Hivi bongo hatuwezi kuwa na website ya kuuza vitabu soft copy?

Hivi bongo hatuwezi kuwa na website ya kuuza vitabu soft copy?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
21,013
nimeona website kama ya wasafi.com inatumika kununulia mziki online, je hatuwezi kuwa na kitu kama hicho kwa vitabu? nina kakitabu kananisumbua sana kuuza. na pia bongo kuna waandishi wengi sana sema gharama za uchapaji na namna ya kuuza ndiyo tabu.
 
kwa bongo kununua vitu ni shida kubwa sana labda lenga soko la nje tu, mfano kuna watu wana blogs lakini kila siku mtu anaomba msaada wa kupata free templete na anarudi tena kuomba msaada jinsi ya kupata google ads kwa urahisi ili apige pesa.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
nimeona website kama ya wasafi.com inatumika kununulia mziki online, je hatuwezi kuwa na kitu kama hicho kwa vitabu? nina kakitabu kananisumbua sana kuuza. na pia bongo kuna waandishi wengi sana sema gharama za uchapaji na namna ya kuuza ndiyo tabu.

unaweza ku invest huko nafikiri hao jamaa wasafi ulo wataja washaonesha njia kuwa tunaweza kuwa na local stores na tukafanya malipo automated kwa mobile money na tukapata kile tunachokilipia mara moja!
 
mkuu ipo maktaba ya mtandaoni ya kitanzania, niliwahi kuitumia ni nzuri tembelea hii thread

TOVL - Maktaba ya mtandaoni inayohimiza matumizi ya kompyuta kwa watoto

website ya maktaba

Tanzania Online Virtual Library
nimeiona ni nzuri sana kwa wanafunzi. wizara ya elimu wanatakiwa kusupport hii kitu na ile ya mrs Nyalandu. ila kuweka kitabu na kutegemea subscription fees naona ngumu kibiashara. hivi inawezekana kutengeneza kama app ambayo mtu akinunua kitabu kinakuja kama updates ili kupunguza sharing?
 
nimeiona ni nzuri sana kwa wanafunzi. wizara ya elimu wanatakiwa kusupport hii kitu na ile ya mrs Nyalandu. ila kuweka kitabu na kutegemea subscription fees naona ngumu kibiashara. hivi inawezekana kutengeneza kama app ambayo mtu akinunua kitabu kinakuja kama updates ili kupunguza sharing?
ku download watu wanaogopa piracy, njia hii pia unaweza kuiba ila inakuwa ngumu kidogo, hiyo ya kudownload akidownload mmoja mnashare wote.

hio ya MRS Nyalandu ni ipi?
 
unaweza ku invest huko nafikiri hao jamaa wasafi ulo wataja washaonesha njia kuwa tunaweza kuwa na local stores na tukafanya malipo automated kwa mobile money na tukapata kile tunachokilipia mara moja!
ishu hizi zinahitaji mtaji mkubwa na mambo mengi. maana ni kama kuanzisha publishing company. ila tukiunga nguvu watu wengi kazi inaweza fanyika.
 
nafikiri anamikataba na walimu mbalimbali wanaoziandaa maana ni masomo yote, topics zote za form 1-4.
Boss nnatengeneza hizo website pia hata websites za
mashirika,
makampuni,
vyuo,
muziki
Habari n.k

nichek whatsapp tuyajenge 0652105601
 
nimeona Tigo kwa kushirikiana na hawa jamaa wameunda kitabu app. ngoja niwatafute niingize mchuzi.

Tigo, Jackson Group kushirikiana uzinduzi wa Kitabu App
bukuku 1 week ago BIASHARA Leave a comment 93 Views


Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kitabu App ambayo iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania Pembeni yake ni mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa.




Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa akielezea namna ya kupakua KItabu App kwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa Android uzinduzi wa Kitabu App ambayo iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania pembeni yake ni Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael



Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa akielezea namna ya matumizi ya Kitabu App kwa waandishi (Hawapo pichani) mara wakati wa uzinduzi wa Kitabu App ambayo iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania. katikati mtunzi wa hadithi Frank David na pembeni mwishoni ni Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael
Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imeingia ubia na Kampuni ya Jackson Group kuzindua App mpya ya mtandao inayofahamika kama Kitabu App ambayo iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania.
App hiyo inaingia sokoni kama suluhisho sio tu kwa wasomaji bali pia kwa waandishi wa vitabu ambao sasa wanaweza kuuza na kufuatilia na mauzo ya vitabu vyao kupitia simu zao za mkononi, kwa kutumia mtandao wa Tigo 4G LTE ambao ni mkubwa, wa kasi na mpana nchini.
Kujumuisha vitabu kwa njia ya sauti katika jukwaa moja inatarajiwa kuwa App hiyo itabadilisha jinsi ambavyo Watanzania watakavyojijengea mazoea kujisomea, hali ambayo itakuwa ni kinyume na kupungua kwa mazoea hayo ambapo kwa kiwango kikubwa kumekuwa kunahusishwa na kuwepo kwa utamaduni mbovu wa kujisomea miongoni mwa wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa App hiyo Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael alisema, “Kampuni yetu inaendelea kuthibitisha kujikita kwake katika kuwekeza n katika kuboresha utamaduni wa kujisomea nchini Tanzania. Tuna imani kwamba App hii itahamasisha mvuto wa kujisomea miongoni mwa jamii na hivyo kufufua kudorora kwa utamaduni hapa nchini.”
Shisael alisema, “Tayari wateja wetu wengi wanapenda kutumia simu kuchati na marafiki pamoja na wanafamilia,” na kuongeza, “Kupitia Kitabu App tunatoa jukwaa muhimu kwa waandishi, wachoraji na wasomaji kwa ujumla kufikia sehemu rahisi ya kusoma mada mbalimbali kupitia simu ya mkononi.
Akizungumzia kufurahia kwake kushirikiana App hiyo na wateja wa Tigo Shisael alibainisha kwamba hivi sasa wanaweza kuvipata vitabu wavipendavyo wakati wakifanya mambo mengine kwenye simu zao
Akitoa maoni yake kuhusu App hiyo Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa alisema, “ App yetu ya Kitabu App ni ubunifu ulioendeshwa kimkakati ukiwa unahamasishwa na kukua katika kujumuishwa kiteknolojia. Kupitia App hii tunawaruhusu waandishi wa vitabu kufikia kiwango cha hali ya juu cha usoamaji kupitia simu zao za kisasa. Wakati tuna waandeishi wengi wenye vipaji katika aina mbalimbali za vitabu, hali kadhalika kuna uhitaji mkubwa wa uelewa ndani yake.”
Alisema, “Tunaamini kwa kuangalia zaidi katika kukua kwa orodha yetu tunaweza kuleta mabadiliko ndani ya usambazaji kote nchini na kuirudisha tena furaha ya kujisomea kwa Watanznania.”
Twissa aliongeza, “ Kitabu ni App ya kuelimisha, kuburudisha na kuunganisha na mada za kidini. Elimu ni moja ya mitazamo yetu ya msingi, hivyo tunajenga ushirikiano na tunatoa wito kwa taasisi za kielimu kupakua mada zao, kuhifadhi kwa ajili ya kuchapisha na kusambaza vitabu.”


App ya Kitabu App inaweza kupakuliwa bure na kwa hivi sasa inapatikana katika simu za Android ambapo mtumiaji anatakiwa tu kutoa malipo kupitia TigoPesa kwa mada zinazohitajijka na mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom