Hivi hawa nao wanaitwaje?


Jamii ni nani?
 
Unadhani ni kwanini?

Nadhani ni kutokana na kutojitambua na ujinga uliopo ndani yetu haswa huu mfumo dume. Haiwezekana watu wawili wa jinsia tofauti wafanye kosa moja la uzinzi. Kwa mwanamke ikaonekana ni umalaya but kwa mwanaume ikaonekana ni ushujaa. Kwani wote hawajazini?, kwa nini mmoja ahukumiwe na mwingine asifiwe?
Tunawajaza ujinga kwa kuwasifia wanaume wasiojitambua. Kwa sababu mwanaume anayejitambua hatofungua zipu yake hovyo kwa wanawake, na hata ikitokea amefanya hivyo nafsi yake itamsuta na sio kwamba ataona ni sifa kuwa mzinzi. Yani mtu unajitambua utaanzaje kuona sifa kulala hovyo na wanawake?
 
Kwanini unadhani mwanaume kujidhalilisha kwake ni sifa?

Kufanya hivyo kwetu sisi si kujidhalilisha, ni asili yetu tangu enzi na enzi.
Ndiyo maana mwanamke akiingiliwa na wanaume wengi anakuwa kadhalilishwa, lakini mwanaume akiwaingilia wanawake wengi ni kawaida. Ndiyo maana umeleta huu uzi hapa kwa sababu hata wewe hujui kwa nini ni kawaida kwa sisi kushepuka na hatuna jina la kuchepuka kwetu.
 

Binafsi sipendi kabisa kuingilia maisha na machaguo ya watu wengine. Hivyo suala la wadada kuvaa wapendavyo halinisumbui hata kidogo.

Tanzania kuna sehemu nyingi tu wamama huachia wazi nyonyo zao. Juzi juzi tu hapa nilikuwa natoka Lamadi nikienda Dutwa na njiani tukaona mama kabeba kuni huku kifua chake kikiwa wazi kabisa na sikuona mtu yeyote yule kwenye Hiace aliyechukizwa.

Kinachonisumbua ni watu kujichukulia sheria mkononi.

Hivi kimsingi, kumvua mwanamke nguo hadharani na kumpiga mtu (hadharani) hadi kufa kisa tu zimepigwa nduru za 'mwizi, mwizi', kuna tofauti gani?

Tanzania hayo matendo mawili hutendeka hadharani na wenye dhamana na mamlaka ya kutekeleza sheria hawafanyi lolote.

Bottom line, hakuna mtu mwenye haki ya ku impose maadili yake kwa mtu mwingine. Utovu wa maadili kwako unaweza usiwe hivyo kwangu. Tunaishi kwenye jamii anuai hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu na wastaarabu kwa wale walio tofauti nasi.

Mimi sipendi kabisa yale mavazi ya nikab. Lakini najitambua kiasi cha kuweza kuheshimu uhuru wanawake wanaoyavaa na sina haki ya kwenda kuwachania kisa tu mimi siyapendi.

No one has a right to impose his/ her morals on anyone.
 
Binafsi naona tatizo linaanzia hapo red. Hatuna mfumo unaoeleweka unaosimamia sheria kwa umakini na uthubutu. Kama kweli sheria zikisimamiwa vizuri, hakuna mtu awezaye kumvua mwenzake nguo [iwe kwa sababu yoyote ile] au kuua mtu kisa kaiba kuku au simu. Lakini watu wanakuwa na hasira kwa sababu mfumo wa kisheria/mahakama umejaa ufedhuli na rushwa. Mtu amekamatwa leo, kwa kesi kubwa...kesho anaringa mtaani, watu wanakuwa na hasira. Still, hamna mwenye mamlaka ya kuchagua lifestyle ya mwenzake.

Ulimwengu wa tatu una shida nyingi, niliwahi shuhudia sehemu flani, jamaa kampiga mkewe kibao.....yule jamaa alishitakiwa na kuwa charged kwa kumlamba kibao kimoja tu. Kwa nchi kama TZ, domestic violence kwa mfano liko kwa hali ya juu sana
 

You are absolutely right on the money. Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuchagua au kumpangia mwingine maisha yake.

Kuhusu kuua watu hadharani, ambacho huwa sichoki kushangaa ni pale sura za hao wauaji kuonekana dhahiri. Tena kunaweza kukawa hata video ya tukio lakini hakuna hata mmoja atakayekamatwa hata kwa lengo la kuhojiwa tu, achilia mbali kushitakiwa.

Walau kule Kenya, baadhi ya hao wahuni waliomchania huyo dada nguo zake wamekamatwa na mkurugenzi wa mashitaka kamsihi huyo dada ajitokeze aende akaandikishe malalamiko yake kwa lengo la kufungua kesi.

Ingekuwa huku kwetu huyo dada angeishia kutetewa na Nyani Ngabu tu huku JF huku wanawake wenzake wakiunga mkono kitendo alichofanyiwa.

Ulimwengu wa tatu una shida nyingi, niliwahi shuhudia sehemu flani, jamaa kampiga mkewe kibao.....yule jamaa alishitakiwa na kuwa charged kwa kumlamba kibao kimoja tu. Kwa nchi kama TZ, domestic violence kwa mfano liko kwa hali ya juu sana

Huwezi kuona uhalifu kama huo wa mtu kuchaniwa nguo zake unatokea NYC au London halafu hatua kali za kisheria zisichukuliwe.
 
Aagghh toka nakua hadi sasa mama huwa anasema mwanaume huwa hakosei hii kauli inanikera nikiuliza kwanini anaipenda kauli hio toka zamani hanipi majibu ya kuridhisha
 
Mtoa mada unataka kick kwa wanawake umu huna lolote unalouliza.....ila jua tu mwanaume ni simbaa
 

Ume maliza mkuu!
 
Aagghh toka nakua hadi sasa mama huwa anasema mwanaume huwa hakosei hii kauli inanikera nikiuliza kwanini anaipenda kauli hio toka zamani hanipi majibu ya kuridhisha

Jibu lake ni kwamba baba yako hakukosea!
 

Mkuu neno malaya linatumika kwa mwanamke anayejiuza,lakini vilevile malaya hutumika kwa mwanamke au mwanaume mwenye tabia ya uzinzi.
 
Nature ndiyo inayoexplain establishment of living organism, and how they interact

Hujaelewa nilichokuuliza ...

Sijauliza kazi ya nature ....

Nimekuuliza sababu za nature kulaaniwa halafu nimekuuiza hiyo nature ni nini .....

Haya jibu basi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…