Hivi ATCL itawahi kuja kuwa na Marubani mahiri kabisa kama hawa wawili?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,887
2,000
Huko nyuma ulikuwa ukijua tu unasafiri na ATCL ( zamani ATC ) kwenda Mikoani au nchi za jirani halafu katika Ndege unayoipanda ama yupo Captain Mapunda au Captain Mazula au wapo Wote wawili ilikuwa ni burudani na uhakika tosha wa safari yako kwani walikuwa na vitu vingi sana vya ziada ambavyo ni nadra mno kuviona kwa Marubani wa sasa waliopo ATCL.

Walikuwa ni Marubani wachangamfu sana na ambao walikuwa siyo tu wanaijua Kazi yao bali walikuwa wanaipenda sana Kazi yao ya Urubani na ndiyo maana haishangazi mpaka hivi leo wanasifika na kukumbukwa mno na Wadau.

ATCL nawapongezeni kwa kuwa na Marubani wenu wa sasa ila nisiwaficheni kwa kuwaambia kuwa sijui ni aina ya Ndege zenu au ni Wao wenyewe labda wanaogopa kuziharibu mwishoni Dereva wa Lori akawasweka Jela / Lupango kwani wanaendesha Ndege hizo kwa mwendo siyo wa Kasi vile halafu muda ambao huwa wanatutangazia kuwa tutafika tuendako huwa hauwi huo na badala yake lazima tu mtachelewa kati ya dakika 15 hadi 30 na hata wakiwachelewesheni hivyo hawawaombi radhi na badala yake mkiwa mnashuka na kukutana pale Mlangoni au chini wanabaki tu kuwatoleeni tabasamu zao za kulazimisha na kuwaulizeni safari ilikuwaje.

Je tatizo ni nini hasa? Mbona akina Captain Mapunda na mwenzake Captain Mazula wao Dar to Kilimanjaro walikuwa wanatumia dakika 55 hadi 60 badala ya dakika zinazotakiwa 75? Hao hao tena Dar to Mwanza walikuwa wanatumia dakika 80 badala ya dakika 90 hadi 105?

Kwa hili ndiyo maana nadiriki kusema kuwa ATCL hata mje na Ndege zenu za kila aina ila jitahidini hawa Marubani wenu waige ule umahiri hasa wa kurusha Ndege wa Marubani wenzao Waandamizi kabisa akina Mzee Mapunda na aliyekuwa Brazameni enzi hizo Uncle Mazula kwani hata uwepo tu wa Marubani ambao wanawahi kuwafikisha Abiria waendako huongeza idadi ya Abiria na kuwapeni Sifa kubwa kitu ambacho ni faida kubwa mno katika biashara yenu hiyo ya Usafiri wa anga ambao ni wa muhimu na tegemezi kwa Watu wanaojielewa.

Nawasilisha.
 

MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,120
2,000
Endelea tu kujijaza mwenyewe katika Frame nikupe kitu murua na mujarab kabisa upumzike vizuri jioni hii.
Acha utoto wako....ninakufahamu kwa kupenda utata na kutishia tishia mikwara watu , sasa basi nakufahamisha kuwa jaribu huo ujinga wako.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,887
2,000
Acha utoto wako....ninakufahamu kwa kupenda utata na kutishia tishia mikwara watu , sasa basi nakufahamisha kuwa jaribu huo ujinga wako.
Kawatishe MAPOPOMA wenzako na siyo Mimi. Nilitaka tu urudi tena na Kashfa zako kama ile ya mwanzo ili nikunyooshe vizuri tuheshimiane ila bahati nzuri umejishtukia. Halafu nakutamani siku nyingi mno ila hujai vizuri katika Frame yangu ili nikuwashe vilivyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom