Hivi 2020 kuna Mtanzania ataichagua CCM?

Hivi 2020 kuna Mtanzania ataichagua CCM?

Tokea uchaguzi wa mwaka 1995, WATANZANIA walianza kutoichagua CCM.

Lakini tume ya uchaguzi Tanzania sio huru.

Kuna namna wanachezesha matokeo, aliyechaguliwa anakuwa siye, na asiyechaguliwa anakuwa ndiye!

Hasa kwenye ngazi ya Urais.
 
Kwa aina ya uongozi tulio nao sasa hivi, uongozi usiojali wananchi wake hata pale wanapopata majanga, uongozi usiowajali watumishi wake, uongozi usiowajali wananchi maskini, uongozi usiowajali wanyonge, uongozi usiowajali watoto wa maskini hadi kuwanyima mikopo, kuzuia ajira.

Uongozi uliojaa ghiliba, chuki, visasi vya kila aina, ni uongozi ambao wao ni bora kununua ndege kuliko kununua madawa mahospitalini, uongozi usiopenda kukosolewa hata kama wamekosea lakini ni uongozi unaopenda sifa binafsi kuliko utendaji kazi.

Hivi kuna Mtanzania atapanga foleni tena 2020 kuwachagua watu hawa.
HASHIMU RUNGWE......QUOTES: Sasa ndo nchi imepinda sio awali
 
Tunajivunia tu kete ya tume ya uchaguzi!! Kwa mtaji huo CCM itachaguliwa tena!!
 
Mimi nipo nitaichagua. Mimi na wanaukoo wangu wote, marafiki zangu na michepuko yangu yote tutaichagua ccm rais na baadhi ya wabunge na madiwani.
 
kama kura zitapigiwa jf basi watanzania hawatoichagua lakini kama sivyo basi utajionea mwenyewe kwenye sanduku la kura
2005; 80%
2010; 62%
2015; 58%
2020; ??%
??% = what? Jaza mwenyewe. Na hiyo hesabu hapo juu ni pamoja na wizi wa kura, matumizi ya vyombo vya dola, udhibiti wa media na uchafu wote. Lakini graph ilikuwa inachuka kwa kasi sana.
Sasa hiyo ??% toa za ulaji wa rambi rambi, lugha ya matusi kwa wapiga kura, uchumi mbovu, vijana kushindwa kusoma kwa kukosa msaada wa mikopo, njaa na kunyimwa chakula kwa vile ukame haukuletwa na ccm na mazagazaga mengine.
Hakika hiyo ??% yaweza kuwa 35%. Na kama wizi ukidhibitiwa ni 29%. Tume huru ya uchaguzi ikifanikiwa kuwepo hapo ndio funga kazi maana hiyo ??% itakuwa 11.7% sawa na kura za Lipumba kipenzi chenu.
 
Kwa aina ya uongozi tulio nao sasa hivi, uongozi usiojali wananchi wake hata pale wanapopata majanga, uongozi usiowajali watumishi wake, uongozi usiowajali wananchi maskini, uongozi usiowajali wanyonge, uongozi usiowajali watoto wa maskini hadi kuwanyima mikopo, kuzuia ajira.

Uongozi uliojaa ghiliba, chuki, visasi vya kila aina, ni uongozi ambao wao ni bora kununua ndege kuliko kununua madawa mahospitalini, uongozi usiopenda kukosolewa hata kama wamekosea lakini ni uongozi unaopenda sifa binafsi kuliko utendaji kazi.

Hivi kuna Mtanzania atapanga foleni tena 2020 kuwachagua watu hawa.
Wananchi ni nyie tu wahaya? Mbona wasukuma Kahama hawajalalamika? Mbona Morogoro miaka michache walipata majanga makubwa hawakulalamika? Acheni hizo. Wote wana haki sawa ikiwa ni pamoja na mmoja mmoja ambao nyumba zao huezuliwa na upepo. Kama ni kujengewa wote tangu enzi wangejengewa
 
Sisiem haina mpinzani hapa tz, wengine wote ni wapiga dili wako kibiashara hawana nia ya dhati kabisa, mtu hana mbinu mbadala yaani sera yake kuu ni kupinga, mwingine uyu ndio usiseme leo kajiuzulu kesho karudi yaani ni mchanganyo tu uyu nae kamezwa hana sauti kafanywa mtaji sasa kwanini asishinde 2020
Kinachofanya waonekane hawana mpinzani ni uelewa na utashi mdogo wa watanzania katika kufanya maamuzi ...

Wakionhozwa na wewe mwenyewe KAJOLIJO.
 
Nina wasiwasi sana na Kura za wafanyakazi na familia zao!
 
Mkuu wakishapewa kanga na buku saba kama lumumba, vidole wanaweka juu
 
watu hawawezi kuacha kuichagua ccm kwa sababu ya post yako hii ya kijinga! wataacha kuichagua ccm endapo tu utatokea upinzani wenye nia ya dhati ya kuondoa umaskini wa watanzania, Leo hii upinzani una wagombea ambao walikuwamo ccm miaka zaidi ya 30 na hakuna jipya!
 
Magufuli ntamchagua mpaka atakapokufa. Mpaka sasa sioni kosa lake hata moja!
 
Back
Top Bottom