Hivi bodi ya mikopo kutukata 15% inategemea nini?

Hivi bodi ya mikopo kutukata 15% inategemea nini?

VPN USED2020OCTOBER28

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2011
Posts
1,505
Reaction score
677
1.Unamkata mfanya kazi asilimia 15 ya mshahara wake ilihali kwenye mshahara wake hakuna maboresho yoyote???

2.Kwa makubaliano yapi bodi ya mikopo inamkata asilimia 15 ya mshahara wake?

3.Serikali naona kama haitambui umuhimu kwa wafanyakazi wa umma maana maisha yamepanda mmno na mishahara imedumaa je hapo serikali inategemea nini?

4. Vyama vya wafanyakazi vinakazi gani dhidi ya maslahi ya wafanyakazi? Maana sijaona umuhimu wowote wa @tucta kwa wafanyakazi zaidi kwa viongozi wa tucta kuwa na @vitambi yaani hiki chama kipo kipo tu siajawahi ona wala sikia kikifanya juhudi zozote zile!

5.Hakuna wa kumuamini si wa vyama pinzani wala chama tawala lao ni moja tu yani matumbo yao kwanza mengine baadae!!

6.Mzunguko wa hela umekuwa mgumu sana tena sana!!!! Maisha ya mtaani ni magumu sana na mbaya zaidi wafanyakazi wa umma ndiyo wahanga zaidi maana wao mishahara yao imedumaa wala haipewi lishe bora!!

7. Viongo wa juu wa awamu ya tano wote wana taaluma ya ualimu !! Mbona wamesahau kabisa kuboresha maisha ya mwalimu na wafanyakazi kwa ujumla?

8.Bodi ya mikopo ijue kuwa asilimia 15 ya mshahara kumkata mtumishi ni pigo kubwa kubwa sana maana inamkatisha tamaa mtumishi!!

9.Rais Magufuli tunakuomba uingilie kati swala hili la makato yanayofanywa na bodi ya mikopo maana rais wetu tunajua unajua kabisa hujafanya maboresho ya mishahara kwa wafanyakazi please rais tunakuomba!!
 
Tume huru idaiwe Tanzania mapema kabla ya 2020.
Hili ndo suluhisho hakuna kingine.
Waondolewe kabisa ccm
 
Mtoa mada umeanza vizuri.
Kumbuka huo mkopo unaulipa ili wenzio wapate,hasa wasukuma,wahaya,wachagga,nyakyusa na makabila yote 126 .

Kumbuka kitambi ni juhudi binafsi ya mtu,mbona Manji hana kitambi!

Kumbuka kusoma vizuri disclaimer (maelezo yakiyopo kwenye fomu ya mikopo) na sheria iliyoanzisha HELSB!

Tatizo hizo fedha mnazililia kwakuwa mlizichukua ilhali mna uwezo wa kujisomesha mkifikiri ni ruzuku,wengine walikuwa wakipata ni kushinda Baa ya chuo mpaka ziishe,wengine tena ndio wengi wanapatia mademu wote wakali.

Sasa kwa uliyechukulia demu hela ya BODI mtafute huyo mwanamke mwambie akusaidie kulipA.

Hoja kwamba eti mshahara uongezwe ili wewe ukatwe hiyo 15% ni hoja mfu sana.Ni sawa na serikali isikate tu,maana badala ya kukuongeza mshahara si hiyo hela ingeingizwa BODI?

Mheshimiwa Ndalichako,JPM nawashukuru sana kwa hili la kukata 15% lakini nawalaumu sana ,narudia nawalaumu sana,na sitaacha kulaumu, Wapo wahitimu wengi wa VYUO WAMEJIFICHA MTAANI NA WAPO PRIVATE SECTOR, Tupeni Mfumo Rasmi wa KUWAPENYEZEA Majina yao na namba za simu,kituo cha kazi na aina ya kazi wanazofanya,Tunaomba sana mtusikie.


Form six wanaotarajia kujiunga chuo mwaka huu kama unajijua mZazi wako ana hela/mbumba/mshiko /mtonyo wa kutosha bora akusomeshe tu,itakuja kulipa tena kwa riba.

Mfano ,kwa mwanafunzi aliyesoma chuo ghali kama RUCO/RUCO Ruaha University College kwa sheria ada ilikuwa 1.5 Mil,na wanasoma miaka 4 hapo hujaweka hela ya field,,kama unapata mkopo 100% ukimaliza unadaiwa Mil 20, hapo bado riba,kuna aliyemaliza mwaka 2011 mpaka sasa anadaiwa mil 26!
 
Sehemu fulani wananchi waliulizwa mnataka maji au katiba?!
Wakataka maji, poleni wafanyakazi
 
Back
Top Bottom