Hivi Bunge huwa linatunga au linapitisha tu sheria?!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,165
164,660
Kama wanatunga sheria kwanini huwa "wanaiomba" serikali ilete muswada wa sheria bungeni?Wadau naomba kuelimishwa
 
Kama wanatunga sheria kwanini huwa "wanaiomba" serikali ilete muswada wa sheria bungeni?Wadau naomba kuelimishwa
Bunge letu tukufu chini ya CCM,kazi kubwa ni kupitisha sheria maana hatuhitaji Elimu kubwa maana kazi yetu ni ndiyoooooooooo.
 
Kama mtu wa kawaida (layperson), naamini kibunge kutunga sheria sio lazima ianzie kwao na mara nyingi mswaada huanzia serikalini (wizara inayohusika au sector) na kutua baraza la mawaziri wakishafanya yao ndio hushushwa kwa spika na bunge kufanya kazi yake (kamati inayohusika halafu bunge zima) ambapo wanaweza wakaongeza, kupunguza au kubadilisha. Kwa hiyo bunge hapa linashiriki kwenye kutunga sheria ikipita (sheria imepitishwa) hupelekwa kwa mkulu either akubali au akatae (kutokana na mabadiliko yaliyofanywa na utashi wake). Njia ya pili ni mbunge au kikundi cha wabunge kuja na mswaada wao (wanaita mswaada binafsi), ukabidhiwe bungeni halafu upitie mchakato kama uliyowekwa hapo juu. Serikali nyingi hasa za huku kwetu huwa hazipendi hii kitu na mara nyingi miswaada binafsi hufa kibudu au serikali inasema tuko mbioni kuja na mswaada kuhusu hilo jambo hivyo tuachieni sisi tulete mswaada. Upinzani ndio usahau kabisa kuleta mswaada utafia tumboni. Mswaada haupiti mpaka upate kuungwa mkono na wabunge wengi na pia marekebisho hivyo hivyo. Kwa hali kama hiyo ndo maana wanaiomba serikali ipeleke mswaada (kwani ni rahisi kuungwa mkono -mawaziri na wabunge wa chama chao, wengine baadae).

Kama wanatunga sheria kwanini huwa "wanaiomba" serikali ilete muswada wa sheria bungeni?Wadau naomba kuelimishwa
 
Back
Top Bottom