Hitaji kubwa la mwanaume ndoani ni kuheshimiwa hata pale anapokuwa amekosea

Ni rahisi kumuheshimu mwanaume anaekupenda

Mapenzi yakikosekana ni ngumu sana
Sana..


Kwa mfano:Mtu kakusaliti,ama kauli ngumu sana
Yataka moyo mtu aone unajishusha mana kujishusha nacho kipaji
 
Ili mahusiano yadumu ujue kuna mjinga mmoja. Hamuwezi kuwa wajanja wote then mkatoboa. Mashindano ni sumu ya mahusiano, ile "kama hafanyi B nami sifanyi C" kama nafasi inaruhusu we fanya hiyo B na C uone.
Kuwa mjinga mda mrefu napo mtihani
Inabd mbadilishane tu hahaha
 
Ujumbe mzuri kwa wanawake wenzako lakini na mimi ngoja nichangie kitu, muwe munatoa huduma ya ndoa basi mana kumekuwa na malalamiko kwa wanandoa wa kike kuwanyima penzi waume zao
Malalamiko ya kukosekana nguvu za kiume nayo yameshika kasi sana sikuhiz😱
 
Ila bro mimi naona hata sisi wanaume pia tuna matatizo haiwezekani mtu siyo mume mwema ila anataka mke mwema tukumbuke kuwa mtu hupewa wa kufanana naye na mimi naungana nao wanaosema kuwa mwanaume anayestahili kupewa heshima ni yule anayetimiza majukumu yake maana imeandikwa mwanaume mpende mkeo na mwanamke mtii mumeo sasa mwanaume haumpendi mkeo unamsaliti kutwa michepuko halafu unataka yeye akutii eti afuate maandiko tujue tu haya maandiko hayakuandikwa kwa ajili ya wanawake pekee ni kwa ajili ya wote kwahiyo mwanaume asiyempenda mkewe na asiyetimiza majukumu yake kwa mkewe anataka hadi mke amsaidie huyo hastahili kuheshimiwa wala kupewa utii
Thank you end of discussion
 
Baki hivyo hivyo na kibri chako. Ndoa ni agizo la Mungu na ni muunganiko wa Kimungu ambao bila kupepesa macho hauelezi suala la KUOWANA. Mwanamke unaolewa. Suala la kuowana ni dhana inayojengeka sana vichwani mwa dada wetu wa dot com na ndio sababu ya wengi kukosa ndoa, kutodumu kwa ndoa zenu na kubaki single maza.

Huu ni ukweli mchungu msiopenda kuusikia mmebaki kutaka kusikia yale yanayowapendeza tu. Kwamba unaowana? Bullshit, unaowana na nani?
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Sawa naomba nikuulize tena swali jingine ndoa ni kuvumiliana na kusameheana sasa wewe kama mwanaume utakuwa tayari kumvumilia mkeo kwa kiasi kama ambacho wewe utataka yeye akuvumilie? Naomba unieleweshe mkuu
Mkuu una point hatari
Best comments of the thread
Ndoa is two way
Heshima inaendana na mapenzi
Maadamu wote ni watu mnajielewa
 
Ndugu yangu labda nikueleweshe kitu kimoja hivi ushawahi kujiuliza kwanini Mungu alisema mwanamke amtii na amuheshimu mwanaume? Ulidhani kwamba anatakiwa afanye hivyo bure bure tu wakati hujamuumba wala hujamzaa?

Mungu aliweka hivyo sababu alimuumba mwanaume kuwa ndo mwenye jukumu ya kuhudumia na kutunza familia kiuchumi na ndo maana akamwambia mwanaume atakula kwa jasho lake tu na siyo kwa njia nyingine yoyote lakini mwanamke hakuambiwa kuwa atakula kwa jasho lake yeye aliambiwa tu atazaa kwa uchungu

Sasa shida inakuja dunia ya leo wanaume tunataka wanawake watusaidie kutafuta hela na kuhudumia familia wakati tunajua majukumu yao ni kupika kufua kuosha vyombo kufanya usafi kuzaa na kulea majukumu ambayo wanaume hatuyafanyi ila sisi tunataka wao wafanye ya kwetu

Sasa mwanamke ukishamwambia aingilie majukumu ya mwanaume automatically lazima ataingilia na ile nafasi ya uongozi aliyopewa mwanaume yaani hiyo ni nature sababu kuwa kiongozi siyo kwa sababu eti wewe una jinsia ya kiume tu hapana na pamoja na kutimiza majukumu yako yote kama mwanaume sasa ukitegemea mke akusaidie unatagemea nini? Ina maana ni lazima na wewe uwe tayari kumsaidia majukumu yake ya ndani pia
Ukweli mchungu
Dunia imebadilika sn
Ht km mwanamke unataka kujishusha mwanaume pia anakua kama nae haelewii
 
Jukumu la kwanza ni kuwa na akili ya kufanya maamuzi sahihi kwa wakati husika

Jukumu la pili ni kutambua kwamba wewe ni mwanaume na mwanamke anakutegemea kwa kila hila hitaji, KILA HITAJI, kimwili na kihisia

Jukumu la tatu ni kumpenda kweli mwanamke wako ambaye naye anaonesha kukupenda kwa dhati

Jukumu la nne ni kutafuta suluhu ya mambo yaliyoshindikana
E bwana eee!!! Mahitaji ya kihisia ndo yapi hayo
 
maneno hayo!

c.c Honey Money Penny
Mume wake akichepuka Miaka 3 anamkanya anamwombea anamsihi amemstahi haya alioandika huyu bibie ataendelea kuyatenda?

Kama hatoyatenda Kwa sababu ya ubinaadam naomba kurudi kuandika Hadithi za money penny

Hiki alichoandika NI theory aingie kwanza Kwenye ndoa akae Miaka 5 mpaka 8 tuone Kama hajakata kamba
 
Back
Top Bottom