Hivi hii nchi inaendeshwa kwa UBABE ama vipi? Kuna DEMOKRASIA HAPA?

Sharo hiphop

JF-Expert Member
May 17, 2011
660
100
Kiukweli kutoka moyoni mwangu huwa na umizwa sana na hili suala, kwa nini tz inaendeshwa zaidi kwa nguvu za dola?
Utakuta wanafunzi wamegoma tena maandamano ya amani kudai haki zao, lakini polisi wanaingilia kati na kufanya vurugu ikiwa ni pamoja na kuwapiga na kuwajeruhi, mfano kilichotoke chuo kikuu cha Dodoma.
Utakuta vyama vingine vya siasa wanafanya mikutano yao tena ya amani kujadili maswala ya wananchi(wenye nchi) lakini polisi wanaingilia na kufanya ubabe wa kuwapiga hadi kuwaua wananchi, mfano kilichotokea Arusha miezi michache iliyopita kwa wana Chadema,
sasa tujiulize ni kwamba viongozi wa nchi hii ni wababe au nini? Au hatutaki changamoto? Au hii nchi kisirisiri ni ya kidikteta?

Jamani karibuni, hili huwa linaniuma sana, natamani ningekuwa mtu fulani niwateketeze wote wanaotumia ubabe usio na maana.
 
Kwani wanachopigania vyama vya upinzani ni nini? Wewe hapo ulipo anza kuwaamsha ulio karibu nao. Waambie nguvu ya kukabili ubabe ni moja tu: nguvu ya umma! Waielewe na kuitumia.
 
Kwa kweli hata mimi naona kama nguvu kubwa inatumika bila sababu!! Hapa serikali inakosea!!
 
hii ndo tanzania mwenye nguvu ni mwenye nguvu tuu ila muda unakuja kitaeleweka tuu kwanini kisamvu hakiivi kikikatwa katwa mpaka kipondwe
 
Back
Top Bottom