HIV - AIDS tishio kwa sasa

Anakosa kufa kwa ukimwi, anabutuliwa na bodaboda, hachukui Muda anakata moto........ Hivi vitu tunavichukulia serious sana ila aaaaaah..... Kufa kupo tu, sasa shida ni utakufaje basi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama unajuwa kifo kipo hakikwepeki kwanini usifanye maamuzi mazuri hata kesho ya kuwahi peponi mapema! Kalaze shingo yako kwenye reli pindi utakapo ona treni ikija.kwisha habari!
 
Maambukizi yalikua miaka ya 85 mpaka 90. Ndani ya miezi kadhaa tu unakonda kama kama, unaharisha kamba bomba na nywele zinakua kama manyoya ya panya halafu nyekundu. Nyie vijana ukimwi mmeusikia tu. Enzi hizo pale posta, bima na nssf kulikua na mabinti wengi sana. Lkn haikuchukua raundi.
 
Sasa tutafyatua vipi watoto Kama tutatumia kondomu?, tunatekeleza agizo la CCM
Ukibaki mwaminifu na mwenzio akiwa mwaminifu hakuna ubaya kufunya tendo la ndoa kiasili bila kuvaa mifuko ya plastic.
Kama hautaki mtoto tumieni njia za uzazi wa mpango za asili au za kisasa ambazo hurusu tendo bila mifuko ya plastic.
 
Nikiwa Hospital ya ST Elizabeth (Kwa Padre Babu) Ngarenaro, niipita sehemu nikakuta watoto wamejipanga kwenye benchi nyuma ya jengo la mapokezi. Hakika niliingia Hospital hapo kwa lengo la kukojoa tuu kwenye vyoo vya hospital maana nilibanwa sana.

nilikaa na wale watoto (kama miaka 16 kushuka chini walikuwa kama 20 hivi) kwenye benchi na mara alikuja kijana na kuwauliza "Mnaendeleaje toka mwezi uliopia? Kuna mtu ameumwa au kupata shida yeyote?" walimjibu wako poa.. ikabidi niangalie vizuri kwa kusoma matangazo mbali mbali ubaoni. Kuna wanawake kadhaa walikuwa kwenye foleni ya kuelekea chumba fulani hv. kumbe ni mambo ya CTC bhana dah! Nilihudhunika sana. watoto wale pamoja na afya njema walizonazo lakini ndo hivyo tena.

Vijana wenzangu tulinde afya zetu. Tumuombe Mungu atuepushe na Janga la HIV. Machozi yalishukia tuu tumboni. Imagine unajua una mtoto wenye HIV...... Dah i cant handle the pain.

Vijana wenzangu PIMENI MJUE Afya zenu ili hata mkiamua kuwa na watoto kuwe na tahadhari kubwa wasizaliwe nao.


Mtakatifu Anthony Wa Padua Utuombee
Mtakatifu Aloyce Gonzaga Utuombee.
Bikira Maria Malkia wa Mitume Utuombee
Watakatifu wote wa Mungu Mtuombee

Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na la Roho Mtakatifu. Amina.
 
Back
Top Bottom