Mzee Mohamed Said, wewe umekuwepo wakati wa mkoloni unafahamu fani ya historia ilimopitia, Hegel aliitoa Africa kwenye historia ya walimwengu kwa madai waafrika hatuna akili-raizini, miaka ya 1960 mwanahistoria mwanahistoria mwandamizi - Jumuia ya Madola Prof. Hugh Trevor-Roper aliueleza ulimwengu kuwa hakuna fani ya historia ya waafrika, kabla ya wakoloni Afrika ilikuwa gizani n,k,. Wanahistoria mna viwango na vigezo vinavyokubaliwa na wanahistoria wengi duniani, kama ilivyo kwa fani nyingine. Swali langu kwanini tusizingatie viwango vya kimataifa? Kwangu mimi nadhani inabidi tuiandike historia yetu kwa viwango vya juu zaidi kuliko vinavyotumiwa na wengine.