Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,357
- 23,760
Ndugu zangu Watanzania,
Tunaweza kuwa tunailaumu CHADEMA kwa mpasuko, Mgawanyiko,mtanziko, mvurugano na mivutano bila kujua kiini chake na kwanini chama kinapitia Mkwamo na hali hiyo .
Ikumbukwe kuwa Ushindi wa Jeshi lolote lile katika uwanja wa vita unaanzia katika Umoja na Nidhamu ya hali ya juu waliyonayo wanajeshi wake pamoja na umoja ulio imara. Hata jeshi liwe kubwa vipi na lenye silaha za kisasa haliwezi kamwe na katu kushinda vita yoyote ile ikiwa jeshi hilo limekosa Nidhamu na umoja ndani yake.Hata Familia imara na yenye mafanikio ni ile iliyo na umoja na Nidhamu ndani yake.
Yenye kujua Baba ni nani na yupi na yupi ni nani na akina nani ni wazazi na yupi ni mkubwa wao hata miongoni kwa watoto. Familia iliyogawanyika na ikakosa Nidhamu haiwezi kusimama wala kupata maendeleo wala mambo kusonga mbele.
Leo ukiangalia ndani ya CHADEMA hakuna umoja wala nidhamu kwa chama na kwa uongozi uliopo madarakani. Ndio sababu unaona mwanachama wa chini asiye na cheo akitoka hadharani akimtupia maneno ya shombo Mwenyekiti wake. Ndio maana unaona mtu akiibuka Bungeni kupitia chama hicho hicho akimtupia dongo mwenyekiti wake aliye mahabusu.
Hii maana yake nini? Maana yake ni kuwa chama kimekosa nidhamu ,adabu na umoja miongoni mwa wanachama wake. Hakuna anayesikilizwa baada ya kuzungumza. Hakuna Sauti inayotambulika kama ndiyo ya mwenyekiti na hii ya katibu na hii ya chama na hii ya vikao rasmi vya chama.
Kila mtu ni Beberu na kambale ndani ya CHADEMA,kila mmoja ni mkubwa ndani ya CHADEMA,kila mmoja ni Dume la mbegu ndani ya CHADEMA. Ni chama ndani ya chama ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kwa ufupi ni kuwa chama kipo katika mkwamo mkubwa sana katika tope zito. Mambo ya kipuuzi yanayofanyika na kutokea CHADEMA huwezi kamwe na katu kuyaona yakitokea wala kufanyika ndani ya CCM.
Huwezi kuleta Fyokofyoko zako ndani ya CCM na ukaachwa salama na uendelee kuwa sehemu yetu. Huwezi ukapinga maamuzi halali ya chama ndani ya CCM yaliyofikiwa katika vikao rasmi. Huwezi ukaleta upumbavu wako na ujinga wako wa kumtolea lugha za matusi , udhalilishaji na kumtweza mwenyekiti wetu. halafu sisi wanachama tukakukalia kimya. Hiyo haiwezekani kamwe na katu.
Na yeyote yule mwenye kutaka hata kuhamia CCM leo hii asije jaribu kamwe kufunua Mdomo wake kufanya kama haya yanayofanyika CHADEMA leo hii. CCM ni chama chenye kuongozwa kwa mujibu wa sheria ,kanuni ,taratibu , miongozo na katiba yetu .ndani ya CCM usilete Mihemuko yako. Kwa hakika hata mimi mwenyewe nitakurarua.
CCM tunarinda chama chetu kwa jasho ,machozi na Damu ya upendo kwa chama chetu. Tunarinda viongozi wetu kwa wivu mkubwa sana. Mwenyekiti wetu ndio Mboni yetu. Ukiigusa hata kwa bahati mbaya tu lazima ujieleze vizuri. Sisi ni jeshi lenye nidhamu na utii na lenye umoja imara sana. Ndio maana tumekuwa washindi katika vita vyote vinavyojitokeza mbele yetu tangu enzi na enzi .na tutaendelea kuwa washindi na kushinda mpaka mwisho wa Dunia kwa kuendelea kusalia madarakani.
Sasa CHADEMA hii ya lissu imepoteza uhalali. Uasi umetawala na kutamalaki ndani ya chama. Hakuna kuaminiana wala kupanga mikakati ya pamoja ya ushindi katika jambo lolote lile. Maana kila mmoja anamshakia mwenzake. Hakuna wazee unaoweza kusema watakituliza chama wakati kama huu wa Dhoruba na sintofahamu.
Hakuna wazee ndani ya CHADEMA wanaoweza kukipa muelekeo wenye matumaini na wakazungumza na kusikilizwa ndani ya chama. Hakuna wazee ndani ya chama wenye uwezo wa kusema maamuzi hayo yatakiangamiza chama na hivyo tusiyachukue au kuendelea nayo au msimamo huu siyo sawa na badala yake tushike msimamo na kufuata njia na muelekeo huu.
Kwa sasa chama hakina wazee wa kukikwamua kwa maneno ya busara na hekima. Maana watu ni kama wamekata kamba za akili na kubakia wakifyatuka tu kimaamuzi. Kila mtu kivyake na kwa staili yake. Huku chama kilichojengwa kwa jasho , Damu na machozi kwa miaka mingi na kujizolea umaarufu na sifa kikiendelea kudhoofika, kugawanyika,kukatisha watu tamaa,kupoteza imani kwa watu na uungwaji mkono na ushawishi kwa watu.
Ni Mwisho wa Enzi wa CHADEMA. Anguko lake limekuja kwa kasi ambayo wengi hawakutarajia. Lakini tuliokuwa mbele ya muda tuliwatahadhalisha sana juu ya kufanya maamuzi kwa Mihemuko na pupa Bila kutazama mbele na athari zake .walioifia CHADEMA itakuwa wanabubujikwa na machozi ya huzuni na mujuto huko waliko lala na kupumzika. Kwa sababu wangejua na kuyaona haya yanayotokea leo ndani ya CHADEMA wangeona ni bora wangekaa majumbani mwao kulea Familia zao tu kuliko kuacha mayatima na wajane wao Bila Faida.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.