Hivi hakuna njia ya kuwashitaki TANESCO

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,982
2,915
Hili shirika la umeme ambalo ni monopoly serikali ingeruhusu wawekezaji binafsi waanzishe makampuni binafsi ya kusambaza umeme kuleta ufanisi katika sekta hii.
Yani hawa TANESCO huduma zao mbovu umeme wanakata bila taarifa kila mara. Huku ninapoishi haipii siku mbili lazima tushinde bila umeme tena siku za kazi mfano leo hapa wamekata umeme kurudisha saa 11 au 12.
Sasa mtu kama biashara yako inategemea umeme ndiyo wamekwisha kuingiza hasara sijui hata Tanzania ya viwanda itatokea wapi kwa huduma kama hizi.
Kwa haya mambo uwa najiuliza hivi haiwezekani mtu ukawaburuza mahakamani kuwadai fidia kwa kuharibu uzalishaji wako?
 
Back
Top Bottom