HITS Telecom (T) inamilikiwa na Mwinyi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HITS Telecom (T) inamilikiwa na Mwinyi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MtazamoWangu, Jul 15, 2009.

 1. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kampuni ya Hits ( ExcellentCOm T Ltd) ambayo imekwama sasa kutokana na kukosa pesa na kukimbiwa na wafanyakazi wake wote wa ngazi za juu, inawezekana ikamtia doa Dr. Mwinyi kwa ushiriki wake kama local director.
  Hits Iliyosajiriwa kama ExcellentCom (T) Ltd inamilikiwa na kampuni mbili;

  1. Excellent Systems 65% (wamiliki ni Yahya alwahi na ndugu yake Nasor Alwahi) ni Watanzania (kutoka singida) wenye uraiya wa Oman, wafanyabiashara.
  2. Jitco 35%- Inayomilikiwa na Dr.Hussein Mwinyi na nduguye Abdulah Mwinyi,

  Hawa walipewa nafasi hii kutokana na sheria za TCRA kutaka 35% ya kampuni kumilikiwa na mtanzania na kutokana na urafiki wao na waomani, japo waliweza kumshawishi Mramba na Chenge kuwasaidia wakati wanatafuta leseni, Mramba aliomba ajengewe shule jimboni na pia angeshirikishwa kwenye mradi wa kiwanda cha mbolea walichokuwa wamepanga kujenga kusini.

  Mramba alialikwa Oman kuhudhuria vikao vya kiserikali na ma-investor hao ambao pia walikuwa rafiki zake japo aliambulia kupigwa SOUND.....hamna kitu...

  Baada tu ya ExcellentCom kupewa leseni, waomani walitafuta investor mwenye uwezo kifedha na uzoefu katika biashara ya simu, ndio Hits Telecoms walipoingia, wakuza nusu ya shea zao, kwa hiyo kampuni ikawa:

  1. Excelent Systems 32.5%
  2. JITCO 35%
  3. Hits Telcoms 32.5%

  Na kufanya JITCO kuwa ndio majority shareholder, japo Hits alitakiwa ndio awe investor...

  Abdulah Mwinyi ndio mwenyekiti wa bodi kwa sasa na ndio ameonekana mara kwa mara akifika ofisini kuwatuliza mzuka wafanyakazi na kujua hatika ya mishahara yao ambayo sasa imeonekana kuwa mgogoro.

  Japo hatuwezi kuwalaumu akina Mwinyi kwa ushiriki wao na pia kuilaumu kampuni, maana waliamnza vizuri sana kwa kasi mpaka pale uchumi ulipoyumba...ila tu wajue pia walitumiwa na wale waOmani ambao walikuwa opportunist tu, wababaishaji mno, kila aliyekumbana nao anawalaumu sana kwa sound, na hata ushiriki wa akina mwinyi ulikuwa na mashaka in terms of investment (hapa siweki wazi).

  Kwa wale waOman walisharudisha gharama yao mara tu baada ya kuuza 32.5% ya kampuni na hawana hasara kabisa..kwani hata kile kikampuni kidogo cha ndege kwenda znz wamekinunua...wanaendelea kufanya hivyohivyo pia baadhi ya nchi kama Uganda, mozambique...lakini kutokana na uchumi kubana naona spidi yao imeisha....

  Kama Hits haitauzwa au kupata pesa kwa njia yoyote ile, itakuwa ni aibu kwa kina Mwinyi...na TCRA itabidi ichukue hatua...
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa wameshaanza kufanya kazi au vipi??
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Sioni tatizo, hizo ni reality za biashara hauwezi kutabiri kila kitu, kuna wakati mambo yatakukumba by surprise kama hii recession.
   
 4. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeah,

  Kampuni inaweza ikafirisika kabla haijaanza. Biashara ya telecoms ni biashara kubwa inayohitaji mtaji mkubwa. Hakuna nafasi ya ubabaishaji. Hivi vikampuni vinavyoanzishwa leo na kesho vingi vitakufa mapema tu. Soko la Tanzania sasa hivi limeshajaa. Kwa biashara ya simu za mikononi kuwa sustainable kampuni inatakiwa angalau ifikishe wateja laki tano.

  Ingawa market surveys zinaonesha kuwa bado kuna wateja wengi wa kutosha, ushindani unafanya iwe vigumu kwa kampuni moja kujichotea wateja hao kwa muda mfupi. Kwa kifupi, mafanikio ya Vodacom, Zantel, Tigo na Zain hakuna kampuni itaweza kuyaiga tena kwa hali ya sasa hivi.

  Hits Watahitaji kuuza frequency spectrum zao kwa kampuni nyingine. Kwa hali ya soko la Tanzania sasa hivi si rahisi kwa investor yeyote kumwaga pesa kwa ajili ya kuanzisha kampuni mpya. Kwa hiyo uwezekano mkubwa ni kuuza spectrum zao kwa makampuni yaliyopo tayari kwa ajili ya kupanua mitandao yao.

