Asante na naendelea kujifunza kitu, haswa kwamba Kenya tuna umiliki mkubwa wa Kiswahili, lakini hebu nipe elimu mbona ikawa kimekopa sana maneno ya msingi kutoka lugha zingine, kwa mfano tu neno "damu", ina maana Waswahili hawakua na neno mbadala.
Nimeuona na nnajifunza mengi sana.
Waswahili walikuwa na tabia ya kukopakopa halafu wakaja wengi wanaojifanya ndo waswahili wakajaza maneno ya kwao.
Kwa Kingozi ( Kiswahili kikongwe) neno lilikuwa likitumika badala ya 'damu' ni NGEU.
Asante dadangu, Kiswahili kilikuwepo kabla ya Waarabu kuingia Pwani ya Afrika Mashariki, Wabantu walikuwa wanajua kuhesabu, walikuwa wanapeana majina na sio haya ya Mohammed, Said, waliwapa Wanyama wote Majina , kwa Ufupi Waarabu walikuta kuna Lugha iliyokamilika,
Maneno karibu yote ya Kibantu yaliyo ndani ya Kiswahili unayapata ndani ya Lugha ya Kishona ya Zimbabwe, Lingala ya DRC nk
Umeanza sasa,Usichanganye kati ya Kiswahili na Kimvita.
Usichanganye kati ya Kiswahili na Kimvita.
Wewe ndiyo umeanza unajifanya kutoa darsa nakushauri kuwa msomaji tu utajifunza mengi.Umeanza sasa,
Wewe ndiyo umeanza unajifanya kutoa darsa nakushauri kuwa msomaji tu utajifunza mengi.
Umeanza sasa,
nimependa historia kuna maneno mimi siyaelewi mfano hilo neno mbari