Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,156
Nimemsikia Dr Bashiru akilalamikia sana huko Morogoro kuwa watu wanaojitokeza kupiga kura hivi sasa ni wachache sana na idadi hiyo inazidi kushuka kadri siku zinavyosonga mbele
Lakini Dr Bashiru amejiuliza chanzo cha watu hao wanaopiga kura kupungua kwa kasi hiyo ya kutisha??
Ngoja mimi nimpe jibu la moja kwa moja kuwa chanzo cha kupungua huko ni CCM wenyewe.
Nitajaribu kuelezea ni kwanini CCM ndiyo adui namba moja ya kupungua wapiga kura
1. Unapoenda kwenye uchaguzi ni lazima uyakubali matokeo ya aina 2/ ambayo ni kushinda na kushindwa. Lakini kwa Bahati mbaya sana hivi sasa CCM wanaingia kwenye hizo chaguzi wakiwa na uhakika wa asilimia 100 wa kushinda chaguzi hizo!
2. Tume ya uchaguzi haiko huru katika muundo wake, kwa kuwa kuanzia Mwenyekiti hadi wajumbe wake wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais wa nchi, ambaye chama chake ni mmoja ya washindani, jambo linalofanya wananchi wakose Imani na Tume hiyo
3. Matumizi makubwa ya vyombo vya ulinzi katika chaguzi hizo, hususani Jeshi letu la Polisi, nayo inawanyong'onyeza sana wananchi. Iweje tunafanya uchaguzi ulio huru na haki kuwe na askari wa Jeshi la Polisi walio wengi kama vile nchi iko vitani?
Hizi ndiyo sababu zangu juu za watu kutokwenda kwenye vituo vya kupigia kura na kama hatua za haraka zisipochukuliwa, tusije shangaa katika chaguzi zijazo tukawaona Wasimamizi wa uchaguzi na askari Polisi kuwa ndiyo pekee ya watu watakaoonekana kwenye vituo hivyo wakati wa kupiga kura!
Mungu ibariki Tanzania