Hivi Dr. Omar Ali Juma alifariki 2005?

Hivi Dr. Omar Ali Juma alifariki 2005?

Tuwaseme

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
645
Reaction score
1,197
Kama ntakuwa sijakosea, Lubuva nimemsikia akisema Dr. Omar ali Juma alifariki 2005.

Hivi ni kweli, sio wakati ule wa rais mkapa?

=======

Dk. Omar alizaliwa tarehe 26 Juni, 1941 katika kijiji cha Wawi, Wilaya ya Chakechake, Kusini mwa Mkoa wa Pemba.

Elimu yake ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi ya wavulana ya Chake, ambayo kwa sasa inajulikana kama Shule ya Msingi Michakaini tangu mwaka 1949 mpaka mwaka 1957.

Elimu ya sekondari aliipata katika Shule ya Sekondari ya Euan Smith Madressa, ambayo nayo hivi sasa imebadilishwa jina na kuitwa Shule ya Sekondari ya Haile Selassie tangu mwaka 1957 hadi 1960. Kuhusu elimu ya juu aliipatia kwenye vyuo mbalimbali tofauti vilivyomo nchini Tanzania na nje.

Alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha Moscow State, ambako alimaliza mwaka 1967 na pia mwaka 1969 alimaliza katika Chuo Kikuu cha Cairo, Misri.
Pia alisoma Chuo Kikuu cha Edimburgh ambapo napo alimaliza masomo yake mwaka 1977, akapata nafasi tena ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Florida, Marekani na alimaliza mwaka 1980.

Dk. Omar aliendelea na masomo yake na mwaka 1982 alikuwa mmoja wa wahitimu katika Chuo Kikuu cha Reading, Uingereza na pia kiongozi huyu alipata fursa ya kwenda kusoma katika Chuo cha Kivukoni Ideological mwaka 1982.
Shughili za Kiserikali

Dk. Omar Ali Juma alikuwa mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tangu mwaka 1967 hadi mwaka 1984 ambapo alihamishiwa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1995 hadi alipofariki dunia.

Alipokuwa mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) alishika nyadhifa nyingi kubwa.

Mwaka 1967 - 1969 alikuwa Ofisa Wanyama Msaidizi, mwaka 1969 - 1970 alikuwa Ofisa Wanyama na mwaka 1970 hadi 1971 alikuwa Ofisa Wanyama Mwandamizi.

Mwaka 1971 -1972 alikuwa Ofisa Mifugo, pia alikuwa Ofisa Mkuu wa Mifugo katika miaka ya 1972-1978.

Wakati mwaka 1978-1984, alifanikiwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mifugo, mwaka 1984-1987 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Zanzibar, na Januari 1988 - 1995, alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 
Lubuva amechemka...Dr Omari Juma alikufa gafla tena usiku wa dhifa ya kitaifa walimwandalia rais Kabila (mtoto) si kipind cha uchaguzi...then aliekufa kipindi cha uchaguzi ni mgombea mwenza wa Mbowe...hakuwa ccm
 
Kama ntakuwa sijakosea, Lubuva nimemsikia akisema Dr. Omar ali Juma alifariki 2005. Hivi ni kweli, sio wakati ule wa rais mkapa?
Suala la msingi ni je Uchaguzi Zanziber,haukiendelea kama kawaida?Msilazimishe mambo, mtawafanya watanzania Wasiwamini kwa kila jambo sasa.
 
hilo swali kamuulize makamba jr. au subiri waje.... wako njiani wanatokea lumumba
 
Mie toka Aman Karume aseme kwamba.....namnukuu "nyinyi nyote hata msiponipa kura zenu,kura yangu na ya mke wangu mama Shadya zinanitosha kuingia ikulu",huwa sifuatilii tena chaguzi za kisiwani,yaani hawa viongozi wa ccm wamejigeuza miungu watu wanaona kama nchi yao wao na familia zao.
 
Mi nakumbuka 2001..july....nilikua form one...kilikua ni msimu wa saba saba ...lol

Ni kweli hata mimi nakumbuka jana yake alikua sabasaba nadhani ni kati ya tarehe 3-6 july 2001...
 
Lubuva amechemka...Dr Omari Juma alikufa gafla tena usiku wa dhifa ya kitaifa walimwandalia rais Kabila (mtoto) si kipind cha uchaguzi...then aliekufa kipindi cha uchaguzi ni mgombea mwenza wa Mbowe...hakuwa ccm

In preparation for the 2005 elections, Mbowe was nominated as CHADEMA's presidential candidate.[SUP][2][/SUP] Jumbe Rajab Jumbe, a Zanzibari was chosen as his vice-presidential candidate. The election was originally scheduled for 30 October 2005, but was postponed until 14 December due to the death of Jumbe.
https://en.m.wikipedia.org/wiki/Freeman_Mbowe
 
wazanzibar wamepga kura 5 lkn sasa hv kura 4 kati
ya 5 zimekuwa batili na kura 1 tu ya Urais wa
Jamhuri imekuwa halali? Kura zimepgwa na mtu 1,
kituo ki1, kitambulisho 1 na mda m1 hlf 4 ziwe feki
na 1 iwe halali? ONLY POSSIBLE IN TANZANIA
Ni balaa. Tanzania kila kitu kinawezekana.
 
Fijisu kwa nn ccm wasiunde kamat ili team yetu ya taifa ifanye vzur tena kwa goli hili la mkono watachukua hata kombe la dunia
 
wazanzibar wamepga kura 5 lkn sasa hv kura 4 kati
ya 5 zimekuwa batili na kura 1 tu ya Urais wa
Jamhuri imekuwa halali? Kura zimepgwa na mtu 1,
kituo ki1, kitambulisho 1 na mda m1 hlf 4 ziwe feki
na 1 iwe halali? ONLY POSSIBLE IN TANZANIA

mtapewa kura za wazanzibar wote kama laki nne hivi mulizike maana hatuna cha kuwasaidia
 
Mie toka Aman Karume aseme kwamba.....namnukuu "nyinyi nyote hata msiponipa kura zenu,kura yangu na ya mke wangu mama Shadya zinanitosha kuingia ikulu",huwa sifuatilii tena chaguzi za kisiwani,yaani hawa viongozi wa ccm wamejigeuza miungu watu wanaona kama nchi yao wao na familia zao.

nchi ya kimapinduzi haichukuliwi kwa karatasi-samia
 
nchi ya kimapinduzi haichukuliwi kwa karatasi-samia


Yaaan wana kiburi cha ajabu,ukimuuliza huyo mama nini maana ya mapinduzi atakwambia ni rais kupigwa risasi na kuuawa bila kujua kwamba hata mapinduzi kwa njia ya kura yanawezekana..hakuna marefu yaso na ncha ipo siku.
 
Rais Kagame kapiga marufuku television yoyote ya nchi yake kuripot uchaguzi wa Tanzania kwa madai kua ni wa kipumbavu na hauna maana yoyote.Ni baada ya kushuhudia yaliyotokea zanzibar....source star tv
 
Suala la msingi ni je Uchaguzi Zanziber,haukiendelea kama kawaida?Msilazimishe mambo, mtawafanya watanzania Wasiwamini kwa kila jambo sasa.

Hii nyongo ya Zanzibar CCM mtaharisha hadi utumbo.
Soma hii:
I'm just thinking aloud. Mie ni mzenji. Nimeamka asbh kwenda kituo cha kupigia kura. Nilipofika nikamkuta MTU anaitwa msimamizi wa uchaguzi kwenye hicho kituo (je alikuwa wa NEC au ZEC?). Huyo msimamizi akanipatia fomu 5. Moja akaniambia nimpigie diwan nimpendaye. Ya pili akaniambia nimpigie muwakilishi nimpendaye. Ya tatu akaniambia nimpigie mbunge wa bunge la muungano nimpendaye. Ya nne akaniambia nimpigie rais wa zenji nimpendaye. Ya mwisho akaniambia nimpigie rais wa muungano nimpendaye. Nami nikaenda kwenye kikabati nikawapigia wale niwapendao. Nikadumbukiza kura zangu kwenye masanduku accordingly. Nikachovya kidole kwenye wino kisha nikataka kulinda kura yangu afande akaniambia no rudi home ukale ulojo na alua zako (huyo afande alikuwa wa NEC au ZEC?). Baadaye naambiwa uchaguzi wangu umefutwa. Itakuwaje tuseme (logically, legally & constitutionally speaking) kwamba eti uchaguzi niloufanya kwa mbunge wa bunge la muungano na rais wa muungano havikuathirika?????

Does his justice Lubuva need us to have PhDs to understand that logic????

Come on justice Lubuva!!!
 
Back
Top Bottom