Leo asubuhi nimeona msafara wa magari manne yaliyojaa askari na gari la maji ya kuwasha yakielekea njia ya Chalinze-Segera nilipofuatilia nimegundua ni askari wa Ukonga na wengine wa Pwani na wanaelekea huko Arumeru kwa ajili ya ulinzi.
Ndo nauliza inamaana hao askari wa Arusha Moshi hawawezi kuimarisha ulinzi hapo Arumeru?
kazi ipo huko!!
Je wakati wa uchaguzi mkuu watafanyaje maana kila jimbo litahitaji askari wa kutosha pamoja na gari la maji ya kuwasha! watakodi toka nchi jirani?
matumizi mabaya ya fedha za umma wakati askari haohao hawajalipwa malimikizo ya stahiki zao