Hitilafu ya Umeme, Agosti 01, 2019: Waziri wa Nishati amshusha cheo msimamizi umeme Mitambo ya Kinyerezi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kalemani amemshusha cheo msimamizi wa nguzo kubwa za umeme katika mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi kutokana na kutoridhishwa na taarifa ya hitilafu ya umeme iliyotokea asubuhi ya Agosti moja na kusababisha taaruki kwa wananchi.

Akizungumza baada ya kutembelea nguzo hizo zilizo umbali wa Kilomita moja kutoka kituo cha Kufua Umeme cha Kinyerezi, Dkt. Kalemani amesema serikali haiko tayari kufanyakazi na watendaji wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

Akielezea tatizo liliotokea Mhandisi Msimamizi aliyoteuliwa na Dkt. Kalemani kushika nafasi hiyo, ameahidi kutafuta umbuzi wa hitilafu ya umeme haraka iwezekanavyo.

Aidha Dkt. Kalemani ametembelea kituo cha Shirika la Umeme Tanzania Ubungo ambapo ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo kuwasilisha taarifa ya maelezo ya kuungua kwa moja ya mitambo katika kituo hicho pamoja na kuunda timu maalumu kufuatilia tatizo la kuungua mara kwa mara kwa baadhi ya mitambi ili serikali ichukue hatua.
 
wanatutia hasara mno wananchi.
Huo mtambo ulioungua huenda ndio wa huku Ubungo hadi Kimara maana kwa miezi miwili umeme ni kukatikakatika tu,juzi niliwauliza wanasema kuna hitilafu Ubungo.Hizi hitilafu gani haziishi?Hawawezi kuforesee mambo wakaishauti serikali kuwekeza mapema?mtambo unaungua,unarekebishwa,unatumika huo huo,kila muda unazimika tena,tunaopata shida ni sisi end user.Hopeless kabisa.
 
Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kalemani amemshusha cheo msimamizi wa nguzo kubwa za umeme katika mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi kutokana na kutoridhishwa na taarifa ya hitilafu ya umeme iliyotokea asubuhi ya Agosti moja na kusababisha taaruki kwa wananchi.

Akizungumza baada ya kutembelea nguzo hizo zilizo umbali wa Kilomita moja kutoka kituo cha Kufua Umeme cha Kinyerezi, Dkt. Kalemani amesema serikali haiko tayari kufanyakazi na watendaji wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

Akielezea tatizo liliotokea Mhandisi Msimamizi aliyoteuliwa na Dkt. Kalemani kushika nafasi hiyo, ameahidi kutafuta umbuzi wa hitilafu ya umeme haraka iwezekanavyo.

Aidha Dkt. Kalemani ametembelea kituo cha Shirika la Umeme Tanzania Ubungo ambapo ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo kuwasilisha taarifa ya maelezo ya kuungua kwa moja ya mitambo katika kituo hicho pamoja na kuunda timu maalumu kufuatilia tatizo la kuungua mara kwa mara kwa baadhi ya mitambi ili serikali ichukue hatua.
Technical issues si sawa na kusaini cheki ufisini ofisini au nje ya ofisi
 
Back
Top Bottom