Historia ya Vimbweta

Historia ya Vimbweta

Alicho kifanya ni copy maana ata vyuo vya nje ya nchi ivyo vibweta vipo na vilikuwepo kabla ya ivyo.
Mkuu, no matter what, we just consider the one who has introduced it in our country.

By the way, unaweza kunambia Kingereza cha Kimbwete?
 
Kila la kheri Mkuu. Piga kitabu. Ujichukulie watoto warembo pia... Hahah!


Hahahaa haswaa Mkuu. Watoto warembo tumeumbiwa.

Nitakomaa na kitabu Mkuu, vimbwete vitasimlia aisee.

-Kaveli-
 
Salaam WanaJukwaa.

Kama wewe ni Mwanafunzi au umepata nafasi ya Kuingia Chuo, bila shaka msamiati wa neno "Kimbwete au Vimbwete" haukupigi Chenga.
Naam, usishangae sana na kudhani nimekosea kuandika. Wengi wamebadilisha jina halisi na kulipachika jina jipya la Kimbweta au Vimbweta. Je, umewahi kujiuliza asili ya jina lenyewe na maana yake? Basi twende pamoja ukapate kulifahamu vema.

Miaka ya Nyuma huko, kulikua na wizi, upotevu na uhamishaji wa viti katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Viti vingi vilikua vinahamishwa katika eneo ambalo vilipaswa viwepo wakati mwingine hata kuibiwa na kuleta Usumbufu wa hali ya juu.

Baada ya kuwa ni jambo lenye Usumbufu mno chuoni hapo, Uongozi wa Chuo ulifanya namna mbalimbali katika kutatua tatizo lenyewe. Tatizo lilikuwa kubwa hasa kiasi cha kufikirisha vichwa vya Wahadhiri na Wanafunzi kwa ujumla.
Katika utoaji wa Mapendekezo, aliyekuwa Mhadhiri Chuoni hapo Prof Tolly Mbwete alitoa pendekezo kuwa yajengwe madawati ya saruji yaani Cement. Wazo au pendekezo lake hilo lilifanyiwa kazi na lilizaa mafanikio makubwa. Lilitoa ufumbuzi wa tatizo husika.


Wazo hilo la Prof Mbwete,lilipunguza kwa kiasi kikubwa kama siyo kumaliza kabisa tatizo husika. Alipongezwa sana kwa wazo hilo na alipandishwa ngazi kutoka Lecturer mpaka Senior Lecturer.

Hiyo ni moja kati ya kazi ya Kitaaluma ya Prof Mbwete. Baadae, alisema hayo madawati yaliyojengwa kwa Saruji, ikiwa kimoja iitwe "KIMBWETE" na vikiwa Vingi viitwe "VIMBWETE". Jina lake likiwa limehusishwa. Prof Mbwete baadae alikuja kuwa Vice Chancellor wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (Open University of Tanzania) mpaka alipostaafu.

Baadae vyuo vingi hapa nchini, viliiga kazi hiyo na kuanza kutumika karibia vyuo vyote hapa nchini. Na hakika imekua msaada mkubwa sana kwa Wanafunzi huko vyuoni.

Naam, hiyo ndiyo historia ya Vimbwete hapa nchini na siyo Vimbweta kama wengi wanavyolitamka.

Nawaomba wanafunzi walioko vyuoni,waanze kutamka kisahihi kulitumia ilivyo sawa ili kuenzi kazi kubwa aliyofanya Prof Mbwete.

Nawasilisha.
Ha ha naona mdegreee paleee
 
Waviwekee socket za umeme tuchaji laptop zetu na kujiburudisha hapo assignment zetu
 
Aisee huu mti wa mdegree wa kitambo lakin hauoneshi hata dalili za kuchoka.
 
Historia umeipindisha. Nilikuwa UDSM wakati vinajengwa hivyo vimbwette.
Usahihi ni kwamba Prof Mbwette aliongoza "University Transformation Program" iliyokuwa na majukumu, pamoja na mengineyo; kuongeza idadi ya wanafunzi wa chuo , kuongeza mapato ya chuo, kujenga miundo mbinu itakayohimili ongezeko la wanachuo.
Kujenga vimbwette kulitokana na ongezeko la mahitaji ya viti kwa ajili ya "kujisomea" au discussions.
Kwa hiyo ni wanafunzi tuliobatiza hilo jina na kwa kweli lilikuwa la dharau (derogatory) sababu wengi hatukuvipenda na hata program yenyewe hatukuipenda sababu iliongeza idadi ya wanachuo bila kuendana na infrastructure zilizokuwepo.
 
Ni kweli mkuu.

Professor Mbwete nimewahi kusoma na kijana wake UDSM pale, ni watu wenye jina kubwa sana lakini very humble.

Anastahili sana kupewa heshima huyu mzee wa kuja na wazo hili.

Hata Project ya kujenga shopping center kubwa ya Mlimani City ililetwa na muhadhiri mmoja na ikapingwa sana na Serikali miaka hiyo, ikabidi chuo kijenge kwa fedha zake, ajabu ilivyoleta mafanikio Serikali imepakumbatia kama pao na jamaa aliyeleta wazo hili na kulipigania kasahaulika kabisa.

Napendekeza watu wanaofanya mambo mazuri na ideas nzuri kama hizi kwa taifa wakumbukwe angalau hata kwa kuenz majina yao kama ilivyofanyika kwa Profesor Mbwete.

Mkuu inawezekana wazo lilikuwa land for equity, hata sasa UDSM sio waliojenga Mlimani City bali walitoa ardhi yao kwa ubia pajengwe Mlimani City Mall na zile apartments.
 
Yap... Mkuu hicho kimbwete kiwekwe chini ya nn na jua lote hili....Ppoz znajaa tu cafe discussion....
 
Sijui haya mazoea yanatokea wapi, watu hujikuta tu wanaviita hivyo lakini jina halisi ni Vimbwete.
Caltex = Shell
BP = Shell
Oilcom = Shell
nk, all are Shell course of mazoea😀!
 
Pamoja na yote hayo, vitaendelea kuitwa vimbweta tu... mazoea na inasaundi vema kuliko vimbwete!
 
Hivyo viti mbona vipo sehemu nyingi tu duniani. Huyo siyo wa kwanza
 
UDOM hamna hivi vitu sijui kwa vile tunaishi porini huku
 
Back
Top Bottom