Hivi bei ya soda Dar ni shilingi ngapi

Hivi bei ya soda Dar ni shilingi ngapi

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
22,312
Reaction score
55,971
kusema kweli mimi mpaka leo bei ya soda siiijui ukienda madukani ni sh 600,bar 700,800,au 1000,sijawahi kusikia 900 sijui kwa nini wameiruka au ndio kukwepa ile una mia nikupe mia mbili,kwenye mahotel inaanzia 1500 mpaka 10,000,huko sina tatizo tatizo ni bar matokeo yake ukienda bar unaanza kuuliza bei kabla hujahudumiwa
 
fanta ndio nakunywa mpaka leo nanunua 600 hadi buku inategemea na mahali gani upo
 
fanta ndio nakunywa mpaka leo nanunua 600 hadi buku inategemea na mahali gani upo
mi huwa nahisi naibiwa nikiuziwa mia nane kwenye vijibaa vya uchochoroni
 
Kumbe mjini soda bado zipo....?
kwani hujui soda ni aina ya dawa kwa baadhi ya wagonjwa ,dokta huwa anaandika kabisa kuwa huyu apatiwe dawa aina ya sod ndio maana wagonjwa wengi hawapewi bia wanapewa soda
 
Bei ni 600 ila baadhi ya maeneo ni 800, 1000 na hata 2000

si unajua tena biashara huria

ila huku mtaan kwetu tunanunu 600
 
bei halali ni 600 ukiuziwa 1000 mia nne ya baa med.kumbuka kuna baa hapa dar baamed halipwi mshahara
 
Ila kiukweli hata mie hili swali niliwai kumliza bro bei halali ya soda nae hakuwa na jibu sahihi
 
Inategemea na jinsi unavyoonekana mjomba , kama una tumbo kubwa bei inapanda .
 
Kabla hujafungua thread ya kuuliza bei ya bia ngoja nkujibu kabisa, inaanzia, 1500 kule kwa wale jamaa zetu wenye uniform, bar 2300, 2500, 3000,4000,5000,6000 nakuendelea.
 
Bei ya soda ni sh.600/-lakini kama ni bei hiyo nikuuzie kama inavyotoka kiwandani,namaanisha bila kuiweka kwenye friji kuifanya iwe ya baridi.kwa wale wanaojua bei za umeme watakubaliana na mimi!
 
Back
Top Bottom