instanbul
JF-Expert Member
- Jun 26, 2016
- 11,381
- 14,186
Nasubiri siku ya kesho kuangalia atakachoongea mheshimiwa kuhusu Yale aliyoyatekeleza miaka mitano mjini Bukoba.
Kimsingi mji huu yaani manispaa hii hakuna kitu chochote kutoka serikalini kilichotekelezwa.
Barabara za mji ni ndogo na mbovu zote wakati hata hazifiki 20 km lakini wakazi wa mji huu wanasikia maflyover na madaraja ya baharini yakijengwa huko Tanzania.
Mji huu mkongwe ulioanzishwa mwaka 1890 hauna stendi ya mabasi na daladala mpaka Leo hii. Kuna kiuchochoro flani chenye tope jekundu ndo hupaki magari. Wakati huko Tanzania hata wilaya na vimiji vidogo vina stendi kubwa Tu za kisasa.
Mji huu hauna jengo lolote la maana la serikali. Yaani hata makao makuu ya NIDA, TANESCO ni vijumba vidogo. Hata makao makuu ya CCM mkoa ni gofu flani wakati huko Tanzania kuna mikoa inajenga miji ya kiserikali kama Chato na Geita nk
Mji Una soko kuu la mabati ambalo mvua ikinyesha ni kama dampo flani la mji. Wakati huko Tanzania kuna masoko ya kisasa.
Mji huu taa zake huwa haziwaki, mji umejaa vibaka kama wote ndio maana hata 2015 watu walikuwa wanakatwa makoromeo na kuchoma makanisa. Wakati huko Tanzania kuna miji midogo Sana ina mpaka traffic lights.
Wakati NHC wakijenga maghorofa marefu huko Tanzania, Bukoba kumejaa magofu ya 1957 ambayo nayo yalinyanganywa wahindi na kuyataifishwa ambayo hayafanyiwi ukarabati hata kidogo na ndio yaliua watu wengi kipindi cha tetemeko.
Mji huu una uwanja wa mpira mzuri tu, pitch nzuri ya kuchezea, Kaitaba lakini majukwaa yake ni ya mbao na ni machache lakini huko Tanzania tunasikia viwanja vikubwa vikijengwa.
Nimeona katika tumetekeleza, Kagera wanaongelea ukarabati wa Ihungo na Nyakato sijui kituo cha afya yaani bila tetemeko hayo yasingefanyika.
Watasema meli, meli CCM hao hao ndo waliiharibu Leo wanajitapa kuirudisha
Yaan katiba ingeruhusu kuuliza maswali wagombea ingekuwa vyema Sana.