Hivi BOT wanajua jumla ya pesa zilizo kwenye mzunguko nchini?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Its just curiosity;

Kwamba BOT wanajua kwa sasa kuna jumla ya Shilingi ngapi kwenye mzunguko nchini?

Kama ndio. Wanajuaje? Au wana hesabu tu ya walizoprint.

Tupeni elimu wajuzi.
 
Wakibadilisha fedha huwa wana nakili idadi ya fedha walizochapa na zile walizo pokea wakati wa kubadili. Wanajua kiasi kilichopo kila benki pamoja na akiba waliyonayo huko walipo.

Jibu: Ndio wanafahamu sana zaidi ya unavyodhania.
 
Sio BOT tuuu hata USA na developed countries wanajua ujazo wa pesa yetu katika mzunguko. Na iyo inasaidia kujua uchumi wetu upoje na mzunguko wake
 
economical inajulikana
lakini naamini hawajui wanakuwaga na empty words tu unajua cc, yule, aya mambo c focus yetu kwa sasa, tuko makini,
 
Its just curiosity;

Kwamba BOT wanajua kwa sasa kuna jumla ya Shilingi ngapi kwenye mzunguko nchini?

Kama ndio. Wanajuaje? Au wana hesabu tu ya walizoprint.

Tupeni elimu wajuzi.
Fanya hivi: hela walizoprint A, hela zilizoko BoT na benki za biashara: B, then hela zilizoko kwenye mzunguko ni: A - B = C, kwahiyo wanajua!
 
Hawajui maana kuna wengine wamechimbia hela chini....Ukichimbia hela chini it means kwamba haipo kwenye mzunguko,labda kama inazunguka ardhini.
 
Hawajui maana kuna wengine wamechimbia hela chini....Ukichimbia hela chini it means kwamba haipo kwenye mzunguko,labda kama inazunguka ardhini.
Haha haha haha haha haha haha haha haha
 
wanajua ndio,

hiyo concept inaitwa " Monetary Base".

ili uweze kupambana na inflation pamoja na kusukuma uchumi ukuwe ni muhimu kujua money supply iliyopo. pia hata katika kupambana na counterfeit.
 
Kuna pesa zinaingia nchini bila mifumo ya kibenki mfano biashara za kimataifa na za mipakani, zipo zawadi kutoka walio nje ya nchi wanapotembelea ndugu na marafik n.k.

Hapo inakaaje?
 
Wanajua ila sio rahisi kujua the exactly amount kabisa ... Wanachokifanya wanapiga hesabu ya money supply, money supply ni kiasi cha fedha kilicho kwenye uchumi wa nchi husika ambayo inahusisha kiasi kilichopo kwenye mzunguko jumlisha kilichopo benki za kibiashara..... Wakiitaji kujua the grand amount wanajumlishia reserves (kiasi walichonacho huko bot)
 
Yes, wanajua kila kitu ikiwa tunaprint labda noti za elf 10 za bilion 500, ujue noti nyingine za elf 10 zenye thamani ya 500 bilion zinachomwa moto zineteketea zote, na pia kwenye mzunguko wa pesa saivi kuna kama 60-70 tln pesa ya kitanzania
 
Kuna pesa zinaingia nchini bila mifumo ya kibenki mfano biashara za kimataifa na za mipakani, zipo zawadi kutoka walio nje ya nchi wanapotembelea ndugu na marafik n.k.

Hapo inakaaje?
Izo pesa unazopewa kama sio currency ya tz haituhusu ila ukiichenji kua tzs wanajua... so mambo yapo kiuchumi zaid...
 
Back
Top Bottom