Historia ya Shule ya Vidudu Mlimani

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,605
1,704
1: Darasa Liloloungua na Kupelekea Selebriti Ahamie Pabliki Inglishi Midiamu

Image0033.jpg

2. Mzambarau alioukwea Selebriti Nyani uko Pembeni ya Darasa Jipya
Image0050.jpg

3. Bembea Zimeongezeka - Enzi za Selebriti Ngabu zilikuwa Chache Sana

Image0035.jpg

----------------------------------------------------------------------------------​
Katika matembezi yangu ya alfajiri huwa napita kwenye shule mbalimbali. Leo nimepita tena katika shule niliyosoma chekechekea. Maswali mbalimbali yalinijia kichwani hasa baada ya mwanafunzi wa zamani wa shule hiyo kudai kuna jengo liliungua. Cha ajabu tulikuwa tukicheza kwenye jengo hilo na kulitumia kama ulingo wa kupigania na kufanya mazoezi ya skauti. Nikiwa mdau nambari wani wa elimu Tanzania na mwanahistoria wa kujitegemea wa Taifa, ningependa kujua haya:

1. Shule hii ilijengwa lini na nani?
2. Kwa nini iliitwa shule ya vidudu?
3. Nini kililiunguza jengo lake la awali?
4. Mbona siku hizi hawaruhusu kuingia?
5. Wadau gani maarufu wamefundwa hapo?

Bahati mbaya sikuweza kupiga picha kwa kuwa simu yangu haina kamera. Punde tu nitakapopata kamera nitapiga baadhi ya picha ili niweze kuzitumia kuuliza maswali vizuri zaidi. Wadau wa shule hiyo naomba mjimwage ukumbini kujibu maswali.
 
Nitaanza na kujibu swali la tano. Mmoja wa wadau maarufu waliofundwa hapo ni mimi wenu mtiifu, The Legendary Nyani Ngabu. Najua Dr. Magimbi pia alifundwa hapo tena kwenye hiyo iliyoungua.

Kuna maprofesa wengine vijana kabisa ambao bado wako kwenye miaka ya 30 ambao pia walifundwa hapo. Maprofesa hawa wapo kuanzia Atlanta, Georgia hadi University of Witwatersrand, Johannesburg, South Africa. Hawa wasomi watakuja kuwa na mchango mkubwa sana katika academia.

Bado nina kumbukumbu ya ung'avu ya muda wangu pale. Nakumbuka saa nne asubuhi ilikuwa muda wa kunywa maziwa. Tena yale maziwa ya kwenye pakiti. Halafu mchana tulikuwa tunaachiwa kwenda kucheza nje na mimi zangu zilikuwa kwenda kwenye mti wa zambarau na kuangua zambarau.
 
kumbe ulisoma pale?lol ila sijui historia yake pia!!
mie nimesoma kuanzia vidudu mpaka std 7 pale pembeni..
 
Nyani Ngabu, unamuongelea Dr. Magimbi kaka yake Salma - Udokta wa MD na/au PhD?

Naomba contacts zao hao young profs, tunahitaji warudi nyumbani asap kujenga taifa!

Da ule mzambarua nadhani nao bado upo, nitaucheki vizuri kesho; mwembe bado upo.
 
Yep...Magimbi, MD....

Ila hao ma young profs sidhani kama wataiweza mishahara ya hapa nyumbani.
 
NN, mzambarau bado upo,halafu kumbe kuna mbuyu, halafu kuna yale matunda kama mabungo kule nyuma, tulikuwa tunafanya kitenesi; nimepata kamera leo, nikiweza kesho nitaweka snepu humu - yale mabwawa 7 sasa yana mvuto wa ajabu hata siwezi kuelezea, subiri picha!
 
Ebana eeeh umenitamanisha sasa. Ngoja na mimi kukicha lazima niende nikapacheki. Halafu kule mabwawa ya 7...duuuuh umenikumbusha mbali sana. Nako itabidi niende....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom