Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,198
Salaam WanaJukwaa.
Kama wewe ni Mwanafunzi au umepata nafasi ya Kuingia Chuo, bila shaka msamiati wa neno "Kimbwete au Vimbwete" haukupigi Chenga.
Naam, usishangae sana na kudhani nimekosea kuandika. Wengi wamebadilisha jina halisi na kulipachika jina jipya la Kimbweta au Vimbweta. Je, umewahi kujiuliza asili ya jina lenyewe na maana yake? Basi twende pamoja ukapate kulifahamu vema.
Miaka ya Nyuma huko, kulikua na wizi, upotevu na uhamishaji wa viti katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Viti vingi vilikua vinahamishwa katika eneo ambalo vilipaswa viwepo wakati mwingine hata kuibiwa na kuleta Usumbufu wa hali ya juu.
Baada ya kuwa ni jambo lenye Usumbufu mno chuoni hapo, Uongozi wa Chuo ulifanya namna mbalimbali katika kutatua tatizo lenyewe. Tatizo lilikuwa kubwa hasa kiasi cha kufikirisha vichwa vya Wahadhiri na Wanafunzi kwa ujumla.
Katika utoaji wa Mapendekezo, aliyekuwa Mhadhiri Chuoni hapo Prof Tolly Mbwete alitoa pendekezo kuwa yajengwe madawati ya saruji yaani Cement. Wazo au pendekezo lake hilo lilifanyiwa kazi na lilizaa mafanikio makubwa. Lilitoa ufumbuzi wa tatizo husika.
Wazo hilo la Prof Mbwete,lilipunguza kwa kiasi kikubwa kama siyo kumaliza kabisa tatizo husika. Alipongezwa sana kwa wazo hilo na alipandishwa ngazi kutoka Lecturer mpaka Senior Lecturer.
Hiyo ni moja kati ya kazi ya Kitaaluma ya Prof Mbwete. Baadae, alisema hayo madawati yaliyojengwa kwa Saruji, ikiwa kimoja iitwe "KIMBWETE" na vikiwa Vingi viitwe "VIMBWETE". Jina lake likiwa limehusishwa. Prof Mbwete baadae alikuja kuwa Vice Chancellor wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (Open University of Tanzania) mpaka alipostaafu.
Baadae vyuo vingi hapa nchini, viliiga kazi hiyo na kuanza kutumika karibia vyuo vyote hapa nchini. Na hakika imekua msaada mkubwa sana kwa Wanafunzi huko vyuoni.
Naam, hiyo ndiyo historia ya Vimbwete hapa nchini na siyo Vimbweta kama wengi wanavyolitamka.
Nawaomba wanafunzi walioko vyuoni,waanze kutamka kisahihi kulitumia ilivyo sawa ili kuenzi kazi kubwa aliyofanya Prof Mbwete.
Nawasilisha.