Hitaji kubwa la mwanaume ndoani ni kuheshimiwa hata pale anapokuwa amekosea

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
Wanawake wenzangu, kila siku napenda kuwaweka wazi mambo muhimu sana katika mahusiano na ndoa zetu.

Leo nataka nikukumbushe tena jambo hili. Kama unaona ndoa au mapenzi yako yanayumba yumba lakini mwanzoni yalikuwa na furaha na uliyafurahia, basi inawezekana kabisa kuna mahali uliyumba ama ulianguka hasa katika kipengele cha kumheshimu mumeo.

Nisikilize my dia, hitaji kubwa la mwanaume katika ndoa yake ni kuheshimiwa zaidi na mkewe. Tunapozungumzia heshima kwa mwanaume, katika mazingira yetu, tunamaanisha hali ya kutamani kujiona yu na hadhi ya juu, yu na mamlaka zaidi pengine kuliko mwanamke.

Kinyume chake ni kudharauliwa, kuwekwa katika mazingira ya kujiona hana hadhi, hana mamlaka, asiye na kauli wala uwezo kufanya lolote bila mwongozo wa mwanamke.

Kwa wanaume wengi, heshima ni namna unavyoongea nae, maneno unayoyatumia katika kueleza mawazo yako, ishara za mwili wako katika mazungumzo, kumpa nafasi ya kwanza katika maamuzi na mambo kama hayo.

Heshima, vile vile, ni kumstahi mwanaume unayempenda hata anapokosea. Kosa linapotumika kama sababu ya kufanya vitendo vinavyodhalilisha hadhi yake ni kujipunguzia alama. Ndio kusema, staha ni kuong
ea naye kwa nidhamu hata katika mazingira ambayo ni dhahiri yeye ndiye mkosaji.

Kadhalika, heshima ni kuwa tayari kumtunzia hadhi yake kwa watu wengine. Kumjengea taswira inayomwongezea thamani yake kwa watu unaojua anawaheshimu. Kuonesha fahari yako kwake unapoongea na watu wengine kwa kauli, matendo na hisia kunaongeza alama za sifa anazozihitaji kwa mwenza wake.

MWANAMKE LIELEWE HILI NA UJITATHMINI
 
Tatizo tunatofautiana kwenye definition ya neno majukumu
Majukumu unayoyajua wewe ni yapi????

Mwanamke wako inabidi apendeze utajua wewe anapendezaje......inabidi ale ashibe....akiumwa aende hospital basi hayo mengine majaaliwa
.....

Hayo niliyoyataja ni yangu lakini ninayoona ya msingi nilisahau sehemu ya kulala
 
Sitamuheshimu mwanaume asiyejua heshima yangu, kikubwa hapo tuheshimiane, tuthaminiane, tupendane, na kujaliana kwa sababu siku hizi tunaoana.
 
Majukumu unayoyajua wewe ni yapi????

Mwanamke wako inabidi apendeze utajua wewe anapendezaje......inabidi ale ashibe....akiumwa aende hospital basi hayo mengine majaaliwa
.....

Hayo niliyoyataja ni yangu lakini ninayoona ya msingi nilisahau sehemu ya kulala
Ni kama unayoyajua wewe lakini bado tutatofautiana definition ya baadhi ya mambo.

Nakubali mwanamke wako anatakiwa apendeze lakini je kupendeza ni vipi na apendeze kwa mujibu wa nani?? Anampendezea nani?? Mimi kwangu kupendeza ni kutokuweka minywele bandia na mikope ya ajabu. Kwangu kupendeza ni kutojitia mi-lipsticks na mikorogo.

Hayo mengine tutakubaliana. Akiumwa ni jukumu langu na kula ni juu yangu. Makazi yake ni jukumu langu pia
 
Yes naungana na wewe hata Mimi kupendeza kwangu sio kuweka mavitu bandia ...hata zile hijabu zinatakiwa kua nzuri angalau na nguo nzuri na apendeze kwa ajili yako sio kwa ajili ya wengine
 
Back
Top Bottom