  Yeah, hata GTV waliliwa na recession hii.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sio mbaya kwani ili kufanya biashara lazima utegemee mambo mawili kushinda au kushindwa.

  lakin yoooote ndio uanamume
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Line yangu ya voda jamaa walikuwa wana bipu tuu
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  aibu ya nini sasa? kaa kafanya biashara imekufa, mbona inawatokea watanzania weengi tu?
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Hizo ni ups and downs za kibiashara and its normal, hakuna aibu yoyote
  kwa Mh.Mwinyi.
  Kama kampuni ingekuwa hewani halafu wajeshi wakatumia kampuni hiyo kama kampuni rasmi ya simu za wajeshi, hapa ndio ingekuwa issue. Kufilisika sio issue.
  Hizi kampuni za simu zilizopo ni kweli zimejiimarisha sana, ila soko bado ni kubwa na liko wazi sana, ikitokea kampuni yenye deal bomba zaidi, wataja itawahamisha.
  Makampuni ya wenzetu wanatoa handset bure, na very low rate mpaka bure kwenye mtandao wao. Wanakapitalize kwenye units of sales na volume ya interconectivity na mitandao mingine huku wateja wake wakijifaidia free airtime ya mtandao wao. Soko lipo tatizo ni strategies.
   
 9. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #9
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nawapa pole sana walioacha kazi zao sehemu zingine na kwenda kuajiriwa na HITS..daa..
   
 10. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kibiashara sion tatizo at all, and due to recesion it is explainable, the isue ni kwamba ile kampuni isipopata muafaka mapema itasababisha matatizo makubwa na huenda ikamtia doa mh, Mwinyi;
  1. kabla hata kampuni haizaanza kazi ishaajiri watu zaidi ya 140, wote hawa lazima walipwe mishahara yao
  2. Hits walikuwa na malengo makubwa, wamerent jengo kubwa sana na linalipiwa kiasi kikubwa cha fedha kila mwezi na pale ndani wameweka mitambo ambayo hawawezi ku-abandon
  3. Hits walishajengga minara mingi dar na mikoani na kila site inalipiwa kodi kila mwezi
  4. Hits wamekopa mitambo ya simu yenye zaidi ya thamani ya $100M kutoka kwa supplier,
  5.Hits inatakiwa ilipie masafa (frequencies) kwa TCRA zaidi ya $700K kila mwaka whether on or off air.
  6. hits imesaign roaming agreement na Zain kwa nchi nzima, na mpaka sasa Hits inapatikana kwa wafanyakazi wao tu...

  sasa yote haya ni mzigo ambao wale investor washaanza kususia kutoa pesa na Abdulah Mwinyi amekuwa anafanya kazi ya ziada kuwapooza wafanyakazi....
   
 11. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hits iko hewani kwa wafanyakazi wake tu, lakini haijaanza kufanya biashara....imekwama
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kaaaaaazi kweli kweli. Mitandao mingi, tarrif kibao!!! Sasatel nao vipi???
   
 13. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ni kweli biashara za simu zinataka heavy investments na return yake ni ya muda lakini pia in profit sana ukisha break even...
  ndio maana hata mh, Mengi aliahirisha kufungua kampuni ya simu japo alishaomba leseni...na yeye akiwa mjumbe wa NICO aliishawishi board wasiInvest kwenye Dovetel (sasatel) baada ya sasatel kuwa wanatafuta investors kabla hawajapa hawa waNorways na Mama Rwakatare kuchomoa kuweka pesa kuhofia return...initial mama Rwakatare ndio ilikuwa awe main investor in Sasatel...

  Na labda ndio maana hata Yusuph Manji mpaka leo analeseni (kampuni inaitwa Mycell) hajaweza kufungua biashara..naye anatafuta investor...wachina walitaka kumfadhili wakamshtukia baada ya kukataa hesabu zake ziwe audited na international firm and afanyiwe due dilligence....

  bado kuna list ndefu ya kampuni mpya zinazotaka kuingia Tanzania na mwisho wa mwezi huu huenda TCRA wakatoa leseni mpya....kwa mfanyabiashara, bado soko lipo kwakuwa katika population ya 40M kuna about 13M users japo wanasema 15M users, na soko kubwa lipo mijini tu....
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hapana shaka wewe ni mmoja wa hao wafanyakazi 140... Pole kwa matatizo yaliyowakuta
   
 15. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hapana mkuu just feel sorry for them maana wengi walitoka kwenye makampuni makubwa sana...tigo, vodacom, ttcl, banks.....tatizo ni kwamba hata wale waliokuwa wamewaajiri wamekimbia....
   
 16. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  jamani ni balaa sana wenzetu walioacha kazi zao nawaonea huruma sana sana...sijui wataanzia wapi tena
   
 17. K

  Kilambi Member

  #17
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kipimo cha ukubwa/kukomaa ni jinsi ya kupambana na hali hiyo, wale sio watoto na naamini walifanya maamuzi sahihi tu kujiunga na kampuni hii japokuwa mambo hayakwenda kama walivyotarajia. nasikia waliaajiri watu waliokuwa "vizuri" hivyo sidhani kama itakuwa ngumu kiasi hicho kupata ajira/muafaka
   
 18. BabaBabuu

  BabaBabuu Member

  #18
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mkuu kwani hiyo kampuni imeshakufa rasmi? kama bado ni lazima watakua wanajua wapi pa kuanzia
   
 19. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  rafiki yangu alikuwepo hits sasa ametoka ameenda sasatel!!! mambo magumu
   
 20. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  jamani tukiacha vibarua tuache kwa amani wala tusiache kama tumegombana maana kuna leo na kesho ni ushauri wangu tu...
   
Loading...