Habari za jumapili wakuu, napenda kuchukua nafasi hii kutaka kujuzwa hasa na wakazi wa mkoa mpya wa geita ambao bado miundo mbinu yake ni mibovu....! Nauliza hivi huyu mbunge wa jimbo la geita yupo wapi? Mbona haeleweki hata kiduchu? Yani toka amechaguliwa mwaka 2010 hata kugeuka kusema asante wa wapiga kura wake hawezi au ndo dharau kwa vile alishapata??? Popote alipo mfikishieni salamu za wakazi wa geita, najua atajichanganya 2015 agombee tena ndipo atajua tumeshachoka au la
Kwani kuna mbunge wa mkoa au jimbo? Mbona na wewe unakuwa kilaza?
jamaa mshenzi kweli wakati wa uchaguzi alikuwa anajiita jembe, sikuhizi ukimuita jembe anajibu jembe mamayako
ha ha ha nimecheka sana ...jamaa mshenzi kweli wakati wa uchaguzi alikuwa anajiita jembe, sikuhizi ukimuita jembe anajibu jembe mamayako
ha ha ha nimecheka sana ...
Enyi watu wa Geita, mnamtafuta Mbunge wa nini?
- Si mlimalizana naye wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu? Aliwapa hela, ubwabwa, chumvi, kapelo, kanga, t-sheti na vilemba; nanyi mkamchagua kwa kishindo baada ya kupokea vitu hivyo!
- Hamkujua kama ile ilikuwa biashara?
- Hamkujua kuwa ninyi wenyewe mliamua kuwa thamani ya kura zenu kwa miaka mitano ni chumvi pakti moja moja na ubwabwa wa shughuli?
Yuko bize bana, na tena msimsumbue, muacheni arudishe pesa zake alizotoa kukuhongeni.
Tulieni myameze maumivu taratiiiiiiibu bila kelele kama mlivyokubali kuhongwa kimya kimya. Mnae huyo, mpaka 2015 labda mtatia akili japo kidogo. NASEMA TOKENI HAPA!
Sababu kubwa iliyompa ubunge ni kujenga choo cha umma na garden ya kupumzikia basi raia wakamwaminia ile mbaya!!
Walimchagua Donald Max wakawa wanamwita jembe,sasa jembe limelima kwenye rami limeishiwa makali!
Kazi yake imebaki kunywa pombe na kutanua na walembo hili ni funzo kubwa kwa wanageita 2015 msifanye tena kosa hakuna jembe ndani ya ccm.