hivi mtu akiuudhi kununa ndo suluhisho? Mume hanuniwi ulikosea tangu mwanzo kama kakosa kaa nae chini mwambie 1,2,,3 sijapenda baada ya hapo kama anajirekebisha maisha yanasonga kama kawa na mwanaume asiechepuka hapa duniani ni moja ya kumi baada ya kugundua anachepuka usingenuna ungesuluhisha sidhani kama mngefika mahakamani
wanaume wengine ni headache tu pambafff pole....
bora mazimwi ya humu hata akitueleza hatuwezi kumsambaza kuliko ya uraiani
Upo sahihi ila huyu Mwanaume mwenzangu kazidi aisee(kama haya yasemwayo kweli). Yani unafumaniwa halafu una nuna wewe,duh! Mbaya zaidi unanyogewa mpaka hela ya matumizi ya watoto hutoi!!
Kwa upande wangu bora hawa unaowaona mazimwi kuliko hawa wanaonizunguka,amini nimepumua kweli
Asante sana
Lakini si umeona mwenyewe kasema "Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote .Asanten"
Kwa hiyo hata mazimwi ya humu nayo huwa yana mambo mpaka imembidi aje na alternate ID la sivyo angeweza kutangazwa huko kwenye PM.
nuna mchepuko unazidisha manjonjo zaidi mafahari wawili hawakai zizi moja
Pole dada!ndoa ni agano la milele kununa si suluhisho bali kukaa na kuyaongea huku ukimtegemea mungu yaani mtangulize mungu ktk kuomba.Inavyoonekana mume wako hana hofu ya mungu
aiseeee nilikuwa sijasoma hapo chini afu mazimwi ya humu nayo mtu humjui hakujui kusambazana sijui inasaidia nini? ni kukosa kazi
Kwa nini umekuja na alternate ID....?
Hapo sasa.....imagine yangekuwa yanajua watu.
Ni upumbavu tu.
tungekuwa tunajuana sijui ingekuwaje ila ukiona mtu anakusambaza jua kuna kitu umemzidi
Nimeamua tu ili baada ya kuutua huu mzigo niliokuwa nao moyoni, niweze kuchangia mada zingine kama kawaida
Haya mambo ni marahisi kwa kumshauri mwingine...
Unadhani likikukuta utakumbuka kuwa ukinuna ataenda kwa mwingine...akili hapo haifanyi kazi kabisa...
Kila siku unakuja na mkakati mpya wa kumtibua...
Ila ndio tujue kuna tofauti kati ya mwanaume na mwanaume...
Mwanaume anayependa familia yake...yuko tayari kufanywa chochote na ahami...
Anakupa muda ili uponye maumivu...
Sasa wanaume jeuri; kosa kafanya afu anageuka mbogo...lazima ndoa ivunjike...
Na hata ningekuwa mimi wife wala sijutii kuvunja ndoa ya mume kama huyo...
Kuchiti ni kosa kuuubwa sana...mwache mkeo atoe hasira zake atakavyo...
Haya, kila la kheri.
Ni kweli ukiongea mtu unajisikia umetua mzigo...hata ukiongelea kwenye chungu...
Ila sasa kama mmenuniana miaka 5 imekuwaje mna watoto 3?
Kingine ameondoka kuelekea wapi?
Kama ana tabia za hovyo huko alikoenda nako atatoka dima...atakuwa mtu wa kuhama hama...
Ila hapo mbona ndoa imeshakwisha...mtu kaondoka mwenyewe...hakuna ndoa hapo...lea wtoto..jipe raha kila upatapo nafasi...