Hivi hapa iliwezekaje jamaniiii!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi hapa iliwezekaje jamaniiii!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by firstcollina, May 26, 2010.

 1. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wajumbe leo naomba niulize jambo nipate hekima zenu,

  Miaka ya nyuma wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere jambo hili lilikuwa linawezekana, wanafunzi walilipiwa ada, walipewa fedha za matumizi hasa wale waliokuwa shule za kulala vyuo na kwingineko. walipewa fedha alimaarufu kama kichele, japo ilikuwa ndogo lakini iliwasitiri sana, walipewa sabuni, mafuta na hata wakati mwingine walipelekwa kwa treni na mabasi yaliyokuwepo. Chakula ilikuwa si shida... maana walipewa na waliula vizuri.

  Hayo yote yaliwezekana licha ya ukweli kwamba nchi ilikuwa na watu wachache na hivyo uzalishaji mali ulikuwa mdogo. Vilevile ikumbukwe wakati huo haikuwa rahisi kuzalisha ziada maana hata nyenzo zilikuwa duni, lakini juu ya elimu liliwezekana.

  Sasa tatizo ni kwanini mambo hayo siku hizi hayawezekani? Au ndio kusema haya kuwa na tija kwa taifa? Leo vyanzo vingi vya uchumi vinatumiwa. Madini(Tanzanite, Dhahabu,Almas n.k) Maliasili wanyama na misitu pia. Kikubwa zaidi wakati huu hata misaada toka nje imekuwa ni mingi ukilinganisha na enzi zile lakini yet haiwezekani..... Pamoja na kwamba wazazi wanajitolea kwa kuchanga michango mingi tu tena mbalimbali lakini serekali inashindwa nini kufanya yale ya kipindi kilee......

  Kwa sasa watu ni wengi....kweli. lakini pia uzalishaji nao pia umeongezeka, makusanyo ya kodi nayo siyo haba. Najiuliza kwanini kule iliwezekana licha ya hali ngumu in both Social, Political, Economic and Technological aspects. Leo hii licha ya kuwepo hayo yote still haiwezekani wajumbe nisaidieni........!
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwangu jibu ni rahisi, priority ilkuwa elimu na afya na kile kidogo tulichozalisha chote kilikwenda hazina sasa tunachozalisha kingi kinakwenda kwenye mifuko binafsi very sad.
   
 3. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2010
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Simple maths
  1)Hesabu mashangingi mangapi serikalini
  2)Watoto wangapi wa vigogo wanasomeshwa nje
  3)Allowance,accomodation,transport na perdiem za Viongozi wakiwa safarini nje na ndani
  4)Mishahara ya wabunge

  List ni ndefu,hiyo list kidogo tu ian toafauti kubwa na enzi za JKN na cha ajabu, ni wote hawa ambao wako serilakilini wamepitia shule na matibabu bure enzi za Nyerere lakini leo ndio ma selfish wakubwa
   
 4. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Luteni nimekupata ndugu yangu, lakini hazina si bado ipo palepale na haijakufa...... Tunachozalisha leo si kinaenda hazina...? Priority ni kweli Afya, Elimu ilipewa kipaumbele lakini hata leo serekeli inasema vivyo hivyo Elimu, Afya tena na Kilimo..... lakini wapi bwanaaaa.. It is true, very very Sad
   
 5. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  I wish ningepitia kipindi hicho maana sasa hali tulionayo sasa ni aibu tupu, kwetu sio kina kabwela tunazidi kupata taabu!
   
 6. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yes! Lakini ni jinsi gani tuna weza kuibali hali hii maana mawazo ya haiwekani ni mawazo ya Mfu tu
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,504
  Trophy Points: 280
  Swali lako ni zuri sana..tena miaka ile makusanyo ya kodi hayakuwa makubwa kama leo dhahabu yetu ilikuwa haijaanza kuchimbwa...ongezeko la mapato lote limeishia kwenye mishahara na marupurupu makubwa ya waheshimiwa na matanuzi yao ya hali ya juu. Wamewekeza kwao tu na kusahau sehemu nyeti kama elimu, kilimo na hospitali. Kuna madarasa yetu mengi tu nchini hayana hadhi hata ya kuitwa choo achilia mbali kuitwa darasa.
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Simple.......back then it was a priority.
   
 9. masharubu

  masharubu Senior Member

  #9
  May 26, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na mimi nakumbuka watoto wa wakubwa wakisoma shule za wazazi mfano abdallah kawawa akisoma boza pangani enzi zile za miaka ya 80, kweli mipango sio matumizi kingwendu aliimba. Jk wakati anaomba kura alikua na mipango mingi sana sasa sijui ule mfuko uliokuwa na document zile aliziwacha wapi?kweli wanasiasa waongo sana na hili linanikera hasaa
   
 10. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo yaliyovuruga hapa katikati kama Structural Adjustment Programmes (SAPs), neo-liberal policies (globalization), kuvunjika kwa USSR, muungano wa West na East Europe, kuongezeka kwa idadi ya watu bila mipango mirefu na endelevu, ufisadi, vita vya Kagera, kuchanganya biashara na siasa, na mengine mengi uyajuayo wewe.
   
 11. doup

  doup JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  100% naunga mkono
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  wala hujakosea Luteni

  Mkullo anakuambia wanapunguza matumizi yasiyo ya lazima baada ya wafadhili kudinda. Kwahiyo anataka kutuambia siku zote serikali yetu imekuwa na matumizi yasiyo ya lazima?

  Inakatisha taamaaa sana kwa kweli:angry:
   
 13. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  MR, wabenzi wanaendelea kutanua kwa rasilimali zetu

  Mimi nafikiri viongozi wetu hawajui consequences ya mgawanyo mbovu wa rasilimali baina ya matabaka mbalimbali kwenye nchi kama ya kwetu
   
 14. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hayo tunayajua vizuri sana, Tena sisahau kuwa hata nchi yetu ilibadili mfumo mzima wa siasa kwa wakati huo, ili kulinda maslahi yake kwa mapana zaidi. Ikiwemo Siasa ya kutofungamana na upande wowote. Ilitupa marafiki wengu kuliko hata pale mwazo.
  Nahisi ukitazama kwa undani hivyo siyo kigezo kikubwa sana vya kutufanya turidhike eti kwa sababu nchi ilipigana vita vya kagera. Vietinam, Congo na nchi nyingine nyingi tu zilipigana mpaka wakanza na moja. Today wako wapi compared to us?
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka nilisoma na watoto wa Dk Salmin Amour.....sijui leo kama hata wajukuu zake waweza soma shule zetu za TZ
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tatizo la Umaskini wa Tanzania ni kutokana na baadhi kama si kwa sababu ya yafuatayo:
  1. wakati wa nyerere pamoja na kujitahidi kutoa huduma bure uzalishaji ulikuwa chini na watendaji hawakujua kuendesha mashirika kwa faida, pia kupeana madaraka kwa kutumia ukada wa CCM kuliharibu mashirika mengi.
  2. Baada ya mwl. nyerere kuanchia ngazi nchi haikua na hata senti moja ya akiba, mzee mwinyi aliona njia pekee ya kukwamua nchi ni kufungua milango ili bidhaa ziingie, hapo makosa yaliyofanyika ni kwamba nchi haikujiandaa kufungua milango kwa hiyo wezi na matapeli wengi walitumia nafasi hiyo kuiibia nchi. Pia mzee mwinyi alishindwa kukusanya kodi walau hata kidogo.
  3. Mkapa ameingia akajitahidi kukusanya kodi kweli mapato yakaongezeka lakini wazungu wakambana ili awauzie madini, wanyama, n.k.
  4. Lakini kubwa zaidi ktk kukwamisha nchi hii ni CCM kutokuwa na nia ya dhati ya kutenda haki. Mikataba inayoingiwa na watawala wa CCM 90% yote ni ya wizi baada ya wao kuchukua 10%.
  Kwa sasa watanzania tuamue kuchagua chama chenye sera tofauti na mambo yatabadilika.
   
 17. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mhh
   
 18. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Mahali penyewe ni hapo penye nyekundu! Kipindi cha Mwinyi kidoooogoo kulikuwa na unafuu fulani hv lkn ukapa ukaingia baada ya kuingia hapo kwenye nyekundu!
   
 19. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Msisahau kuwa kipindi fulani cha hapo nyuma, Bunge letu lilikosa meno KABISA yaani lilibaki ku-symbolize unit badala ya kutenda yaliyolipasa kutesa. Wabunge nao walipoteza sifa yote ya kuwa wabunge maana walikaa kimya wakati sehemu kubwa ya wananchi wakiweka matumaini mikononi mwa wabunge ili kuipata ile haki yao ya msingi iliyopotea au kuhujumiwa na wachache.

  Recently! Bunge likapata damu mpya na changa, watu wenye hoja tena wenye itikadi mbalimbali, hoja motomoto zilianza kuibuka Bungeni, Bunge likawaka moto. Kibaya zaidi katika hatua hii badala ya wabunge kuongeza nguvu na mshikamano katika hoja hizo motomoto ili kupata kile tunachokiosa(Haki ya wanyonge walio wengi), wabunge wakageuka na kuanza vita vya chinichini tena baina ya wao kwa wao .....! Hapa najiuliza yote haya ni kwa maslai ya naniiii!
   
Loading...