisadi??mengi ana personal vendetta na wafanyabiashara wenzake lakini na yeye ni fisadi tu...after all a person is innocent until proven guilty,.that is a general rule,..exception ni RA
 
Wanachadema mnafikiri mmepata kumbe mmepatikana. Chui hata siku moja hawezi kuacha ngozi yake ya madoadoa. Huyu mwanasheria ni mtu yuko kwenye system na hii ni kazi yake ya siku zote. Hela ya dugu Manji tamu sana hawezi acha mimi. Kazi iko!!
 
Jifunzeni kutenganisha siasa na kazi (taaluma ya mtu kufanyia kazi ili kupata riziki). Ila ktk suala la maadili (morality) ya jamii ndio linaloweza kumbana Mabere kama nchi yenu ingekuwa na sheria zenye maadili. Ila kwa jinsi Tz ilivyo sasa Nyaucho yuko sawa.
 
Jifunzeni kutenganisha siasa na kazi (taaluma ya mtu kufanyia kazi ili kupata riziki). Ila ktk suala la maadili (morality) ya jamii ndio linaloweza kumbana Mabere kama nchi yenu ingekuwa na sheria zenye maadili. Ila kwa jinsi Tz ilivyo sasa Nyaucho yuko sawa.
Hivi na wee kumbe umeionaee!!
 
Nadhani hapa kitu cha kujiuliza ni:
1. Je kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Manji ni fisadi papa?
2. Kwa kumtetea Manji, Marando anavunja katiba ya chadema?

Kuhusu kula hela za Manji sidhani kama hilo ni kosa, kwa sababu Marando anakula kwa jasho lake halali; mbona hata Yanga anatoa mamilioni ya pesa na ninyi wengine ni washabiki wa timu hiyo na mnamshangilia na wala sijawahi kusikia hata siku moja mtu akilalamikia hilo.

Suala hili tunatakiwa kuliangalia kwa marefu na mapana yake. Unakumbuka ishu ya marehemu Dito? Kulikuwa na ushahidi wa kutosha kabisa kuwa aliuwa, Zombe alkadhalika lakini bado walikuwepo mawakili waliowatetea kuwa hawajaua.
So suala la Marando usiliweke kirahisi namna hiyo.
 
"The act itself does not constitute guilt unless done with a guilty intent"......Actus non facit reum nisi mens sit res (Sir Edward Coke)

Wanasheria wanaruhusiwa kumtetea mtu yeyote mpaka ithibitike kuwa alifanya kosa.

Manji is innocent until the court proves otherwise.
 
Kazi ya advocate siyo kulinda uhalifu bali ni kusaidia mahakama itoe haki anayostahili mtuhumiwa.
Hivyo basi Marando anfanya kazi kama ofisa wa mahakama anayesaidia haki itendeke.
 
Kesi ya Manji ni ile dhidi ya Mengi....Manji akitaka Mengi amlipe fidia na kumwomba radhi kwa sbb ya kumwita fisadi papa...Manji anachodai ni kuwa Mengi anatumia vyombo vyake vya habari kumchafua na ndiyo kesi anayosimamia Marando....binafsi siamini kama Marando anakosa hapo kwa sbb yeye anasimamia kesi ya mteja wake kuchafuliwa na sio kwamba anamtetea manji kuwa si fisadi au kumtetea Manji kwenye kesi ya rushwa.
 
kwa hiyo kama mimi ni mhandisi au architect, manji akaniajiri nimchoree ramani ya jengo lake atakalojenga kwenye kiwanja alichotapeli nikifanya ivo nifukuzwe au ni msaliti?
 
Wandugu napenda kueleweshwa Mh. Mabere Marando ni mtu aliye mstari wa mbele katika kupiga vita ufisadi na mafisadi akiwa na joho la CDM. Lakini wakati huo huo anakuwa wakili wa Manji (mtuhumiwa wa ufisadi) ili kupinga kumuhusisha yeye Manji na ufisadi. Je hapa hamna conflict of interests? au sio unafiki kabisa?
imekaa ndivyo sivyo mbona greatthinker hamlioni Marando anamtea mengi ikiwa(defendant) na wala siyo Manji hebu weka sawa hii.
 
Baada ya Mungu kuumba mbingu na dunia ..... akamuumba mwanadamu na wote waliozaliwa na mwanadamu huyo wataishi kwa jasho lao. Mungu alitoa Kazi mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya watu. Wahandisi aliwaachia kuendeleza kazi ya uuambaji. Kwa kuumba Wahandisi watakula..... Madaktari wakaachiwa kazi ya kuhakikisha wanyama na wanadamu wanaendelea kuwa na afya njema. ......Kwa udhaifu wa miili yetu madaktari wanakula. ........orodha ni ndefu lakini cha msingi ni kuwa Kwa dhambi za watu Askofu Kakobe, Mzee wa Upako, Sheikh Simba na wengine wote walioitwa kwa jina la Mungu wao wanakula fedha za madhabahuni. Kwa ugomvi na faraka za watu Wanasheria kama Mabere Marando na wenzake wanakula fedha za watu kupitia mlango wa mahakamani. Je, kunatatizo gani? Manji na Mengi wasingefarakana Mabere Marando na wanasheria wenzake wote wasingekuwa na kazi......

Jamani acheni ale kwa kadri Mungu alivyomwamuru na kwa kadri aonavyo tatizo ni pale kweli Manji akiwa ni fisadi na yeye kumtetea kwenye majukwaa ya siasa.
 
Back
Top Bottom